Fabian the Jr
JF-Expert Member
- Aug 4, 2012
- 756
- 743
Ni kweli kwamba tuna matatizo ya upungufu mkubwa wa waalimu wa masomo ya sayansi nchini kwetu, Nilitegemea serikali ingechukua hatua mbadala kutatua tatizo hilo, lakini sikuwahi kufikiria kwamba ingefanya hivyo kwa kuchukua watoto waliomaliza kidato cha nne waliopata credit za chini na kwenda kuwatengeneza ndio wawe waalimu kwa watoto wetu.
Kijana ambae alipata div 3 form four huku akiwa na F ya hesabu na physics ndo anatengenezwa kuwa mwalimu wa sayansi. Ni hapo ndo nikafikiri zaidi, Ni vijana wangapi ambao form 6 walimaliza wakiwa na div 1, 2 and 3 ambao walienda vyuo vikuu wakamaliza lakini hii leo wako mtaani wakiwa hawana mahali pa kushika kutokana na ugumu wa ajira, Wangapi waliopata div 1, 2 o_level wakaenda a_level wakapata div 3 wakakosa vyuo vya kwenda na sasa hivi wako tu mtaani wakiwa hawana cha kufanya?
Kwanini serikali isitumie gharama kidogo tu kuwaweka sawa hawa ambao mimi naamini wanaweza kuwa BORA SANA kuliko hawa vijana. Hivi anaefeli form 6 akiwa na div 6 au hata 4 kwa PCM na aliepata div 3 o_level nani anakuwa bora zaidi? kwanini tusiwachukue hawa?
Leo mtu anasoma chuo kikuu degree hana mkopo lakini mdogo wake anaesoma special diploma ya ualimu anapewa 520,000 kila baada ya miezi miwili. Iko wapi thamani ya elimu yetu.?
Je hawa watoto tunaowasomesha kwa kiasi chote hiki cha fedha ni kweli watakuja kuwa na tija? Au ndo hiyo ya mtoto anaenda kumfundisha mtoto mwenzake?
NIKIWA KAMA MZAZI NAAMINI HAWA VIJANA HAWANA SIFA ZA KUWAFANYA KUWA WAALIMU KWA MASOMO AMBAYO TUMEWAPANGIA.