Spika Job Ndugai, Naibu Spika Tulia Akson Mwansasu, lazima UKAWA wanyooke

Ndugai lazima awanyooshe. Wakileta za kuleta anawatandika na siwa

Patawaka moto! ukawa jiandaeni kwenda vitani sio bungeni

Nashindwa kuelewa uelewa mdogo ulioko JF kwa sasa! Kwa nini munashangilia kwa mtindo wa kuzomea? Kwa nini munaona kama Kazi ya Spika ni kukomesha UKAWA?

Vijana wekeni nguvu kwenye akili. Siyo kila kitu ni mpira wa kukabana na kufunga magoli. Hilo ni Bunge na tunahitaji hoja za kujenga nchi. Ninyi bado munawaza kuzomea UKAWA. we want action!
 
kwa taarifa tu ndugai ndiyo atanyooka na bunge lilopita upizani walimnyosha mpaka bunge likawa linamshinda yaani tundu lissu,mnyika,mdee,sugu,jay,cuf ndani ndugai atanyooka heeeeeee!
 
Mchakato wa Naibu Spika unaanza leo. Tulia atachukua fomu na ndiye atakayeteuliwa kuwa Naibu Spika. Bahati nzuri mchakato wa Naibu Spika unaishia ndani ya CCM tu. Naibu Spika hapigiwi kura Bungeni

Unadhani watapitisha jina lake kwa sababu ya uwezo wake au jinsia?
 
Wadau,

Sina shaka na uwezo wa Job Ndugai kusimamia bunge. Amefanya hivyo akiwa Mwenyekiti wa Bunge na hatimaye kuwa Naibu Spika. Nina hakika kwa sasa akiwa Spika wetu bunge litakuwa mtetezi wa wananchi badala ya kugeuka kuwa ukumbi wa mipasho na majigambo.

Wasiwasi wangu ulikuwa kwa Naibu Spika. Kwa mujibu wa kanuni za Bunge, Spika anaweza kuwa Mbunge au asiwe Mbunge. Ila kwa upande wa Naibu Spika, nadhani ni lazima awe Mbunge. Kwa vile kwa upande wa Spika tayari tunaye Job Ndugai, nilitamani sana Tulia Akson awe Naibu wake kutokana na umahiri wake wa kujua sheria. Ila kikwazo kikawa ubunge.

Leo Dr Magufuli kanifurahisha sana. Kumteua Tulia kuwa Mbunge maana yake ni kwamba anaqualify kuwa Naibu Spika. Naam. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Natamani iwe hivyo ili bunge letu liwe ni msaada kwa wananchi. Hakika ikitokea hivyo nitalala kabisa usingizi.

Nataraji Wabunge wa CCM hawatatuangusha. Spika ni Job Ndugai na Naibu Spika ni Tulia Akson. Wabunge wa CCM zingatieni ushauri huu.

Mungu awatangulie mnapofanya maamuzi kwa manufaa ya taifa hili
job ndugai ana kashfa ya kupiga mwenzake na fimbo kichwani hadi kuzirai, vipe awe spika? CCM sasa inatufanya mazezeta sisi, Mungu atawaona kombamwiko hawa, inshallah tutakutana mbinguni. Siku hiyo ya hukumu tumbili, nyani na nguruwe na dhambi zao na mahindi yao mdomoni, na CCM nayo na dhambi zao na masanduku yao ya kura vichwani mwao bila kuruhusiwa kuyashusha chini milele. Ndugai sio mfano mzuri ndani ya jamii kiasi cha kupewa uspika.
 
Wadau,

Sina shaka na uwezo wa Job Ndugai kusimamia bunge. Amefanya hivyo akiwa Mwenyekiti wa Bunge na hatimaye kuwa Naibu Spika. Nina hakika kwa sasa akiwa Spika wetu bunge litakuwa mtetezi wa wananchi badala ya kugeuka kuwa ukumbi wa mipasho na majigambo.

Wasiwasi wangu ulikuwa kwa Naibu Spika. Kwa mujibu wa kanuni za Bunge, Spika anaweza kuwa Mbunge au asiwe Mbunge. Ila kwa upande wa Naibu Spika, nadhani ni lazima awe Mbunge. Kwa vile kwa upande wa Spika tayari tunaye Job Ndugai, nilitamani sana Tulia Akson awe Naibu wake kutokana na umahiri wake wa kujua sheria. Ila kikwazo kikawa ubunge.

Leo Dr Magufuli kanifurahisha sana. Kumteua Tulia kuwa Mbunge maana yake ni kwamba anaqualify kuwa Naibu Spika. Naam. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Natamani iwe hivyo ili bunge letu liwe ni msaada kwa wananchi. Hakika ikitokea hivyo nitalala kabisa usingizi.

