vanpersie
Member
- Mar 3, 2012
- 82
- 36
wakuu mambo niaje? naomba kuuliza hivi kwanini mitandao yetu ya voda, airtel zantel na tigo hawana 3g wilayani? nipo mkoa wa kagera kama wiki tatu hivi kikazi lakini ukiwa mkoani pale Bukoba unapata 3g vizuri tu, ila ukifika wilaya za karibu kama misenyi na karagwe basi inakuwa mgogoro, kama ni idm spidi kubwa unapata 20Kb/s na hapo haitulii. wakati ukiwa Bukoba mkoani inafika mpaka 500Kb. je hii ni moderm yangu tuu au ndo hakuna 3g wilayani? naombeni ushauri wenu wakuu nifanyeje niongeze spidi yake maana ntakuwa huku kwa mud kama miezi mitatu hivi na sana sana ntakuwa kwenye hizo wilaya.natanguliza shukrani zangu.