Feedback
JF-Expert Member
- Mar 14, 2011
- 7,988
- 4,508
Usipojiheshimu usitegemee kuheshimiwa.
"Mdee kikalishe"
"hivi kati ya Wenje na Masha nani mwanamke" nilimsikia Spika akitamka.
Kwa wanaomtetea Ndugai hebu mtueleze haya maneno yalistahili kutamkwa na kiongozi mkuu wa moja ya mihimili yetu? Kweli?
Mfano wewe ni binti halafu unamsikia baba yako akikwambia hebu na wewe "kikalishe" utajisikiaje au baba anawaambia vijana wake wa kiume kati yenu nani mwanamke. Definitely haya sio matamshi mazuri kutamkwa na mtu mwenye heshima na busara, kwa sababu si kwamba tu yanamdhalilisha anayeambiwa bali yanamdhalilisha hata yeye.
Kwa case ya juzi Ndugai amekidhalilisha kiti cha spika, nasema kakidhalilisha kiti kwa sababu kuna siku Naibu spika anaweza kuambiwa the same na wabunge.
Ni kweli Mdee alikosea lakini inawezekana aligadhabika kutokana na yeye kudhalilishwa na kwa haraka haraka akaona neno 'fala' linaweza kuwa ndilo sahihi na lenye uzito sawa na alivyoambiwa.
Je, kamati ya bunge ya nidhamu ina uwezo wa kumuita spika kujieleza? Kama kamati haina uwezo na hatuwezi kumlazimisha mtu kujiheshimu basi itafutwe mechanism yeyote ya kumlazimisha angalau akiheshimu kiti.