Nataraji Wabunge wa CCM hawatatuangusha. Spika ni Job Ndugai na Naibu Spika ni Tulia Akson. Wabunge wa CCM zingatieni ushauri huu.

Mungu awatangulie mnapofanya maamuzi kwa manufaa ya taifa hili
Hapa ndipo Watanzania mnapokosea.

Bunge ni chombo cha wananchi na si CCM. Unapowataka wabunge wa CCM wafuate ushauri wa kumchagua mtu wao, tayari unajenga mpasuko, na unaondoa maana halisi ya kazi za bunge

Unaposema hivyo unamuondolea huyo unayempigia debe ''Tulia na Ndugai'' ile nguvu ya kutumia weledi wake wa sheria kuongoza mambo ya kitaifa. Tayari unamkabidhi awe loyal kwa CCM na si bunge! Wrong! wrong!

Hiyo Tanzania unayoitaka haiwezi kujengwa kukiwa na mpasuko na mgawanyiko unaopigiwa debe kwa sasa
Hivi hamuoni tulivyo leo hii? Lini Taifa letu limekuwa hivi? Hii ndiyo Tanzania tunayoijua sote?

Wabunge wanapokuwa bungeni ni wa wananchi na si wa vyama.

Hii dhana ya wabunge wa CCM na upinzani ni mwendelezo wa akili zetu zilizovia.

Akili zinazoamini itikadi na si Utaifa. Inasikitisha inatisha

Kumbuka, Rais anbakabiliwa na mgawanyiko mkubwa wa umma, taifa lsisilo na furaha na kuungwa kwake mkono kwenye mashaka.

Unapoweka maneno kama haya unazidi kujenga ufa katika taifa lenye ufa mkubwa sana

Nchi haijengwi na chama au mtu bali watu. Awamu ilyopita ilijaribu uchama, matokeo ikafeli hata kuongoza Taifa kuandika katiba.

Ikafeli mambo mengi sana kwasababu ya kukosa kuungwa mkono. Hilo halina tija kwa Taifa bali maumivu tu.

Tutabaki kusema Wenzetu Kenya, Ethiopia n.k. wanasonga mbele

Tutatafuta wachawi kumbe wachawi ni sisi wenyewe. Haya mambo ya uchama ni mabaya sana.

Yameliharibu Taifa na sasa tumebaki Simba na Yanga.

Usimba na Uyanga haujasaidia vilabu hivyo tangu miaka ya 1934.

Hatujifunzi tunaendelea na bla bla kesho asubuhi tunalalamika wenzetu wanatuacha
 
Heading yako,kwani bungeni tunaenda kuwanyoosha UKAWA?Tutakaonyooka au kupinda ni sisi malofa huku kitaa

.....hivi ndo vitu vinavyowafanya watanzania wanaichikia ccm......watu wanaoitetea ccm hawazungumzi ktk kuwaunganisha watanzania wengi wao wanazungumza kulinda matumbo yao......sasa ukawa wakinyooshwa na viongozi wa bunge watanzania wanaowakilishwa na hao watu watanufaika na nini!?!?
 
Huyo Ndugai hana impact yoyote ateendeleza uccm kwenye mambo ya taifa na bunge si sehemu ya mipasho.

Mtu kilaza ndio atakwenda kuleta ushindani wa vyama tunahitaji majadiliano ya hoja ili kuliondoa taiga letu hapa tulipo.

So hiyo kauli ya ndugai akiwa spika UKAWA watanyooka ni fikra ya MTU kilaza.
 
Hapa ndipo Watanzania mnapokosea.

Bunge ni chombo cha wananchi na si CCM. Unapowataka wabunge wa CCM wafuate ushauri wa kumchagua mtu wao, tayari unajenga mpasuko, na unaondoa maana halisi ya kazi za bunge

Unaposema hivyo unamuondolea huyo unayempigia debe ''Tulia na Ndugai'' ile nguvu ya kutumia weledi wake wa sheria kuongoza mambo ya kitaifa. Tayari unamkabidhi awe loyal kwa CCM na si bunge! Wrong! wrong!

Hiyo Tanzania unayoitaka haiwezi kujengwa kukiwa na mpasuko na mgawanyiko unaopigiwa debe kwa sasa
Hivi hamuoni tulivyo leo hii? Lini Taifa letu limekuwa hivi? Hii ndiyo Tanzania tunayoijua sote?

Wabunge wanapokuwa bungeni ni wa wananchi na si wa vyama.

Hii dhana ya wabunge wa CCM na upinzani ni mwendelezo wa akili zetu zilizovia.

