Spika asiingilie uhuru wa habari

Spika asiingilie uhuru wa habari

Jarateng

Senior Member
Joined
May 4, 2012
Posts
105
Reaction score
47
Mwanza Press Club, tunaungana na wanahabari wote nchini kulaani kwa nguvu zote amri ya KIUKANDAMIZAJI iliyotolewa na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, la kupiga marufuku kwa wandishi wa habari kufanya mahojiano na wabunge wanaosusia (wasiokubaliana) mwenendo wa uendeshaji wa bunge hilo.

Huo ni ukiukwaji mkubwa na uliovuka mipaka wa haki ya kutafuta, kupata na kutoa habari inayotolewa na Katiba ya Jamhuri.

Wandishi wa habari kufanya kazi za bunge na bunge kufanyakazi na wandishi wa habari sio HISANI, ni takwa la kikatiba na utawala bora. Mwandishi wa habari anao uhuru wa kutafuta habari mahala popote bila ya kuvunja sheria.

Bunge ni mkutano wa hadhara wa wawakilishi wa wananchi, hivyo ni lazima wananchi wapate habari ya yale yanayojadiliwa na wawakilishi wao kwasababu yanawahusu na yanahusu ustawi wao.

Spika anapaswa kutambua kuwa hata alipopiga marufuku kuonyeshwa kwa mijadala ya bunge moja kwa moja (live) wananchi hawakupendezwa na hatua hiyo na hivyo hatua yoyote inayozidi kulitia giza shughuli za bunge haliwezi kuungwa mkono.

Kama Spika anayo ajenda zake za siri ambazo hataki wananchi wazijue ni vema aseme kwa uwazi na azityekeleze nje ya bunge kwasababu bunge hilo ni la wananchi.

Tunamtaka Spika afute katazo hilo na kuwaachia uhuru wa kiutendaji wandishi wa habari na asijaribu kutufumba midomo na macho kama anavyowafanyia wabunge. - Mwenyekiti
 
Hii misimamo ya Ndugai dhidi ya wale wenye mtazamo tofauti, inatuchanganya sana wananchi kutokana na namna anavyo pandwa na mihemko . Hatuelewi ni misimamo yake binafsi, ya wabunge wote wa ccm na chama kwa ujumla, kuna mhimili unamtumia, au ana matatizo ya kisaikolojia!
 
Mwanza Press Club, tunaungana na wanahabari wote nchini kulaani kwa nguvu zote amri ya KIUKANDAMIZAJI iliyotolewa na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, la kupiga marufuku kwa wandishi wa habari kufanya mahojiano na wabunge wanaosusia (wasiokubaliana) mwenendo wa uendeshaji wa bunge hilo.

Huo ni ukiukwaji mkubwa na uliovuka mipaka wa haki ya kutafuta, kupata na kutoa habari inayotolewa na Katiba ya Jamhuri.

Wandishi wa habari kufanya kazi za bunge na bunge kufanyakazi na wandishi wa habari sio HISANI, ni takwa la kikatiba na utawala bora. Mwandishi wa habari anao uhuru wa kutafuta habari mahala popote bila ya kuvunja sheria.

Bunge ni mkutano wa hadhara wa wawakilishi wa wananchi, hivyo ni lazima wananchi wapate habari ya yale yanayojadiliwa na wawakilishi wao kwasababu yanawahusu na yanahusu ustawi wao.

Spika anapaswa kutambua kuwa hata alipopiga marufuku kuonyeshwa kwa mijadala ya bunge moja kwa moja (live) wananchi hawakupendezwa na hatua hiyo na hivyo hatua yoyote inayozidi kulitia giza shughuli za bunge haliwezi kuungwa mkono.

Kama Spika anayo ajenda zake za siri ambazo hataki wananchi wazijue ni vema aseme kwa uwazi na azityekeleze nje ya bunge kwasababu bunge hilo ni la wananchi.

Tunamtaka Spika afute katazo hilo na kuwaachia uhuru wa kiutendaji wandishi wa habari na asijaribu kutufumba midomo na macho kama anavyowafanyia wabunge. - Mwenyekiti
Tatizo wanahabari wengi wamekuwa wachonganishi, nadhani kuna umuhimu wa waandishi kuwa makini na habari wanazoandika, na siyo kuandika vitu visivyokuwa na tija kwa taifa
 
Mimi ni mwandishi ingawa sifanyi kazi za uandishi,ila nacho fahamu Mimi kipindi kile niko shule niliwai kuambiwa story lazima iwe balance so nadhani ili mwandishi akamilishe story lazima ahoji aliyeko ndani ambaye ajagoma na aliyetoka nje ambaye amegoma huwezi ukaita habari ikiwa na upande mmoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie ndio waandishi wachawi.
Kwenda kumuhoji mbunge kile kilichompelekea kususia kikao cha bunge nayo pia una hitaji balance gani ya story..!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Only in Tanzania.... Zitto Alisema nchi imekabidhiwa kwa Washamba

You are strong than what you think...
 
Wanahabari wenyewe njaaa wanaenda mpka press za musiba
 
Subwoofer ana matatizo binafsi anahitaji wataalamu wa saikolojia hakuna binadamu Mwenye akili timamu yeye muda wote ni kutengeneza chuki tuu mara leo CAG kesho wabunge na pia ukiangalia matendo yake unajua tu alikua wa kawaida sana shule kwa hiyo anatengeneza vita na wanaompinga waliomzidi uwezo wa kufikiri kila kukicha...
 
Mimi ni mwandishi ingawa sifanyi kazi za uandishi,ila nacho fahamu Mimi kipindi kile niko shule niliwai kuambiwa story lazima iwe balance so nadhani ili mwandishi akamilishe story lazima ahoji aliyeko ndani ambaye ajagoma na aliyetoka nje ambaye amegoma huwezi ukaita habari ikiwa na upande mmoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Waandishi makanjanja katika viti vyao!!!....unaelewa ulichoandika ???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwan kuacha kuandika habari zao zote inashindikana..??? Au kuacha kwenda press conference zao inashindikana? Sometimes ni bora uonekane kiburi while fighting for your right.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom