Spika Makinda abebwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika Makinda abebwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kilimasera, Apr 28, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, amejitosa ulingoni kujibu mapigo ya wakosoaji wa utendaji wa Spika wa Bunge, Anne Makinda, wanaodai kwamba kazi hiyo imemuelemea.

  Kujitokeza kwa Dk. Kashililah kunatokea siku chache baada ya kuwapo kauli tofauti juu ya utendaji wa Makinda, baadhi wakisema ameshindwa kumudu mikiki mikiki ya Bunge hilo lililojaa vijana, huku wengine wakisema kwa hali ilivyo ni vema Spika akawa na taaluma ya sheria.

  Makinda alisomea uhasibu, ingawa amekaririwa akisema kuwa anajua sheria pia na kwamba ana uzoefu mkubwa wa masuala ya Bunge ambako amekuwako kwa takribani miongo mitatu sasa.
  Dk. Kashililah alijitokeza jana jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari aliouitisha kuzungumzia mambo mbalimbali ya utendaji wa Bunge.

  Pamoja na kumtetea vikali bosi wake kuwa mwenye busara, uwezo na uzoefu wa kuongoza muhimili huo wa madaraka ya dola, alisema vurugu zinazotokea ndani ya vikao vya Bunge zinatokana na umbumbumbu wa wabunge wapya kuhusu kanuni zinazoongoza chombo hicho cha kutunga sheria.

  Vile vile, alisema Spika Makinda hajashindwa kuzidhibiti ila amekuwa akitumia busara zaidi katika kuliendesha Bunge badala ya kutumia nguvu.

  Dk. Kashililah alisema asilimia 70 ya wabunge ni wapya na wengi wao hawajui kanuni zinazosimamia vikao vya Bunge, hivyo kujikuta wakifanya makosa mbalimbali ambayo bila busara ya Spika wengine wangeshasimamishwa kuhudhuria vikao.

  Alisema wabunge wengi ni vijana ambao hawajawahi kufanya kazi serikalini wala kushiriki mijadala mikali na makongamano, hivyo kuwepo kwao bungeni kunahitaji uvumilivu na kuwapa msaada mkubwa.

  Alisema wengi wamekuwa wakifanya makosa ambayo yangewafanya wasimamiswe hadi vikao kumi, lakini Spika amekuwa akitumia busara zaidi katika maamuzi yake.

  "Wabunge wengi ni wapya, hawajui kanuni na hii ni hali ya kawaida kabisa miaka yote wabunge wapya wanakuwa hivi hivi, lakini baadae wanazoea na mambo yanakwenda kama kawaida, sasa ndiyo maana Spika anaamua kutumia busara zaidi na ameamua kuwavumilia hadi watakapokomaa maana anasema kuwaadhibu kwa sasa ni sawa na kutowatendea haki," alisema Dk. Kashililah.

  Alisema Spika Makinda si dhaifu kama baadhi ya watu wanavyoweza kudhani kwani amekuwa bungeni kwa sehemu kubwa ya maisha yake na anajua vyema namna ya kusimamia vikao vya chombo hicho.

  "Spika ana uzoefu wa kutosha kabisa kuliendesha Bunge, anajua kanuni vilivyo ila kama nilivyosema ameamua kutumia busara zaidi badala ya kuwaadhibu wabunge wanaokosa, mamlaka ya kuwasimamisha anayo mbona amewahi kufanya maamuzi mazito alipokuwa Naibu Spika, lakini hana papara katika maamuzi yake anawalea hadi watakapokomaa" alisema.

  Alisema Bunge limejitahidi kuwapa semina elekezi wabunge wapya kuhusu kanuni na litaendelea na kazi hiyo hadi litakapothibitisha kuwa wengi wameelewa kanuni za Bunge na wanaweza kuzifuata katika shughuli zao za kila siku.

  Alisema hata Spika aliwahi kusema kuwa itachukua muda mrefu kwa wabunge hao wapya kujua kanuni na taratibu zinazoongoza chombo hicho na hatimaye wafanye kazi zao bila jazba.

  "Mfano unajua kanuni za Bunge haziruhusu Mbunge kusoma hotuba mle kwenye vikao, lakini baadhi wamekuwa wakifanya hivyo na Spika anawarekebisha kidogokidogo wanaanza kuelewa," alisema.

  "Kwa kanuni za Bunge Spika akisimama, yule anayezungumza awe mbunge ama waziri anapaswa kukaa chini na asipotii Spika ana mamlaka ya kumwita Sergeant at-arm na kumtoa nje, lakini si mmeona wenyewe kwenye baadhi ya vikao Spika anasimama na wabunge zaidi ya kumi nao wanasimama na wote wanazungumza, lakini katika hayo yote Spika anaamua kutumia busara kwa kutambua kuwa hawajui vyema kanuni, ukiwatoa nje hutakuwa umewatendea haki," alisema.

  Alimtetea Mbunge wa Iramba Magharibi, (Chadema) Tundu Lissu, kuwa amekuwa mdadisi sana wa masuala ya kanuni za Bunge hivyo wananchi wasitafsiri kwamba mbunge huyo ni mkorofi.

  "Anachofanya Lissu bungeni huwezi kusema kuwa ni fujo maana anapozungumza huwa anarejea kanuni kutaka kupata ufafanuzi wa baadhi ya mambo, ingawa wakati mwingine anaweza kupotea kidogo, lakini huwezi kusema analeta fujo, mle bungeni hata akiingia Jaji katika masuala ya kanuni hawezi kujua kila kitu," alisema.

