Spika huapa mbela ya nani?

Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,334
988
Mwanzoni nilikuwa nadhani ni swali rahisi lakini ninavyosoma kanuni za Bunge na baadhi ya thread na matukio ya siku hizi tatu nimeona kuna ugumu kidogo kwa suala hili.

Kanuni za Bunge ibara ya 9(20) inasema hivi:

Mtu au Mbunge yeyote aliyechaguliwa kuwa Spika, kabla ya kushika madaraka yake, ataapa mbele ya Bunge Kiapo cha Utii na Kiapo cha Spika vitakavyokuwa na maneno yafuatayo.....

Kanuni 10(4) inasema hivi:
Mbunge yeyote atakayechaguliwa kuwa Naibu Spika, kabla ya kushika madaraka yake, ataapishwa na Spika Kiapo cha Naibu Spika

Kanuni 25(1) inasema hivi:
Baada ya shughuli ya kuwaapisha Wabunge kukamilika, Spika atasoma Taarifa ya Rais inayotaja jina la Mbunge...

MY TAKE:

Hivyo, ni wazi kwamba Mbunge-Mteule anakuwa Mbunge-Kamili baada ya kiapo mbele ya mbele ya Spika.
Hii ina maana gani. In maana kwamba mnapotoka uchaguzini wote mnakuwa katika ngaiz ya uteule. Bado hamjaapishwa.

Sina matatizo na wote wanaoapa baada Spika kuapishwa akiwemo Naibu Spika. Kwa sababu wanaapa mbele ya mtu ambaye tayari ameapishwa yaani Spika.

Tatizo langu ni kwamba, Je, Spika-Mteule anaapa kwa nani wakati walioko mbele yake wote ni wabunge wateule?

Je, leo pale Ikulu, kama Anne Makinda akiwepo, wakaleta lile gongo la Spika na Spika akavaa majoho yake, halafu James Mbatia, Janet Mbene na Sospeter Muhogo wakaambiwa waape mbele ya Spika kwa sababu yupo, insturments zake zipo, je kuna nini kinakataza isionekane kwamba hicho ni kiapo kamili cha ubunge.

Wenu katika kuelewa
 
Spika anaapa mbele ya Katibu wa Bunge.........Pia Spika ana mamlaka ya Kuwaapisha wabunge wateule kwenye ofc kuu Dodoma,ofc ndogo Dar na Zanzibar!!
 
Mkuu wala usipoteze muda wako bure kuwaza yasiyo na maana! Hivi umuhimu wa kuapa ni upi? Waape, wasiape kwangu naona sawa tu tena wasingeapa ingekuwa heri kwani haitakiwi kuapa kwa chochote.

Mimi naona kwa nchi yetu ni unafiki zaidi umetujaa kuliko dhamira ya moyo. Mtu mwenye dhamira safi na nchi yake atabaki kuwa hivyo hata asipoapa na jambazi litabaki kuwa jambazi tu hata likiapa kwa miungu yote - iliyopo na isiyokuwepo.
 
punguza jazba!!!!!
 
Sasa unataka alete hoja gani hapa! Hili ni swali la msingi sana hasa ukuzingatia tuna mchakato wa kutoa maoni kwenye katiba mpya. Tafakari!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom