Dawa ya Mjinga
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 382
- 145
"Gongo sasa hivi ni haramu sababu inatengenezwa kwa kificho katika mazingira machafu, tukishika dola tutataka SIDO itengeneze mitambo ya kutengeneza gongo ili iwe katika hali ya usafi," alisema.
Mitambo hiyo itakayotengenezwa na SIDO itakapouzwa itaiingizia mapato serikali pia wauzaji wa gongo watafanya biashara hiyo kwa amani tofauti na sasa ambapo wanaifanya kwa kificho na wakikamatwa fedha zote wananufaika polisi.
Kweli jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza, tena kiza kinene. Sasa hivi Tanzania kuna kinywaji kinachoitwa Konyagi na ndio maana jina jingine la gongo ni konyagi pori. Kwa Tanzania utengenezaji wa gongo uliendelezwa na serikali. Konyagi ilipoanza kutengenezwa kiawndani mali ghafi yake ilikuwa gongo. Watu walihimizwa kutengeneza gongo kwa wingi na kukiuzia kiwanda cha Konyagi. Ilipofika kiwandani gongo ile ilitenganishwa kitaalam na kuondoa sumu ambazo huchanganyika na gongo. Hiyo ndiyo aina ya mitambo anayoizungumzia Dr. Slaa.
Baadaye, kiwanda kiliamua kutengeneza pombe yake chenyewe kutokana na mabaki ya sukari viwandani yaani "molasses" na kuachana na ununuzi wa gongo la wananchi. Hapo ndipo wapika gongo wale kwa kificho wakaanza kuwauzia wananchi waliohitaji "konyagi pori". Hapo ndipo ikiwa mwanzo wa matatizo yote ya gongo kuenea nchini.
Kinachoweza kufanyika tena kitaalam kabisa ni kutengeneza mitambo midogomidogo ya kuondolea sumu kwenye gongo na kuifanya salama kama ilivyo konyagi. Baada ya hapo unaweza kubakiza jina gongo lakini kwa hakika kitakuwa kinywaji salama kama pombe nyingine halali. Ni jambo dogo sana kuibadilisha gongo kuwa pombe salama kama konyagi (aka "The Spirit of the Nation")
Wajinga, wapumbavu na wapuuzi wasitumie jambo wasilolijua kumwita anayependekeza hivyo eti mzee wa gongo. Huko ni kujitoa akili, kujilisha upepo, na kukubali kadamnasi kuwa wewe ni bozo. Jielimishe kidogo tu!