Special thread; Tamthilia ya Siri za Familia Inayorushwa EATV

Tamthilia nzuri sana hakikisheni mnakuwa na muendelezo kama isidingo!EATV pana wafaa.

Asante Mkuu, sasa hivi tuko katika maandalizi ya Season 2. Tumejulishwa kuwa Sponsor ametaka muendelezo kwa Mwaka Mzima. So hatujui Year 2 itakuwaje. Walau tuna uhakika wa kufanya Episodes 4 na kila Episode ina Scenes wastani wa 48 hadi 52 na inaonyeshwa kwa miezi 3.
 
Instagram: @sirizafamilia

Salaam Sana

Kwa wale wanaofuatilia tamthilia ya "Siri za Familia" (Family Secrets) inayorushwa EATV hii ni thread maalumu kuhusiana na Tamthilia hiyo.

Familia nyingi zina siri ingawa zinatofautiana. Baadhi ya siri zinaweza kujulikana na familia yote au wachache au hata mwanafamilia moja. Siri zinaweza kuhusiana na miiko, ukatili, mahusiano, magonjwa, uhalifu, mauaji, ubakaji nk. Jambo lolote ambalo mtu au familia inadhani linaweza kuleta tafarani linafanywa siri ya familia.

Hata hivyo hakuna siri ya watu wengi au ya muda mrefu kwani baadhi ya siri hatimaye hufichuka na siri zingine mtu anaweza kufa nazo. Je, ni nini kinatokea pale siri za familia zinapofichuka?

Fuatitlia thread hii ya Siri hizi katika SIRI ZA FAMILIA inayorushwa EATV kila siku ya Jumatatu hadi Alhamisi kuanzia saa 12.30 jioni hadi saa 1.00 jioni na kurudiwa kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 4.30 asubuhi hadi saa 5 asubuhi. Marudio ya wiki nzima ni siku ya Jumapili kuanzia saa 8.

Sasa hivi tamthilia inayorushwa ni season 1 na ina episode 48. Season 2 iko katika maandalizi.

Kwa wale wapenzi tukutane hapa kwa maoni na hata wenye visa vya kweli ambavyo wangependa viwepo katika Season 2. Visa vingi vilivyopo katika Season 1 ni visa vya kweli na vinatokana na utafiti uliofanywa na visa vya kweli ambavyo wadau wanavileta.
Ni nzuri sanaaa naifatilia, najifunza mengi katika hii tamthilia.
 
Ohooo basi hapo sawa ila carlos anamuahidi kumnunulia madaftari na uniform hapo ndipo nikashangaa tena...duu kweli hii siri za familiaa
Mwanzo alitoka shule form six, wakawa wanamsihi atulie asubiri majibu, yy akaanza mahusiano na Obama. Huku tamaa zikahamia kwa Carlos, adi matokeo yanatoka anafaulu akiwa mpenzi wa Carlos na akiwa na mimba yake pia, sasa kununua madaftari alitamka kama zawadi ila Sheila alistuka kiasi, duuu
 
Haaaa haaaa mwanzoni alikuwa anavaa nguo chafu chafu and very shabby, ila baada ya Dayana kuingia akabdailika na Kauka nikuvae zake!
Mmempatia sana na mmeuonesha utofauti na tamthilia nyingine! Mimi hii ndio tamthilia ambayo imefanikiwa kunifanya nisiwe naikosa kila leo!
 
Halafu uzuri hii tamthilia ni kwamba kila mtu ana umuhimu wake kiasi kwamba uwezo sema fulani atoke nime wakubali!

Tunategemea season 2 siyo mbadili story tunategemea muendelezo....
 
Mwanzo alitoka shule form six, wakawa wanamsihi atulie asubiri majibu, yy akaanza mahusiano na Obama. Huku tamaa zikahamia kwa Carlos, adi matokeo yanatoka anafaulu akiwa mpenzi wa Carlos na akiwa na mimba yake pia, sasa kununua madaftari alitamka kama zawadi ila Sheila alistuka kiasi, duuu

Duuh ama kweli unafuatilia Mkuu. Copy and Paste!
 
Inaweza kuwa tamthilia bora zaid kwa nyakat iz apa TZ...
Ushaur:next Episod mkipata vifaa vya kisasa zaid kwa ajil ya production itasaidia kuipeleka kwny Ushindani Kimataifa....
Then Napendekeza mtafute Producer mzur zaid ikiwezekana airud kuanzia EPISODE ya kwnz mpaka ya mwsho ya tamthilia... Hii itaongeza Quality ya pictures,sound,na mengneyo km Subtitles!
Kila nkiiangalia naona kua n pesa nyng Washiriki mnakosa kwa kuiacha iishie Tanzania akat hii tamthilia ina level za kimataifa i mean Hollywood hasa katka stori yke na muunganiko wa matukio!
Hopin mtalfanyia kazi hasa ili la kuipeleka HOLLYWOOD!
wishin u all the Best, na mfanikiwe kwa ili
 
Mwanzo alitoka shule form six, wakawa wanamsihi atulie asubiri majibu, yy akaanza mahusiano na Obama. Huku tamaa zikahamia kwa Carlos, adi matokeo yanatoka anafaulu akiwa mpenzi wa Carlos na akiwa na mimba yake pia, sasa kununua madaftari alitamka kama zawadi ila Sheila alistuka kiasi, duuu
Halafu hako kadaya kana fanana muandiko ni wewe..! Kwenye hii tamthilia kweli watu wamecheza kwa kiwango cha juu hadi nimeshangaa na uzuri ni kwamba kila mtu humo ana umuhimu wake!

Kwakweli huwa sihikosi!
 
Aisee, mwenyewe nimejikuta napenda kuifatilia, kila muhusika kajitahidi kuplay part yake. Mtoto Sheila nampenda kinoma ananimaliza,,, namba zake plz nimpongeze
 
Back
Top Bottom