Amesisitiza hajawekwa na mtu, hamtumikii mtu na hawezi kuondolewa na mtu, ametangaza 2015 hagombei Ubunge, anastaaafu.
Press Conference imeisha, anaelekea bungeni sasa.
Slowly madam speaker, thats a misdirection read Article 84 (7) of the constitution
Spika atakoma kuwa Spika na ataacha kiti cha Spika litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo
(a) iwapo mtu huyo alichaguliwa kutoka miongoni mwa Wabunge, basi ikiwa
atakoma kuwa Mbunge kwa sababu yoyote ambayo haihusiki na kuvunjwa
Bunge; au
(b) ikiwa kutatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa Spika
lingemfanya mtu huyo asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za
uchaguzi wa Spika; au
(c) Bunge litakapokutana kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu
uliofanywa baada ya Bunge kuvunjwa, lakini masharti ya aya hii yatatumika
bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (4) ya ibara ya 90 ya Katiba hii;
au
(d) ikiwa mtu huyo ataondolewa kwenye madaraka ya Spika kwa azimio la
Bunge lilioungwa mkono na Wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi
mbili ya Wabunge wote; au
(e) ikiwa mtu huyo atashindwa kuwasilisha kwa Rais tamko rasmi kwa mujibu
wa masharti ya ibara ndogo ya (3) ya ibara hii; au
(f) ikiwa mtu huyo atapatikana na hatia kwa kosa la kutoa habari za uongo,
kwa kiapo kinyume cha sheria ya Kanuni ya Jinai, kuhusu tamko rasmi
lolote lililotolewa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) ya ibara
hii; au
(g) ikiwa mtu huyo huyo atashindwa kuwasilisha kwa Rais taarifa ya mali kwa
mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (5) ya ibara hii kabla ya kumalizika
muda uliowekwa kwa ajili hiyo kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge;
(h) ikiwa itathibitika kuwa mtu huyo amevunja masharti ya Sheria ya Maadili
ya Viongozi wa Umma.