tatanyengo
JF-Expert Member
- Mar 30, 2011
- 1,133
- 282
dalili ya serikali kupwaya.Spika wa Bunge la Jamhuri Mh. Anna Makinda amemtaka Waziri Mkuu kutoongea na wabunge pamoja na mawaziri wakati kikao kinaendelea ndani ya bunge. Spika amesema kwa kuwa Waziri Mkuu ni kiongozi wa shughuli za serikali bungeni anapaswa kusikiliza na kufuatilia mijadala kwa makini. Amesema kama hali hiyo inaendelea hakuna maana kuwa na kiongozi wa wa shughuli za serikali bungeni.
Katika siku za hivi karibuni wabunge na mawaziri wamekuwa na tabia ya kwenda kunong'ona na waziri mkuu wakati kikao cha bunge kinaendelea. Hata hivyo wakati Spika anatoa onyo hilo, Mh. Mkulo alikuwa anaongea na Waziri mkuu na baadaye Mh. Wasirra akajisogeza na kuanza kuongea na Mh. Pinda.
Pinda ni waziri mkuu kimeo kuliko wote waliotokea tanzania
Asikilize nini wakati hatumii ubongo kuchambua???
bora asafiri nje ya nchi amwachie mnafiki Sitta usukani atukane tena
Ni yeye huyuhuyu ila leo yupo kwenye "joto"<font size="3">ni makinda huyu ninaemfahamu au kuna mwingine?
Makinda ameanza kubadilika. Amesoma mood ya watu. Bora yeye kuliko kilaza Job Ndu...
Ana kisasi cha bosi wake rost tamu kujivua nguo.ni makinda huyu ninaemfahamu au kuna mwingine?
inawezekana huwa wanaenda kudai bahasha nasikia bungeni linaongazoa kwa kugawa bahasha....Hapo mama amenena ukweli. Bungeni ni sehemu ya kusikiliza mijadala ila kwa hivi karibuni wabunge wa kawaida na mawaziri wameanzisha kamtindo ka kwenda kupiga soga na PM sijui kwa manufaa ya nani. Huenda wanamhujumu PM hadi anashindwa kufuatilia mijadala kwa makini na mwisho wake kuishia kutoa kauli tata.
<br />
<br />
Ni yeye huyuhuyu ila leo yupo kwenye "joto"