Soon, Ally Hapi atakuwa ndani ya mfumo

Suzy Elias

JF-Expert Member
Nov 9, 2021
1,067
6,193
Ilikuwa ni vigumu mno kwa Mwenyekiti kuendelea kuishi na watu wenye kumshauri kwa karibu huku akiendelea kusikia pembeni wakijadili namna sahihi na bora ya kumnyang'anya tonge mdomoni.

Kwa muktadha huo, boss lady ameamua kama mbwai na iwe mbwai na rasmi ameamua awarejeshe kundini wale wote anaodhania watakuwa watiifu kwake.

Tayari faili la bwana mdogo Ally ameliitisha mezani. Na duru zinatabanaisha ni swala la wakati tu bwana mdogo yule atajumuishwa.

UWEZEKANO WA MUUNDO WA UONGOZI WA CCM SIKU CHACHE ZIJAZO:-

Mwenyekiti: Samia Suluhu Hassan

Katibu Mkuu: Paul Makonda

Katibu Mwenezi: Ally Hapi

Nafasi za ngazi zingine zitabaki na watu waliopo.

Onyo!

Yule mpayukaji na mlima MTAMA anatafutiwa angle tu wale kichwa! Asiyegusika ameshalia kwa boss na kumwambia asingependa kufanya naye kazi.
 
......umepaniki!
Kwa lipi Suzy? Tuhoja twepesi twa kupima upepo hatuwezi kunipanikisha. Nimekupa tu mifano ili upime huyo unayemshobokea ana nguvu ipi?

Ya watu,ya ushawishi? Ya fedha? Ya network au ya nini? Ukitumia hao niliowataja utajua tu CCM ni litaasisi likubwa mno kuliko mtu au watu wachache. Msimfanye Mwenyekiti wetu na wasaidizi wake hawana akili.

Akiamua ameamua ana sababu za wakati husika na sio za kichonganishi na za kugawa chama kama hizo unazotaja. Kuna mabadiliko ni ya lazima kwa wakati husika.
 
....ameamua iwe hivyo sasa kwa wakati huo husika.
Na iwe tu,kwani ilivyokuwa kwa Makonda kuna wanachama wamerudisha kadi? Kazi inaendelea na wanachama wanatimiza wajibu wao, wampende au wasimpende wanabaki kuunganishwa na Chama chao.

Hakuna kiongozi anapendwa na watu wote so tusishane na fulani na fulani. Watakuja na watatoka tu kama wengine.
 
Hapa nimekuelewa...maana Moto wa Kusaini mikataba na DPWorld ulikuwa si wa kitoto wakati huo, hivyo, ilikuwa ni lazima. Maamuzi yafanyike. Nimekuelewa.
Eeeh watu wanatumia sayansi ya siasa kufanya matukio fulani kwa pamoja wakati fulani halafu kuna mtu anatuletea siasa za mahaba hapa. Siasa ni akili,kuongoza nchi ni zaidi ya kuweka unaowapenda,kuna wakati adui ndio anakuvusha na hitaji la wakati.
 
Back
Top Bottom