Akili zinazoamini itikadi na si Utaifa. Inasikitisha inatisha

Kumbuka, Rais anbakabiliwa na mgawanyiko mkubwa wa umma, taifa lsisilo na furaha na kuungwa kwake mkono kwenye mashaka.

Unapoweka maneno kama haya unazidi kujenga ufa katika taifa lenye ufa mkubwa sana

Nchi haijengwi na chama au mtu bali watu. Awamu ilyopita ilijaribu uchama, matokeo ikafeli hata kuongoza Taifa kuandika katiba.

Ikafeli mambo mengi sana kwasababu ya kukosa kuungwa mkono. Hilo halina tija kwa Taifa bali maumivu tu.

Tutabaki kusema Wenzetu Kenya, Ethiopia n.k. wanasonga mbele

Tutatafuta wachawi kumbe wachawi ni sisi wenyewe. Haya mambo ya uchama ni mabaya sana.

Yameliharibu Taifa na sasa tumebaki Simba na Yanga.

Usimba na Uyanga haujasaidia vilabu hivyo tangu miaka ya 1934.

Hatujifunzi tunaendelea na bla bla kesho asubuhi tunalalamika wenzetu wanatuacha

Mkuu, katika mfumo wa vyama vingi popote duniani,huwezi kuzuia hisia za kisiasa kwa itikadi za kichama. Ndo maana wapinzani wana mwamvuli wao wanaouita UKAWA na wamesimamisha mgombea mmoja kupambana na wa CCM. Katika mazingira hayo, usitegemee kwamba spika atakayepatikana awe wa CCM ama upinzani atakuwa na mizani sawa kwa vyama vyote. Huo ndo ukweli hata kama hutaki kuusikia
 
Huyo Ndugai hana impact yoyote ateendeleza uccm kwenye mambo ya taifa na bunge si sehemu ya mipasho.

Mtu kilaza ndio atakwenda kuleta ushindani wa vyama tunahitaji majadiliano ya hoja ili kuliondoa taiga letu hapa tulipo.

So hiyo kauli ya ndugai akiwa spika UKAWA watanyooka ni fikra ya MTU kilaza.

Msipost hoja sizizo na weledi wa kielimu. naenda facebook kaandike hivyo utakutana na watoto wa shule.
 
Mitanzania Mingine Bora ife aisee, hv unajiskiaje wapinzani wanavyozimwa na hoja zao mbadala? unashadadia hoja za ndiooo.. daa kuishi bongo inatugharimu sana great thinkers
 
Kitendo cha CCM kumpendekeza Ndugai kuwa spika wa bunge, na ambaye anabebwa na idadi kubwa ya wabunge wa CCM, inaonyesha aina ya uongozi dhaifu usiowedha kukidhi kuongoza bunge.

Tutarajie fujo,vijembe na kushuka kwa hadhi ya bunge maradufu kwani kati ya vitu alokosa ndugai ni busara ya uongozi (sio kosa lake) na uvumilivu au kudhibiti hasira.
 
Mkuu, katika mfumo wa vyama vingi popote duniani,huwezi kuzuia hisia za kisiasa kwa itikadi za kichama. Ndo maana wapinzani wana mwamvuli wao wanaouita UKAWA na wamesimamisha mgombea mmoja kupambana na wa CCM. Katika mazingira hayo, usitegemee kwamba spika atakayepatikana awe wa CCM ama upinzani atakuwa na mizani sawa kwa vyama vyote. Huo ndo ukweli hata kama hutaki kuusikia
Ni ukweli katika vichwa vyetu vya hovyo si ukweli kama tunataka Utaifa na maendeleo ya kweli

Nimekuonyesha jinsi JK alivyofeli na katiba.
Jinsi Spika alivyotumika kuua nguvu ya hoja za wananchi na jinsi wananchi walivyogomea na serikali kufeli

Nilidhani sisi kama Taifa masikini tulitakiwa tukimbie badala ya kukumbatia utaratibu wa wenzetu wengine.

Hata utaratibu tunaoiga bado hatuwezi. Hivi si umeona NEC na mauza uza yake kuhusu ZNZ?

Ni wepesi wa kuiga kutoka kwingine, na wapuuzi wa kutekeleza maigizo tunayoyafanya

Tunahitaji Spika atakayesimama ili kuiwajibisha serikali , si Spika atakayesimama na CCM

Nakuhakikishia unapOjenga ufa kwa uchama unavia Taifa.

Awamu ya 4 imefeli kwa miaka 10 tusisubiri mingine tena, tumechelewa

Endelea na siasa za uchama!
 
Back
Top Bottom