Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 59,547
- 139,883
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kufanya vizuri zaidi ya baadhi ya Viongozi wa kiume akieleza kuwa mafanikio yake ni ushahidi wa uwezo mkubwa wa Wanawake katika uongozi.
Dkt. Tulia Ackson ameyasema hayo alipohutubia kongamano la Wanawake wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) lililofanyika Jijini Dar es Salaam likiwakutanisha zaidi ya Wanawake 1,000 kutoka Shirika hilo.
Katika hotuba yake amewahamasisha Wanawake walioko kwenye nafasi za maamuzi ambapo Spika Tulia amewataka kutokuwa wanyonge kwa sababu ya jinsia yao na kuendelea kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Taifa.
Ameongeza kuwa kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya 64 kati ya Nchi 146 duniani katika ajenda ya maendeleo ya kijinsia na ipo miongoni mwa Nchi 10 bora Barani Afrika zinazofanya jitihada madhubuti za kufikia usawa wa kijinsia.
My Take
Sasa Samia ana kipya gani zaidi ya mamiradi ya JPM