Namtazama waziri mkuu wa awamu ya tano jinsi alivyokuwa akichapa kazi. Jinsi alivyokuwa akisimamia utendaji wa serikali akiongea kwa mamlaka ya nafasi yake.
Nikimlinganisha na huyu wa awamu ya sita nagundua kabisa ni mtu aliyejivua kwa kuwa ana ndoto zaidi ya hapo hataki lawama, hataki kuchafuka hataki kuwa sehemu ya mitihani mingi iliyopo sasa. Japo ni mtu yuleyule mmoja.
Huenda shughuli za utendaji wa serikali zimebadilika siku hizi, shughuli usimamizi na kusema kwa niaba ya Rais na Serikali ambazo kimsingi nj za Waziri Mkuu kama mtendaji Mkuu wa shughuli za Serikali hazina mwenyewe tena.
Tulipaswa kumuona Waziri Mkuu kama sehemu ya kusimamia Serikali akisimamia mijadala na kuhamasisha watendaji walio chini yake kuwa kitu kimoja.
Hii inaonyesha wazi Waziri Mkuu ni mtu anayelipwa mshahara mkubwa, anatuzwa vizuri, anapokea kila aina ya vipaumbele pamoja na kuhakikishiwa kila aina ya msaada kikazi, akiwa hajui tena wajibu wa kazi yake.
Rais amepata Waziri Mkuu anayetamani kuwa Rais akijiandaa na kushindana na wanaotaka urais wengine. Hawezi kukubali kuchafuka kwa niaba ya Rais. kuna kitu Rais Samia anahitaji sasa msaidizi wa kutimiza maono yake.