Yaani ndo nashangaa hapa hata kucoment nashindwa leo Colombia anacheza vizuri sana,leo garasa(coz anakwenda CFC) letu Falcao na lenyewe linaonyesha makali.....
Falcao ni mzuri lakini Man U tulishindwa namna ya kumchezesha...
Lile jembe lingekutana na mpiga krosi kama Beckham hivi, tungemfaidi sana...
Ni mzuri ndiyo lakini mimi naona umri pia umemtupa mkono kidogo makali yamepungua, ngoja tumuone Mourinho atakavyomchezesha.....halafu kapendeza alivyonyoa kaonekana so young yale manywele yalikuwa yanamzeesha...

Namshangaa sana Mounrinho kumchukua Falcao, kuna wachezaji wazuri sana kuliko Falcao sijui kwanini anamtaka huyu. Ngoja tuone labda kaona kitu ambacho wengine hatukioni lakini naamini anafanya makosa kumsajili huyu.
Mhh!!! Leo siyo siri Brazil wamekamatika..... Neymar kamiss chansi nzuri alikuwa mwenyewe nikajua goli tayari kwa jinsi ambavyo hafanyagi makosa kwenye chans kama hizo.....
Hata hana umri mkubwa kihivyo...
Ndio kwanza ana miaka 29 kama Wayne Rooney, tena Rooney kazaliwa October 1985 wakati Radamel February 1986...
Mfumo wa kipumbavu wa LvG ndio sababu ya Falcao kuonekana boya...
brazil bado wamekalia?