  Kuhusu muswada wa kuunda tume ya kuratibu maoni ya Katiba, Dk. Kashililah alisema serikali haikuwa na haja ya kuuwasilisha kwa hati ya dharura bungeni.

  Alisema muswada huo ungeweza kuwasilishwa tu bila hati hiyo kwani ulishatimiza sifa kwa kuwa ulishatangazwa gazetini kwa siku 21 kabla ya kuwasilishwa bungeni.

  "Sheria inasema muswada kabla ya kuwasilishwa bungeni utangazwe kwenye Gazeti la Serikali siku 21 kabla ya kuwasilishwa, na ule ulishatangazwa ndani ya muda huo, lakini kwa kuwa hati ya dharura ilishaandaliwa hakukuwa na namna," alisema.
  Alielezea masikitiko yake kwa baadhi ya watu kuuchana muswada huo wakati wa mijadala wakati walichotakiwa kufanya ni kutoa maoni yao.

  Spika Makinda amekuwa akionekana kuboronga kwenye baadhi ya mambo bungeni na moja ya mifano ni namna alivyolichukulia suala la Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema.

  Wakati wa Mkutano wa pili Februari 10, mwaka huu, Lema alitaka kujua hatua ambazo mbunge anaweza kuchukua kama akiona kiongozi mkubwa kama Waziri Mkuu analidanganya Bunge.

  Kauli ya Lema ilitokana na majibu ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akijibu maswali ya papo kwa papo kuelezea chanzo cha vurugu za kisiasa za Januari 5, mwaka huu mjini Arusha zilizosababisha vifo vya watu watatu.

  Baada ya Pinda kujibu maswali hayo kutoka kwa Kiongozi wa Upinzani bungeni, Freeman Mbowe, Lema alisimama na kutaka mwongozo wa Spika juu ya suala hilo, ndipo Spika Makinda aliposimama na kuwa mkali akionekana kukerwa na kauli ya Lema, huku akisema ni lazima Bunge liwe na adabu.

  Alimwambia Lema kwa kauli yake alimaanisha kuwa Waziri Mkuu Pinda kwa maelezo ya serikali bungeni alikuwa amelidanganya Bunge.

  Hivyo, alisema mwongozo aliokuwa anautaka Lema atawajibika kuwasilisha vielelezo bungeni vya kuthibitisha kauli yake ndani ya siku tano kuwa Pinda alikuwa amelidanganya Bunge.

  Hata hivyo, Februari 14, mwaka huu Spika hakusema chochote kuhusu suala la Lema hadi alipoulizwa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, ndipo aliposema kuwa Lema alitakiwa kuwasilisha ushahidi wake kwa maandishi ofisini kwa Spika.

  Hadi sasa Makinda hajalitolea uamuzi suala hilo.

  Wiki iliyopita, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kilitoa taarifa yake kwa vyombo vya habari kikidai kuwa ufuatiliaji ulioufanya wakati wa Mkutano wa Bunge uliopita, ulibaini kuwa pamoja na mambo mengine, Spika Makinda ni dhaifu katika kuliongoza Bunge.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kashllila ndio nani tena; wasifu wake na kachomokea wapi vile????
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,631
  Trophy Points: 280
  Huyu akili zake si afadhali ya makinda wala sikuona ajabu ...kama mnalikumbuka hili jamaa liliambiwa swala la katiba likadai hao wanaopiga kelele awajui umuhimu wake serikali sio chizi ikae kuandika na kuleta mapema nakuhakikishia itappitishwa na wabunge wengi .....

  Ninyi wafanyakazi wa bunge akili za wake zenu mnawaletea watanzania mbele tv amwoni aibu na mkeo akikwambia kamwoshe mkwewe anenda huyu akili zake sidhan kama zimetimia
   
 4. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  hapo penye red ni aje? hao wamama wa watu wamekosa nini, kama upumbavu ni wakwao wenyewe usiwaingize watu wengine.
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,631
  Trophy Points: 280
  MKUU MAMENGAZI
  Unajua kuna raisi alikuwa akitupeleka tegeme na mkewe ameamkaje siku hiyo hawa wamama waache kama walivyo ndio maana nikasema anaweza akawa si yeye kama si ya mkewe basi ana spiritua husband anamsumbua
   
 6. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hapa Katibu wa Bunge anataka watanzania waamini kuwa zile kodi zetu zilizotumika kwnye semina za wabunge kabla ya kuanza bunge zilienda holaa au kunyamaza na suala la uongo wa Pinda ndiyo busara! Spika kazi haiwezi hasa wakati huu ambapo wananchi wamechoshwa na longo longo ya ccm na watu wanataka mabadiliko makubwa panahitaji mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuelewa mambo katika kuliongoza bunge.
   
 7. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #7
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,036
  Likes Received: 3,068
  Trophy Points: 280
  Asubiri List of shame ijayo lazima huyu mcheza makida makida Makinda atakuwemo,kama leo bunge la3 anaoja haya yanayotokea ni ugeni na umbumbumbu wa kanuni za bunge tusubiri sijuhi vikao vya 5,6,7...atatwambiaje,ama ndo atasema sasa wamezielewa mpaka zimewalevya,ama itabidi atwambie kama yeye si mbumbumbu ni nani
   
Loading...