South Africa yafuta VISA kwa Watazania

The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
15,396
12,979
Habari za uhakika nilizozipata mida siyo mirefu, hatimaye South Africa wametufutia visa watanzania. Hivyo kama una shughuli za Holyday, Busness, Transit - No Visa required.

Mwenye more info anaweza kutuwekea hapa!!
 
Hiyo ni safi. Lakini kwa vipato vya Tanzania, hakuna mtu anaweza kwenda Holiday SA. Labda kwa kuiba pesa za matundu ya vyoo vya shule za kata
 
Habari za uhakika nilizozipata mida siyo mirefu, hatimaye South Africa wametufutia visa watanzania. Hivyo kama una shughuli za Holyday, Busness, Transit - No Visa required.

Hatuna shida ya kwenda A. Kusini. Tunakosa nini Tz. Holiday Mt. Kilimanjaro, bustani ya edeni huko bonde le Oldovai Georde, waweza kuchagua mbuga za wanyama, biashara ya kila kitu ipo....... Hata wakiamua kutulipa ili sisi twende hatuendi. Wanajidai sana hawa madogo. Wanatudharau mpaka wanatuuzia mapeasi kwa tsh500 wakati tango toka Dodoma Tsh. 50!
 
Mzee siyo lazima uende holyday tu, hata safari za kikazi na kibiashara. Unajuwa kuwa ilikuwa hata kama unakwenda Botswana au Namibia kikazi kupitia RSA ni lazima uwe na Visa??
 
Kwenda holiday kunataka mtu u-sevu pesa, na si kweli kwenda holiday nje ya nchi ni mpaka udokoe mahali. Jamani, hivi kweli hatukubali kuwa RSA kuna sehemu za kwenda kutembea? tusidanganyane jamani, Sauzi kuko poa kwa holiday , japo ni uamuzi, Gauteng au Gombe, Katavi etc
 
Niliisikia iyo toka last week kuna jobmate wetu mmoja kanyimwa nkadhani labda wamemuhisi gaidi nini kumbe wote.
 
If this is case I assume vice versa is also true??? i.e south africans wont need VISA coming to tanzania? So ..... ..
 
inapendeza mkuu tuhabarishe zaidi utaratibu, ni kukwea pipa tu au kuna maloloso mengine. maana wengi hatujawahi safiri safari za mbali zaidi ya mikoani hapa tz
 
South hakuna haja ya kutuwekea VISA, wanatuibia sana kila kitu. Angalia migodini, angalia bidhaa kibao tunaingiza kutoka south Africa, kwa hiyo ni kama wanatupiga changala macho hivi tufurahi wakati sisi tuko kwenye hatari ya kupoteza resources. Kuna Uranium huko kusini wanataka waichukue kimya kimya.
 
Habari hizi ni kweli na matangazo yamebandikwa kwenye ubalozi wa Afrika Kusini. Hii itaanza kutumika tangu tarehe 1.11.10 na ni kwa kipindi cha Mwaka mmoja. Inaonekana wanafanya majaribio. Iwapo itaonekana kufaa basi wataamua mwakani. Kila la Heri. Lakini kwa watakaokwenda hakikisha mnarejea nyumbani maana mkizamia wengi watautengua uamuzi huu.:smile-big:
 
South hakuna haja ya kutuwekea VISA, wanatuibia sana kila kitu. Angalia migodini, angalia bidhaa kibao tunaingiza kutoka south Africa, kwa hiyo ni kama wanatupiga changala macho hivi tufurahi wakati sisi tuko kwenye hatari ya kupoteza resources. Kuna Uranium huko kusini wanataka waichukue kimya kimya.

Hawatuibii bali tumewaita sisi wenyewe waje wachote wanavyotaka. Kwani walituchapa viboko kusaini mikataba? Tena tumejifunga wenyewe kwa mikataba ya kichifu mangungo. Nakumbuka nikiwa shuleni kuna mwalimu mmoja wa historia alikuwa anapenda sana usemi huu wa kimombo: "Give enough ropes to a fool and he will hang himself". Akimaanisha wakoloni waliwapa machifu wa kiafrika shanga, pipi, magobole, vioo vya kujitazamia na vitu vinavyofanana na hivyo na kisha hawa babu zetu wakajinyonga kwa kusaini mikataba wasiyoijua inatamka nini.

Sisi wa kwetu wanajua kusoma na kuandika lakini ajabu bado wanajinyonga kwa mikataba ambayo wameisoma na kuielewa. Wahenga walisema "Wajinga ndio waliwao" (ni usemi tu siyo tusi)
 
kweli hii dharau,kwamba tukaone tulivo watajirisha na rasilimali zetu au?
 
Hiyo ni safi. Lakini kwa vipato vya Tanzania, hakuna mtu anaweza kwenda Holiday SA. Labda kwa kuiba pesa za matundu ya vyoo vya shule za kata
safi sana... hii ndiyo kumkoma nyani giladi... wanafuta maana wanajua wameshtuchakachua sana na wenye uwezo wa kwenda ni haohao au wanaoenda workshop tu

labda na wazee wa kariakoo
 
Back
Top Bottom