Jamani hivi Rais wetu anatumia vigezo gani kuchagua watendaji wake hasa ukizingatia Mama huyu ni WAZIRI kwakweli hafai kuwa hata diwani.Nimesikiliza mjadala huo mwanzo hadi mwisho bahati mbaya nimeshindwa kurekodi.Kwakweli huyu mama amezungumza pumba inatia aibu.Anaulizwa kuhusu mipango,mikakati na mafanikio yeye anazungumzia sherehe na kwamba sherehe ni vigumu kufanyika kila kijiji.Ukimsikiliza mshiri kutoka Rwanda moja kwa moja utaelewa kwanini wanafanikiwa,mtu maki anaelewa anachokizungumza kwake ni rahisi kuelezea mikakati,mipango na mafanikio.Kwani kwao mipango ipo,mikakati ipo,watendaji makini wapo na hatima yake mafanikio ndio maana katika kipindi kifupi baada ya kutoka katika vita wamepiga hatua kubwa katika sekta zote.Katika nchi yetu ambayo pamoja na amani na utulivu kwa watendaji kama hawa wakina Sophia Simba cha kusikitisha asilimia 99 pamoja na Rais mwenyewe JK uwezo wao wa kuoongoza ni dhaifu nchi yetu inapiga hatua kurudi nyuma.Inasikitisha MUNGU IBARIKI TANZANIA.