Special Thread: CECAFA Senior Challenge Cup 2013

Hivi Amis Tambwe a.k.a Amis Mapenati yuko wapi? Simuoni katika list ya Burundi.
 
timu ya tanzania kiwango ni kidogo sana, tusipobadilika hatufiki popote
 
timu ya tanzania kiwango ni kidogo sana, tusipobadilika hatufiki popote

Mkuu ndo timu yetu na wachezaji waliochukuliwa ndo wanaofanya vizuri kwenye vilabu vyao, hatuna namna itabidi tuivumilie tu hivyo hivyo, tuombe Mbwana Samata na Ulimwengu wawahi labda wataokoa jahazi.
 
hivi ni kweli mbeya city hakuna mchezaji yeyote anayeweza kuchezea kilimanjaro stars? maana hao waliopo wa kawaida sana
 
jamani hivi hii zambia ndo ileile iliyotwaa ubingwa wa africa au kikosi cha pili?
 
Mkuu ndo timu yetu na wachezaji waliochukuliwa ndo wanaofanya vizuri kwenye vilabu vyao, hatuna namna itabidi tuivumilie tu hivyo hivyo, tuombe Mbwana Samata na Ulimwengu wawahi labda wataokoa jahazi.

tunavumilia sana ila hawa wanazidi......mtu unahamu ya kuangalia mpira ila ukishaanza tu unaishia kukasilika, wachezaji wanacheza kwa kunyata sana utadhani wanacheza mpira wa maana.....wamezubaa utadhani wanaumwa.....hakuna ile kucheza kwa kujituma na kutumia akili kwa ajili ya taifa, pale naona ni kipa Ivo mapunda pamoja na beki Yondani ndio wanaonyesha uhai......wengine ni kuruka ruka tu.
 
Hadi sasa ni mapumziko; Rwanda kapigwa kimoja na Sudan, sijui atakichomoa kama Simba anavyofanyaga!
 
Rwanda katolewa rasmi ktk mashindano!!! kapigwa 1 na Sudan..Now Uganda v Eritrea. Okwi, kiiza ndani.
 
Uganda took the lead. okwi on target dk ya 10.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…