Spika asema baadhi ya Wabunge huvuta bangi na Unga, asema vifaa maalum kufungwa kuwabaini

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
ndugai.jpg

Kama unashangaa kusikia kwamba aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Charles Kitwanga kutimuliwa kwa sababu ya ulevi.

Bila shaka utachoka zaidi ukisikia kuwa kuna Wabunge huingia Bungeni wakiwa wamevuta Bangi na Madawa ya Kulevya.

Spika wa Bunge Job ndugai amefichua siri hiyo, Spika Ndugai amesema wanafikiria kuweka vifaa maalum vya kupima ulevi kwa watunga sheria hawa.

Spika wa Bunge amesema wanajaribu kuwatambua baadhi ya wabunge hao na kuwapa msaada wa kisaikolojia.

Maneno ya Spika; "Tunajaribu ku-identify(kuwatambua) watu maalum wanaoweza kutusaidia kuzungumza na hawa watu iliwaondokane na matatizo yale ambayo tutaweza kuyagundua... lakini wale wanaofanya kwa kificho itakuwa tabu kidogo. Lakini huko mbele tutakwenda kwenye vifaa" alisema Ndugai na kuongeza:

"Maana siyo ulevi tu, kuna sigara kubwa (Bangi), unga (Dawa za Kulevya).... watu wanapiga konyagi hadi mchana, kimsingi mambo ni mengi", alisema Ndugai.

Hata hivyo alisisitiza asieleweke vibaya sio wabunge wote hutumia vilevi wakiwa bungeni bali ni wachache.

"Simaanishi wote (Wabunge), maana mtu anaweza kufikiri ni wabunge wote... hapana. Hili ni kundi dogo mno la wabunge (na) hawajai hata mkononi. Lakini Wabunge walio wengi ni wazuru sana, hawanywi pombe wala nini. Kikundi hichi kinahitaji msaada wa ushauri" alisema.



MY TAKE: Hivo vifaa vitasaidia sana kuwabaini walevi, lakini ni hatari sana kwa taifa kuwa watunga sheria kuwa walevi, ifikie hatua sasa waheshimiwa wetu wafanyiwe vetting ili tusiwe na wabunge wasiowajibika ipasavyo.
 
kama vitafungwa kweli vitapunguza maneno ya hovyo, na ugomvi na vijembe mule ndani. ni muda muafaka wa kuona serious talk sio kupotezeana kodi zetu tu waheshimiwa.
 
Kweli hii nchi ni ya movie... Ina maana jamaa asingetumbuliwa all these shits zisingejulikana... Why tunakuwa proactive kwenye mambo???....
haya wabunge is non of their business. wapo kibiashara zaidi mzee. tulitegemea wapinzani watakuwa wapinzani wa kweli kumbe tunaambiwa ni wapingaji tu. maslahi ya taifa wameweka kando.
 
kumbe ndio maana bunge linakuaga na movie za ajabu. baadhi yao wakishavuta mibangi yao wanakuja kurusha mateke bungeni. tumeshagundua chanzo.
 
haya wabunge is non of their business. wapo kibiashara zaidi mzee. tulitegemea wapinzani watakuwa wapinzani wa kweli kumbe tunaambiwa ni wapingaji tu. maslahi ya taifa wameweka kando.
Umeambiwa na nani kuwa ni wapigaji?
13221066_1107532569311200_2094330381078929137_n.jpg


Hivo vifaa vitasaidia sana kuwabaini walevi, lakini ni hatari sana kwa taifa kuwa watunga sheria kuwa walevi, ifikie hatua sasa waheshimiwa wetu wafanyiwe vetting ili tusiwe na wabunge wasiowajibika ipasavyo.
 
the great master mind CCM wanacheza na mind the watanzania. Akili hiz walau wange2mia hata 20% to katka mambo yenye tija kwa nch ingekuwa mbal sana, bahat mbaya wamewekeza kuhadaa uma.
 
Back
Top Bottom