Spika na double standard yake kuhusu rostam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika na double standard yake kuhusu rostam

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by politiki, Jul 21, 2011.

 1. p

  politiki JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  spika anadai anasubiri barua kutoka kwa chama ili aweze kutambua kujiuzulu kwa Rostam na kwamba
  barua ya rostam pekee haitoshi kutangaza kuthibitisha kujiuzuru kwake. lakini kwenye miaka ya 90, CUF ilishawahi
  kumfukuza mbunge uanachama na kumuandikia spika wakati huo kama sikosei alikuwa msekwa kumtaarifu kuwa
  kama sikosei mbunge huyo jina alikuwa anaitwa NAILA JIDAWI kuwa siyo tena mwanachama wao na hastahili kuwa
  mbunge tena lakini spika alikataa kutambua barua ya chama na Naila jidawi akaendelea na ubunge wake. kuna utata hapa.

  mwingine diwani wa chadema huko mbeya aliandika barua ya kujiuzulu kwa meya na baadaye aliandika barua nyingine
  kufuta barua yake ya kwanza ya kujiuzulu lakini meya amekataa anadai kwa kuwa diwani alishaandika barua ya kujiuzulu
  hiyo pekee inatosha na ktk hili haikusubiriwa barua ya kutoka kwa chama wala nini ? hii si double ya nguvu. inakuwaje
  ndani ya nchi moja kuwe na sheria mbili tofauti na itafisiliwe kulingana na mazingira yaliyopo. naomba msaada wa ufafanuzi
  jamani!.
   
 2. T

  Technology JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 733
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  wewe unatakaje? Rostam aendelee kuhudhuria vikao vya bunge??? hebu watanzania tubadilike...hivi unataka sisi tuache kufikiria mambo muhimu tuanze kujadili issue ya Rostam aliejiuzulu!!!!! will it make life different??/
   
 3. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwan huyo diwani wa chadema alikuwa chizi mpaka anajikanganya hivo?inaƶnekana huyo alishinda kwa upepo wa dr slaa,sawa na wale wa arusha,maskini cdm!....eti hata diwani anakitunishia msuri chama,ukishangaa ya musa....
   
 4. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mkuu RA kama ulimsoma vizuri MM Mwanakijiji amesema kuwa kafanya hivyo kukinusuru chama na sio nchi na ndio sasa inadhihirika hilo sasa kwa huyu mh makinda..
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Barua ya Rostam Azizi ya kujuizulu iko kwenye ukarasa wa mbele (front page) ya Mwanahalisi -July 20, 2011. Kwa maneno mengine watanzania wapatao takribani elfu kumi waliosoma hili gazeti week hii wanajua reference number ya barua na contents zake zote. Spika Makinda mwenye access ya kila kitu anasema hajapata barua! Hivi ni kweli hajapata barua au hataki kupata hii barua? Na kama kweli haijafika kwake haoni umuhimu wa kutaka maelezo juu ya swala hili maana Rostam kakaririwa na vyombo vyote vya habari nchini (including TBC) akitangaza kujuzulu?

  Why can't she lift her bam and ask what is going about a member of the parliment? Tabia ya viongozi wetu kusubiri kila kitu kiwe mezani inatia kinyaa. Takukuru hanyanyuki mpaka aletewe ushahidi? polisi hasogei mpaka apate usafiri, waziri (i.e Chikawe) hataki kuchunguza wizi mpaka aletewe ushahidi!

  Kwa maoni yangu, kwa kiongozi yeyote kutojua nini kinachoendelea kwenye 'ulingo' wa kazi au ofisi yake ni uzembe na hafai kuwepo kwenye nafasi hiyo. Kwa spika kutokuwa na barua au kujuwa kujiuzulu kwa mbunge ni udhaifu usiokubalika na inaleta picha ya wasiwasi kuwa she doesnt know anything so how can she lead? Yaani mzazi unalala ndani huku hujui kama watoto wote wapo nyumbani au la!!! Pengine Spika angeacha kujifundisha namna ya kujibu hoja za serikali na kujikita zaidi kwenye kazi za bunge basi angekuwa amepata taarifa kamili juu ya kujiuzulu kwa mbunge. Awasiliane na KUBENEA. He knows something!
   
 6. p

  politiki JF-Expert Member

  #6
  Jul 21, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  mheshimiwa spika ameshakiri kama amepokea barua kutoka kwa RA, utetezi wake mpya hivi sasa ni kuwa hajapokea barua kutoka kwa chama.
   
Loading...