Job Ndugai: Wabunge watarajiwa wapimwe afya ya akili

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,312
24,171
"Ndugai: Kuna wanaotoa maoni wabunge wapimwe afya ya akili

Spika wa zamani wa Bunge, Job Ndugai amesema kumekuwa na maoni wabunge wapimwe afya ya akili kabla ya kwenda kuomba ridhaa ya kuwawakilisha wananchi bungeni akieleza kuwa jambo hilo ni la kuwaachia wananchi ili kuona kama lina umuhimu ama la.
Ndugai ameyasema hayo leo Jumatatu Oktoba 10, 2022 katika hospitali ya Mirembe aliposhiriki maadhimisho ya siku ya afya ya akili duniani.

“Hata kule bungeni wakati fulani panatolewa wito kwamba wabunge wapimwe akili, waende Mirembe kwanza kabla ya kupata Clearence, tunapojaza fomu zile za kuomba ubunge tujaze fomu kisha tuje Mirembe tupimwe na katikati ya muhula tuje tena tupimwe, hili ni pamoja na madiwani na viongozi wengine wakuchaguliwa, sijui kama jambo hilo ni muhimu ama si muhimu lakini kuna wengine wanasisitizaga sana jambo hilo, lakini hilo ni la wananchi tuwaachie wananchi."

“Ni kuonyesha tu kwamba kama mtu ana tatizo aweze kupata tiba, nia sio kumbagua mtu, nia ni kuona kama tatizo lipo ili mtu aweze kupata huduma inayostahili kwasababu madhara ya afya ya akilli ni makubwa sana,” amesema Ndugai.

Ndugai ameeleza dawa za kulevya zimesababisha wagonjwa wengi wa afya ya akili wanaosababisha maovu mbalimbali kwenye jamii, pamoja na wanafunzi kuwa watoro shuleni huku akitoa wito kwa wanafunzi kujiepusha na matumizi ya dawa hizo.

ndugaipiic.jpg

Spika wa zamani wa Bunge, Job Ndugai"

----
Job Ndugai kaamka toka usingizi wa kisiasa.

Akiwa mgeni rasmi sherehe za afya ya akili kitaifa huko Mirembe, ametoa maoni kuwa wabunge wanaowawakilisha wananchi wapimwe afya ya akili.

Katika hili mimi Jidduzz namuunga mkono kabisa.

Awamu ya Tano CCM ilituletea kiongozi mwenye kuhisiwa kuwa na matatizo ya schizophrenia, aina ya ugonjwa wa akili.
Tuliyopitia wote tunayajua.
 
"Ndugai: Kuna wanaotoa maoni wabunge wapimwe afya ya akili

Jumatatu, Oktoba 10, 2022
View attachment 2382971
Spika wa zamani wa Bunge, Job Ndugai"

Ref: Mwananchi online, 10 October 2022

Job Ndugai kaamka toka usingizi wa kisiasa.

Akiwa mgeni rasmi sherehe za afya ya akili kiyaifa huko Mirembe, ametoa maoni kuwa wabunge wanaowawakilisha wananchi wapimwe afya ya akili.

Katika hili mimi Jidduzz namuunga mkono kabisa.
Naunga mkono hoja
P
 
Tazama Urusi na KGB yao. Usiingize psychiatry katika siasa. Adui zako wa kisiasa somehow wakifanikiwa kukuingiza Mirembe,you will never draw a sane breath again. Zipo njama well- documented(katika nchi nyingi duniani) kwamba psychiatry imewatosa raia na inafanya kazi na vyombo vya Usalama kukandamiza raia.

Political abuse of psychiatry, also commonly referred to as punitive psychiatry, is the misuse of psychiatry, including diagnosis, detention, and treatment, for the purposes of obstructing the human rights of individuals and/or groups in a society.[1][2]: 491  In other words, abuse of psychiatry (including that for political purposes) is the deliberate action of having citizens psychiatrically diagnosed who need neither psychiatric restraint nor psychiatric treatment.[3] Psychiatrists have been involved in human rights abuses in states across the world when the definitions of mental disease were expanded to include political disobedience.

Utawala wa Mwendazake nimeponea chupuchupu kupelekwa Mirembe. There was a total breakdown of law and order wakati Magufuli alipokuwa Rais.

Kwa sababu,baada ya yeye kuwa dikteta,waliibuka madikteta uchwala wengi. Mbowe anasemaje? Wapo Chadema wengi wamembsmbikiziwa kesi Uchaguzi uliopita.

Mimi kidogo nipelekwe Mirembe. Hata Daktari alishaandaliwa wa kunipokea kule. I forget the name of the doctor. Literally,I have forgotten the name of the doctor. . It was Dr. Ruta or something. Ukishaambiwa unspelekwa mental hospital na daktari anatajwa,is that not dangerous?

Indeed naona kama yupo psychiatrist mmoja Kinondoni anaitwa "Ruta". But it seems like it's a woman psychiatrist. Good God! Someone wanted to take me to a woman psychiatrist?

Oh, huyu hana furaha,labda anataka kujiua,hana hela mfukoni,anaweza kujiua kwa msongo wa mawazo. Tumpeleke Mirembe upesi. Hafanyi kazi huyu. Hawa wezi wanajiita wafanya kazi?

Hawa watu pay slip inaonyesha milioni chache,wakati bank account yao inaonyesha bilioni chache.
 
Tulisha yasema sana hapa jukwaani lkn tukapuuzwa na Uvccm.

Leo hii sasa yamesemwa na mwana ccm husika naona sasa lugha itaeleweka.

Msikilizeni mh Ndugai tafadhali.
 
Wapinzani mkijiloga tuu ikapita kwisha habari yenu kila clearance utasikia ana ugonjwa wa akili huyo
 
Back
Top Bottom