SOUTH AFRICA: Misplaced anger.

SOUTH AFRICA: Misplaced anger.

mazojms

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2017
Posts
1,625
Reaction score
2,546
"Kuna jumla ya wahamiaji millioni 2.3 wanaoishi SA, idadi hii inajumuisha waafrika kutoka nchi zingine za afrika, wachina, wabangladesh, wahindi na waeurope wasio wazawa wa SA. Milioni 1.6 ya wafrika ni wajasiriamali wadogo wa maduka na wa barabarani. Jumla ya mali zao ni chini ya asilimia 0.00001% ya mali za SA.

Waeurope/wazungu ni asilimia 8.7% ya population na wana controls zaidi ya asilimia 85% ya mali za SA. Idadi hii ni kama 6000 ya familia za kizungu wanaomiliki asilimia 85% ya arthi ya SA.

Nasema kwamba hasira yenu na jeuri yenu haipo mahala pake. wahamiaji wa kiafrica hawamiliki ardhi, hawamiliki kampuni za migodi, hawamiliki trophy hunting companies, hawapeleki fedha za kigeni katika mabenki ya ulaya.

Yenu ni hasira ya kibaguzi iliyojengeka kutokana na inferiority complex iliyotengenezwa na miongo ya ubaguzi wa rangi na unyonywaji. siwaoni waafrika wengine kama washindani bali kama wananchi wenzangu wanaohangaika kilisha familia zao na kupata matumaini katika maisha haya mafupi.

Kama mnahisi mgawanyo wa mali usio sahihi tafadhali fanyeni utafiti upya wa nani ana control na kushikilia mali. na haihusiani na mnaigeria, mmozambique, au mzibabwe anaefanya kazi mgahawani. au methiopia anaye uza duka la rejareja. au makenika mghana anayefanya kazi za nguvu juani."

NI MANENO KUNTU KUTOKA KWA TREVOR NOAH, MMOJA KATI YA WASOUTH AFRIKA WENYE AKILI KUBWA.

#SAYNOTOXENOPHOBIA
 
mkuu kingine ni ahadi alizotoa raisi wao kabla ya kuingia madarakani, kwamba angewafukuza wahamiaji ili nafasi ya kazi itokee, so walikua wanamkumbusha Cyril ahadi yake!
Sikuhizi dunia ni kijiji, moja kati ya vitu ambavyo haviwezi kuwa controled ni mzunguko na muingiliano wa watu.. nafikiri njia sahihi ni serikali ya SA kuweka sheria rafiki ambazo kwazo uwepo wa wahamiaji hauto athiri wazawa.

Unayoisema inaweza kuwa ni sababu lakini kwa mtazamo wangu naona haina mashiko. Waache watu watafute maisha popote pale, cha msingi wasivyunje sheria.
 
Ukifuatilia hutuba ya Malema aliyotoa hivi punde utagundua kwamba watu weupe wanaomiliki biashara kubwa kubwa ndio hao wanaoanzisha mzozo huu, malema anasema ni kwanini unafungua biashara na kumuajiri mtu kutoka nje wakati wa hapa ndani wapo? analaumu watu weupe kuwa wapo na ajenda ya siri kutufanya weusi tuuwane sisi kwa sisi. Yeye anasema kinachoitwa Private sector ni maneno yenye ladha kuyatamka ambayo yanaficha tusi kubwa ikiwa na maana ya weupe kuwatalawa weusi
 
Target ya kila businessman ni kupunguza operating cost.. kama ni rahisi kupata cheap labour wahamiaji na hakuna sheria zozote zinazowaongoza namna ya kuajiri tatizo haliwezi kuisha.. Malema amepoint matokeo ya tatizo na sio tatizo lenyewe.
 
Nchi za Africa zijenge mazingira bora kwa raia wao. Naona jukumu wamemuachia South Africa.
Ni kweli, lakini kumbuka pia wahamiaji walioko SA pia wanajenga mazingira mazuri kwa ndugu zao waliobaki nchini mwao.
 
Target ya kila businessman ni kupunguza operating cost.. kama ni rahisi kupata cheap labour wahamiaji na hakuna sheria zozote zinazowaongoza namna ya kuajiri tatizo haliwezi kuisha.. Malema amepoint matokeo ya tatizo na sio tatizo lenyewe.

Na kwa nini ufanye hivyo? unajua madhara ya kuajiri cheap labour kutoka mataifa mengine kwa nchi yako? mi ninachodhani hapa ni kuwa bado SA wanatumia sharia zile zile za mkoloni ingawa nchi sasa wanatawala wazawa, mimi nipo ughaibuni pia lakini sheria za hapa zinampa umuhimu mkubwa kwanza mzawa wa nchi, SA uchumi wake ni mkubwa na kama watakuwa na utaratibu mzuri kwa wanachi wake sidhani kama Unemployment rate ingekuwa kubwa kama iilvyo hivi sasa.
 
