VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Maisha hayatabiriki. Maisha yana mambo mengi ya ajabu na yenye kutoa majibu.
Maisha yanakwenda kasi sana. Job Yustino Ndugai, Mbunge wa Kongwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yamemfika.
Yamemkuta na amefikishwa kwenye ukuta. 'Ameropoka'; akajitetea, akaomba radhi lakini hakukubaliwa.
Rais 'kumjibu' kwa 'kumtaja' hadharani inamaanisha kuwa msamaha haukutolewa.
Lazima jambo liwe.
Ndugai na historia ya kuukandamiza upinzani Bungeni. Tangu mwanzoni mwa utawala wa Mwendazake na baada ya Ndugai kupokea maelekezo ya kuwashughulikia wapinzani ndani ya Bunge na nje kuachwa Mwendazake mwenyewe, Ndugai alikuwa mahiri bila ubahili katika kusimamia maagizo kutoka juu katika kuwashughulikia wapinzani.
Aliwafukuza kutoka Ukumbi wa Bunge Wabunge wa upinzani; aliwaburuza Kamati ya Maadili; aliwasimamisha kwa tambo wahusika na hata kuwatisha.
Kilele cha yote ni pale alipomvua kikatili Ubunge Tundu Lissu.
Ndugai aliona ameyapatia. Aliona amefika. Alikuwa akicheka kwa mateso ya wenzake na kukasirika kwa mafanikio ya wapinzani Bungeni. Upinzani ukafika tamati Bungeni mwaka 2020 baada ya 'uchafuzi mkuu' wa mwaka huo.
Upinzani ukafutwa Bungeni. Ndugai akafurahi sirini na hadharani.
Akakiona kiti cha Spika rahisi na chepesi kuliko nyasi katika kukiongoza bila kuunguza.
Akaendelea kuwakera wapinzani kwa kuwaapisha na kuwakumbatia Wabunge haramu 'wa CHADEMA' wakiongozwa na Halima Mdee.
Leo, karma imemrudi Ndugai.
Haaminiki.
Hatakiwi.
Hapendwi.
Hathaminiki.
Haeleleweki.
Hapokelewi simu zake wala kujibiwa jumbe zake.
Hapewi ushirikiano na wale alioamini walikuwa wakimfurahia.
Amekwama. Anahema. Anazama. Amekuwa mpinzani wao Bungeni.
Amekuwa mpingaji wao chamani. Amekuwa mpinzani wao sirini na hadharani.
Upinzani umefufuka Bungeni kupitia yeye. Hakika, karma is real!
Spika Ndugai asithubutu kuongoza kikao chochote cha Bunge.
Akifanya hivyo, hataupenda mwisho wake utakaorushwa mubashara runingani.
What goes around, comes around!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)