Special Thread : Elimu ya Ujenzi na Changamoto zake, vifaa vya ujenzi n.k

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,685
22,694
Habari Wana JamiiForums,.

Nimewaza juu ya kuwa na thread maalum kuhusiana na vifaa ama material bora vya ujenzi, mahali pa kuvipata, tahadhari n.k

Pia tuweze kushirikishana changamoto mbalimbali za ujenzi, gharama, tahadhari na mambo ya msingi ya kuzingatia kabla ya kuanza ujenzi wa nyumba, wakati wa ujenzi na hata wakati wa kukamilisha ujenzi yaani finishings.

Naomba tupate kujifunza kutoka kwa wale wenye uzoefu kwa kupeana taarifa sahihi kwani mara nyingi tumekuwa tukipotoshana na wengine kukatishwa tamaa kwa taarifa za uongo.

Naomba kuwasilisha.

Administrators naomba ushirikiano wenu.

Cc: Invisible Paw Rider JamiiForums
 
Tukianza na vifaa, ukweli hii ni changamoto kubwa siku hizi. Mfano kupata pima maji ( level) yenye ubora ni ishu. Asilimia zaidi 90 hazipimi Kwa usahihi. Labda upate Stanley, na uifuate posta mtaa wa India.

Mesumeno shida sio kubwa sana, ila nyundo nazo Siku hizi ni tatizo, hasa mipini yake.Tape hazina shida.vifaa vingine vibovu ni Sululu,majembe, pipe level, pasi ( geremala) nk.

Njoo kwenye materials ndiyo kabisa. Rangi unapaka Leo mwezi mmoja baadae imepauka.Cement ipo safi. Vitu vingine vibovu ni mikanda ya gipsum ( cornice),gipsum plaster, mabati, vifaa vya umeme,nk
 
Back
Top Bottom