Miaka ya 80 Nigeria nao walikuwa na fukuzafukuza ya Wahamiaji haramu haswa Waghana. Tofauti ni kwamba Wanaijeria hawakuwa violent and brutal to the point of hunting down and killing random immigrants in the streets.
 
mi naona hali ya SA haituhusu maana watanzania waliko kule hawafiki laki 1 soo muhimu warudi wenyewe au wabakie uko tupokee miili yao. TUFIKIRIE NCHI YETU TANZANIA SISI TULIOBAKIA NA KUAMINI HAPA HAPA TUTAFANIKIWA tukuze uchumi Tujenge Taifa letu Hao walioenda SA hawana faida nasi kwasasa zaid ya kupendezesha CURRENT CITY in facebook na Kuvaa nguo za kanisani Nje nyumba za watu huko instagram
 
"Kuna jumla ya wahamiaji millioni 2.3 wanaoishi SA, idadi hii inajumuisha waafrika kutoka nchi zingine za afrika, wachina, wabangladesh, wahindi na waeurope wasio wazawa wa SA. Milioni 1.6 ya wafrika ni wajasiriamali wadogo wa maduka na wa barabarani. Jumla ya mali zao ni chini ya asilimia 0.00001% ya mali za SA.

Waeurope/wazungu ni asilimia 8.7% ya population na wana controls zaidi ya asilimia 85% ya mali za SA. Idadi hii ni kama 6000 ya familia za kizungu wanaomiliki asilimia 85% ya arthi ya SA.

Nasema kwamba hasira yenu na jeuri yenu haipo mahala pake. wahamiaji wa kiafrica hawamiliki ardhi, hawamiliki kampuni za migodi, hawamiliki trophy hunting companies, hawapeleki fedha za kigeni katika mabenki ya ulaya.

Yenu ni hasira ya kibaguzi iliyojengeka kutokana na inferiority complex iliyotengenezwa na miongo ya ubaguzi wa rangi na unyonywaji. siwaoni waafrika wengine kama washindani bali kama wananchi wenzangu wanaohangaika kilisha familia zao na kupata matumaini katika maisha haya mafupi.

Kama mnahisi mgawanyo wa mali usio sahihi tafadhali fanyeni utafiti upya wa nani ana control na kushikilia mali. na haihusiani na mnaigeria, mmozambique, au mzibabwe anaefanya kazi mgahawani. au methiopia anaye uza duka la rejareja. au makenika mghana anayefanya kazi za nguvu juani."

NI MANENO KUNTU KUTOKA KWA TREVOR NOAH, MMOJA KATI YA WASOUTH AFRIKA WENYE AKILI KUBWA.

#SAYNOTOXENOPHOBIA

Good analysis.
 
Nchi za Africa zijenge mazingira bora kwa raia wao. Naona jukumu wamemuachia South Africa.
wamemuachia kivipi ilhali wa SA wenyewe wanalia hawana ajira..
 
Na kwa nini ufanye hivyo? unajua madhara ya kuajiri cheap labour kutoka mataifa mengine kwa nchi yako? mi ninachodhani hapa ni kuwa bado SA wanatumia sharia zile zile za mkoloni ingawa nchi sasa wanatawala wazawa, mimi nipo ughaibuni pia lakini sheria za hapa zinampa umuhimu mkubwa kwanza mzawa wa nchi, SA uchumi wake ni mkubwa na kama watakuwa na utaratibu mzuri kwa wanachi wake sidhani kama Unemployment rate ingekuwa kubwa kama iilvyo hivi sasa.
Nafikiri hasira zao wangezielekeza kwa serikali yao, wahamiaji wa kiafrika ni watafutaji tu wanaangali sehem wanayoweza pata pesa kirahisi. Sheria zikikaa vyema hata wahamiaji wanaweza pungua bila kutumia nguvu.
 
Target ya kila businessman ni kupunguza operating cost.. kama ni rahisi kupata cheap labour wahamiaji na hakuna sheria zozote zinazowaongoza namna ya kuajiri tatizo haliwezi kuisha.. Malema amepoint matokeo ya tatizo na sio tatizo lenyewe.
Sheria za Kuajiri wageni wahamiaji Afrika Kusini ni Kali sana, usidanganywe. Nimeahi kuishi na kufanya kazi Afrika Kusini, nafahamu vizuri kuhusu hili.
Tatizo lililopo kule ni ANGUKO KUU LA KIUONGOZI KWA WATAWALA WEUSI, wa chama chama cha ANC.Wahamiaji wanatumika kama SCAPEGOAT (kichaka cha kuficha kushindwa kwao/kisingizio).
 
Ukifuatilia hutuba ya Malema aliyotoa hivi punde utagundua kwamba watu weupe wanaomiliki biashara kubwa kubwa ndio hao wanaoanzisha mzozo huu, malema anasema ni kwanini unafungua biashara na kumuajiri mtu kutoka nje wakati wa hapa ndani wapo? analaumu watu weupe kuwa wapo na ajenda ya siri kutufanya weusi tuuwane sisi kwa sisi. Yeye anasema kinachoitwa Private sector ni maneno yenye ladha kuyatamka ambayo yanaficha tusi kubwa ikiwa na maana ya weupe kuwatalawa weusi
Hao watu sio wajinga wanajua wsnachofanya, kabla walikua wanawachukia makaburu kupita kiasi lakini baada ya dunia kua kijiji wameshaona mataifa yaliyowafukuza hao wazungu wanaomiliki biashara yalivyo. Hao wote wanaopambana nao mtaani walikotoka kuna mapori ya kutosha kuna rasirimali za kutosha. Kama watu wanakimbia sehemu ambayo beberu alifukuzwa na badala yake anakimbilia aliko beberu basi tatizo sio beberu.
 
Back
Top Bottom