South Sudan imesaidiwa saana na UGANDA,Ethiopia,Kenya, Tanzania,Eritrea, na mataifa mengi mno ya Ulaya,Sidhani kama hizi nchi zimeshawahi wabania, Kwa taarifa yako Mtoto wa kwanza wa Garang,ambaye sasa ni mwanajeshi ndani ya SPLAA, amesoma Tanzania, Uganda imewasaidia saana hawa jamaa si kwa silaha, mafunzo, Mpaka leo kaskazini mwa uganda kuna kambi kadhaa za mafunzo za SPLAA. Garang kwa safari zake za nje alikuwa anatumia ndege binafsi ya M7. Operation base ya Garang ilikuwa Ethiopia, nakumbuka kuna kipindi SPLAA walizidiwa nguvu baadaya ya Libya kumpa bashiri ndege za kivita pamoja na silaha ndogondogo, ilibidi Eritrea wapeleke wanajeshi Kusini mwa Sudan waende wakaokoe jahazi
Kumbuka sio Israel pekee hata marekani,Norway, UK; Canada na mataifa mengine walitoa msaada mkubwa saana kwa SPLAA, nakumbuka kipindi vita ilikuwa inaendelea Kulikuwa na NGO moja tu kutoka Norway ilikuwa inatoa misaada South Sudan.
Kutokana na kuonewa kwa miaka mingi, wingi wa maliasili walizonazo Nchi nyingi zilikuwa zinasaidia kwa kila namana isipokuwa china tu, cha kushangaza niliwaona jana wanatangaza wanafungua ubalozi JUBA wiki hii