Songea: Kaya 19 zakosa makazi baada ya nyumba zao kuezuliwa kwa mvua

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,512
mvua(8).jpg
Jumla ya kaya 19 zenye wakazi zaidi ya 100 katika kijiji cha Mipeta kata ya Mhukuru wilaya ya Songea mkoani Ruvuma zimekosa makazi ya kuishi kutokana na nyumba zao kuezuliwa na zingine kubomolewa kwa mvua iliyoambatana na upepo mkali huku pia mvua hiyo ikiharibu akiba ya mazao yao mbalimbali ya chakula yakiwemo mahindi na Maharage.

Mvua hiyo iliyonyesha majira ya saa tisa za mchana na kudumu kwa muda wa zaidi ya nusu saa ikiambatana na upepo mkali imeezua pia madarasa ya shule ya msingi Mipeta, kuharibu vitabu na kusababisha wanafunzi wa shule hiyo kukosa madarasa ya kusomea huku pia nyumba mbili za walimu nazo zikiezuliwa.

Wananchi waliokumbwa na maafa hayo wanasema mvua hiyo ambayo haijawahi kutokea kijijini hapo mbali ya kuezua mapaa na kubomoa nyumba zao pia imeharibu akiba yao ya mazao mbalimbali ya chakula yakiwemo Mahindi na Maharage.

Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Songea, Bw. Pololeti Kamando Mgema amesema serikali bado inaendelea kufanya tathimini ili kujua hasara iliyojitokeza kutokana na maafa hayo huku akiwawatahadharisha wananchi kuezeka nyumba zao katika ubora unaotakiwa ili kuepukana na maafa kama hayo.


ITV
 
Back
Top Bottom