Kuwa na OS itakayokubalika dunia nzima siyo kitu kidogo. Angalia hao Blackberry OS,Microsoft Windows phone OS na Nokia SYMBIAN hizo hazikufaulu kuteka ulimwengu kibiashara kwa muda mrefu wameishia kutengeneza devices zinazotegemea OS zilizo na watumiaji wengi.Kwa HUAWEI Huo ni mwanzo wa kufikia malengo ndugu. Wanaweza kupoteza wateja wengi sana kama watahama mazima,halafu kuna kitu kinaitwa 'custom Rom' hichi ndicho wanakitumia kwenye simu zao ili watumiaji wao waweze kupata experience ya tofauti ukiachilia mbali ile native Android Rom. Kingine ni masuala ya biashara yanawafanya watengeneze devices zinazotumia OS ambazo zinatamba duniani.