SPEED km/h.

Mkuu sipingi jibu lako ila vitu vilivyo kwenye motion under gravity uzito unakua ni factor (kubwa) kwa maana nyingine zinakua constant so kuangusha vitu haitaprove.
 
Mzee baba argument yangu iko supported na reference hapo juu,hebu nenda kasome kwanza hiyo reference halafu uniambie umegundua nini!
Mkuu kwenye reference yako imezungumziwa acceleration, acceleration ni pale unapoitafuta hiyo 80kph ni tofauti kabisa na speed, hizo factor ulizoweka zinaaplly kwenye acceleration ila ikishafikiwa speed husika hakutakuwa na time gap ni km 80 kwa saa 1 (hata mwendesha baiskeli angekuwa na energy ya kuifikia hiyo speed atafika sawa na basi)

Utofauti hapo utakuwa ni kwenye kazi iliyofanyika kwenye engine changanya na fuel consumption
 


Na wewe kabla ya kupost hapa umejiuliza kwamba kuna muda wa kukamilisha mzunguko?
(A time to complete one oscillation).

Tairi likizunguka mara moja litaenda umbali sawa na mzingo wake (circumference).

Sasa tuende kwenye tairi kubwa na dogo.

Bandiko lako linasema tairi dogo litazunguka mara nyingi kuupata Mzunguko wa tairi kubwa (hii sawa).

Umekosea sana ulivohitimisha kwa kusema kifaa chenye tairi ndogo kitachelewa kufika kisa mzunguko wake unaingia mara nyingi kwenye mzunguko mmoja wa tairi kubwa.

Inatakiwa uangalie na frequency yaani muda wa kukamilisha mzunguko wa kila tairi (time to complete one oscillation).

Kufikia hapa nadhani ushajua kuwa ukubwa wa tairi sio suala na kuzingatia na kitu cha kizingatia na frequency ipi kila tairi itumie ili zote ziende na speed sawa. Na zitafika pamoja.
 
Chukua kilo moja ya mawe na kilo moja ya pamba,, ukiwa juu angani dondosha kwa pamoja,, nafikiri ww mwenyewe unajua kipi kitatangulia kufiki ardhini......

Kwa upande wa magari ni injini ya gari na ccc zake,,, Chukua V8,
 
Hakuna YUTONG, higher, Asia star wala zhongtong yenye 120, zote zinasoma 140
 
Kg zitakuwa sawa bt box litakalotumika kubeba mawe ya kg 50 na box litakalotumika kubeba manyoya ya kuku yatakuwa tofauti bob kwa ukubwa hayatalingana .

Mnaulizwa uzito mnajibu ukubwa wa box mukiulizwa speed mnajibu mzunguko wa matairi na ukubwa wa mawe ... Tanzania ya viwanda hii na nyie ndo wasomi wetu Kazi ipo "Long live JF a home of Great Thinkers"
 
Hakuna YUTONG, higher, Asia star wala zhongtong yenye 120, zote zinasoma 140
Speed meter ya zhongtong na YUTONG hizo... zote ni 140 na kuna zingine zina 160... Ila ZA hapa bongo 99% ni 140
 
naona mtifuano ni mkubwa sana.
Mimi naomba nimjibu mtoa mada kama alivyouiliza swali. Kwa kuzingatia umbali wa 10km. Kwanza gari ama pikipiki haiwezi kutembea 8okm/h kwa umbali huo wote, lazima zitafika maeneo spidi itapungua kutokana na hali ya dunia, kuna sehemu kuna mabonde makali, kuna sehemu kuna miinuko mikali na pia kuna sehemu kuna kona kali barabarani hiyo ndio hali halisi. Na zile speedmeter zinasoma ktk speedmeter zinaitwa instanteous speed (yaani spidi kwa muda ule) sio average speed (wastani wa mwendo). Kwa hiyo ili vyombo hivi viwili vifike sawa inabidi tutumie average speed sio instantenous speed nikimaanisha kwamba piki piki itabidi itumie spidi zaidi ya 80 ili vifike sawa na gari kwani piki piki ktk mlima spidi yake itakuwa ndogo kutokana na uwezo mdogo wa injini yake na akifika sehemu tambalale itabidi atembee spidi kubwa zaidi ili kufidia mda alioutumia kupanda mlima,
Nadhani swali hili lingefaa zaidi kwa vitu vinavyotembea angani (space) kwani unapata uhalisia, ila katika barabara itakuwa ni kubuni zaidi kuliko uhalisia. Kama kuna makosa ruhusa kurekebisha
 
Tumia macho yako kuona movement inayokuwepo btn pikipki na gari kwenye iyo misafara ya pres huonagi kuwa the bike inakuwa into high soeed while the car inakuwa into low speed chief jaribu kuexamine vizuri utaligundua ilo mkuu
Hapana. Speed ni speed tu. Hata kama ingekuwa meli na gari. As long as ziko kwenye speed sawa lazima ziende pamoja.
 
Hilo swali lenyewe kwanza lina self-contradiction. Haiwezekani ku-accelerate at the same speed. Physics ya form one/two inasema accelaration ni rate change of speed over time. Pikipiki na gari hazitapitana at the same speed, period.
 
Wanaoleta hoja ya tairi watupe ufafanuzi wa trekta itatumia muda gani maana ina tairi kubwa ndogo pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…