Superman
JF-Expert Member
- Mar 31, 2007
- 5,693
- 1,701
Instagram: @sirizafamilia
Salaam Sana
Kwa wale wanaofuatilia tamthilia ya "Siri za Familia" (Family Secrets) inayorushwa EATV hii ni thread maalumu kuhusiana na Tamthilia hiyo.
Familia nyingi zina siri ingawa zinatofautiana. Baadhi ya siri zinaweza kujulikana na familia yote au wachache au hata mwanafamilia moja. Siri zinaweza kuhusiana na miiko, ukatili, mahusiano, magonjwa, uhalifu, mauaji, ubakaji nk. Jambo lolote ambalo mtu au familia inadhani linaweza kuleta tafarani linafanywa siri ya familia.
Hata hivyo hakuna siri ya watu wengi au ya muda mrefu kwani baadhi ya siri hatimaye hufichuka na siri zingine mtu anaweza kufa nazo. Je, ni nini kinatokea pale siri za familia zinapofichuka?
Fuatitlia thread hii ya Siri hizi katika SIRI ZA FAMILIA inayorushwa EATV kila siku ya Jumatatu hadi Alhamisi kuanzia saa 12.30 jioni hadi saa 1.00 jioni na kurudiwa kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 4.30 asubuhi hadi saa 5 asubuhi. Marudio ya wiki nzima ni siku ya Jumapili kuanzia saa 8.
Sasa hivi tamthilia inayorushwa ni season 1 na ina episode 48. Season 2 iko katika maandalizi.
Kwa wale wapenzi tukutane hapa kwa maoni na hata wenye visa vya kweli ambavyo wangependa viwepo katika Season 2. Visa vingi vilivyopo katika Season 1 ni visa vya kweli na vinatokana na utafiti uliofanywa na visa vya kweli ambavyo wadau wanavileta.
==============================================

Niaje wakuu,
Wabongo waliohusika kuitengeneza Tamthilia hii ya SIRI ZA FAMILIA walitulia na kuifanya kuwa tamthilia nzuri sana sio siri.
Inaeleweka na naona imebase katika matukio halisi yatokeayo katika jamii zetu.
Pia wamejitahidi kumatch couples, yaani wanaokuwa wapenzi wanaendana na dizain kama wameenda shule
Ila zaidi nimegundua kuna wanawake wazuri ninaowatamani sana mle, sio yule mama mzuri mwenye chura tu, bali hata Brenda na wengineo.
■Hongereni Waandaaji na Waigizaji.
Wakuu poleni na majukumu,
Imekuwa faraja sana kwa tamthilia ya siri za familia hasa kwa mida baada ya uchovu na pilika za mchana kutwa kutafuta riziki. Tangu ianze season one imekuwa kivutio pekee hadi sasa maandalizi ya season four.
Mimi nawapongeza sana wahusika wote.
Ombi tu wapunguze muda wa matangazo na muda wa kutoka season moja kwenda nyingine.
Wadau mnapendekeza nini au mna lolote juu ya hii series?