LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa NIGER (Russia + Wagner) na ECOWAS (France + Nato + USA). Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Ha ha ha ,nawaza kimasihara.
Na Russia wala Haina shida na Rasilimali za Niger wala west Afrika wala Afrika,kwa sababu Kila kilichopo Niger kipo Russia,Tena kwa wingi zaidi.

Russia inachota TU huko Niger ni kumwaga mboga.
Kwa sababu west wameshamwaga ugali.

Russia hawana haja na rasilimali za niger? Well ill be damn
Hakuna ngozi nyeupe ambae anakusaidia without something in return. Imetokea before itatokea again
 
Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa NIGER ( Russia + Wagner ) na ECOWAS ( France + Nato + USA). Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Jeshi la Niger kupitia televishen ya taifa limetangaza kupindua serikali ya nchi hiyo. Shughuli site za serikari zimesimamishwa na mipaka ya nchi imefungwa.

======

Wanajeshi wa Niger wadai kumuondoa madarakani Rais Bazoum – DW – 27.07.2023

Grace Kabogo

Kundi la wanajeshi wa Niger limetangaza kumuondoa madarakani Rais Mohamed Bazoum wa nchi hiyo, saa chache baada ya rais huyo kuzuiliwa ikulu na kikosi cha walinzi wa rais kinachoongozwa na Jenerali Omar Tchiani.
66359979_803.jpeg
Kanali Amadou Adramane wakati akizungumza kwenye televisheni ya taifa Picha: ORTN/REUTERS TV

Taarifa iliyosomwa na Kanali Amadou Abdramane kupitia televisheni ya taifa Jumatano usiku, huku pembeni yake wakiwa wameketi wanajeshi wengine tisa, imeeleza kuwa vikosi vya ulinzi na usalama vimeamua kuuondoa utawala uliopo madarakani kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama, utawala mbovu na hali mbaya ya kiuchumi na kijamii.

Kwa mujibu wa Kanali Abdramane, mipaka ya nchi imefungwa na amri ya kutotoka nje imetangazwa nchi nzima, na huduma katika taasisi zote za umma zimesitishwa, hadi hapo taarifa nyingine itakapotolewa. Wanajeshi hao pia wameonya kuhusu uingiliaji wowote ule wa kigeni. Hata hivyo, kundi la wanajeshi hao linalojiita Baraza la Kitaifa la Kulinda Nchi, limesema liko tayari kufanya mazungumzo na jumuia ya kitaifa na kimataifa.


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken ametoa wito wa kuachiwa mara moja kwa Rais Bazoum. Blinken amesema wanalaani matukio yanayoendelea Niger ya kunyakua madaraka kwa kutumia nguvu, ambayo yanaivuruga katiba ya nchi hiyo, pamoja na kudhoofisha utendaji kazi wa serikali iliyochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia.

Kauli za Marekani na Umoja wa Mataifa

Jumatano Blinken alizungumza kwa njia ya simu na Bazoum na kumueleza wazi kwamba Marekani inamuunga mkono kwa dhati kama rais aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia. Amesema msaada wa Marekani kwa Niger unategemea utawala wa kidemokrasia. Blinken pia amewataka raia wa Marekani kuepuka kwenda kwenye maeneo yaliyoko hatarini nchini Niger.

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, ambaye ameonyesha uungaji wake mkono kamili pamoja na mshikamano na Rais Bazoum, alilaani matukio yanayoendelea Niger. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric, amesema Guterres alizungumza kwa njia ya simu na Bazoum Jumatano jioni. Guterres amelaani vikali juhudi za kunyakua madaraka kwa nguvu na kudhoofisha utawala wa kidemokrasia, amani na utulivu. Amewataka wote wanaohusika kujizuia na kuhakikisha wanaheshimu na kuilinda katiba.

Rais Patrice Talon wa nchi jirani ya Benin, amesema yuko njiani kuelekea Niger kutathmini hali ilivyo, baada ya kukutana Jumatano na Rais wa Nigeria Bola Tinubu, ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Uchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS.

Mazungumzo na pande zote

Talon anatarajiwa kuwasili Niamey Alhamisi, ambapo atazungumza na pande zote mbili katika juhudi za kuutatua mzozo huo.

Umoja wa Afrika na ECOWAS wameliita tukio hilo kama jaribio la mapinduzi, na wamewataka waliopanga njama kumuachia huru Rais Bazoum bila masharti yoyote na warejee kwenye kambi zao. Matukio yanayoendelea Niger yamelaaniwa pia na Umoja wa Ulaya, Ufaransa na Benki ya Dunia ambazo zimesema kuwa zinafuatilia kwa karibu hali hiyo ambayo inaleta wasiwasi mkubwa.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais ya Niger usiku wa kuamkia leo, imeeleza kuwa Bazoum na familia yake wako salama, bila ya kutoa maelezo zaidi. Bazoum, mshirika wa karibu wa Ufaransa, alichaguliwa mwaka 2021 kuiongoza nchi hiyo isiyo na utulivu.
Ukisikia Marekani anazungumzia demokradia basi hicho ni kisingizio tu, maana marais wanaochagukiwa kwa kura za wizi (vote rigging) huwa ni vikaragosi wa mabeberu, kama huyo Bazoum ni kibaraka wa Ufaransa.., kwahiyo akae pembeni, atupishe!
 
IMEENDA HIYO.
Economic Community of West African States (ECOWAS) member state Cape Verde opposes a military intervention in Niger under the organization’s auspices, Cabo Verde President Jose Maria Neves said. “We all should work to restore constitutional order in Niger but in no way through a military intervention or an armed conflict at this point

20230813_235412.jpg

 
IMEENDA HIYO.
Economic Community of West African States (ECOWAS) member state Cape Verde opposes a military intervention in Niger under the organization’s auspices, Cabo Verde President Jose Maria Neves said. “We all should work to restore constitutional order in Niger but in no way through a military intervention or an armed conflict at this point

View attachment 2716665
Shetani (USA) mpenda damu za watu hataipenda hii.
Hawezi kuishi bila damu za watu.

Ila nashukuru tayari watu wenye busara wameanza kupinga vita.
 
Russia hawana haja na rasilimali za niger? Well ill be damn
Hakuna ngozi nyeupe ambae anakusaidia without something in return. Imetokea before itatokea again
Ok nimeandika hivyo kwa sababu Russia ana madini yote ambayo Niger anayo na ana madini mengine ambayo Niger Hana.
Navyoona anachokitaka Russia hapo Niger ni kuzuia Bomba la gesi lisipeleke gesi ulaya,kwa sababu ulaya wamemuwekea vikwazo.
Kwa hiyo hapa ni vita ya kiuchumi TU.
Wao wanataka kumuua njaa,nae anataka kuwaua njaa.
 
Leo ndo wakuu wa majeshi wa ecowas wanahitimisha mkutano wao wa kupanga namna ya kuingia kijeshi huko niger. ngoja tuone nini kitafata niger nayo inaendelea kujenga defense line huko mipakani
Huu mgogoro nadhani ndo utakuwa mgogoro ambao utauwa watu wengi sana africa kwa sababu ya tamaa ya viongozi wetu. Kwanza viongozi wazee sana na washa enjoy maisha wanasubilia kufa tu. Tunaitaji viongozi vijana kwa maana bado damu zao zinachemka na watakuwa na maamuzi ya kesho. Africa inatakiwa iamke kutoka usingizini na utegemezi wa kuamuliwa mambo yao wanayoyataka.
 
Back
Top Bottom