Songea boys | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Songea boys

Discussion in 'Matangazo madogo' started by ngoshwe, Oct 28, 2011.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Tupo hapa kwenye Facebook, kwa waliosoma Songea Boys Sec Schoool ( wa Luila )
  Log In | Facebook


  [​IMG]


  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
   
 2. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
   
 3. K

  KAPONGO JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,374
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  DUUU!! umenikumbusha mbali..hususan hilo Ford ambalo kwa wakati huo lilikuwa linaendeshwa na dereva mtanashati -maarufu dereva Ally. Gari hilo lilikuwa maarufu songea kwa vile lilikuwa linabeba wanandinga wa box 2 ambao katika miaka ya 70 hadi mwanzoni mwa 90 shule hiyo ilikuwa ndiyo club bingwa ya mkoa...Du sijui pale kwa Chenjela bado hai! maana viazi na mihogo ya pale vilikuwa vinasupplement diet hasa ya wanafunzi waliokuwa wanaishi katika mabweni ya Nile, Niger na Congo.
   
 4. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Ujamaa, Muungano, Azimio?
  Wale wa TCC Matogoro wanaijua vizuri Box 2
   
 5. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Mademu wenu wa Songea Girls nao wapo kwenye FB?
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ngoswe huu ni uchokozi, wenzako tulishahau huko.... loooong time bwana...
   
 7. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Yap Mkuu!

  Log In | Facebook
   
 8. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Zama zipi zile za wa Tambaza??
   
 9. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Ingependeza kama ingekuwa ni Fan page more than a group... Kwani wengine Box 2 ilitugusa sana ilhali hatukusoma huko!
   
 10. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,947
  Likes Received: 1,507
  Trophy Points: 280
  Uhuru,Muungano,mama Sizya ,mayao ya kwa Nuru, je hivi lile Grunding bado lipo ,kingine kulikuwa na bugo lilikuwa likipulizwa kujulishwa kuwa mbufu na zege vipo tayari hata ukiwa Gorani utalisikia tu ,vijana wa Box 2 oyeee ,ingawa wengine mnatuangusha kwa kuwa mawakili wa mafisadi na wengine maarufu kwa kuandika mikataba inayo liingiza taifa mkenge,nyumbi hii bombi hiii ndio nyumbani kwangu
   
 11. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,947
  Likes Received: 1,507
  Trophy Points: 280
  Kibu ulikuwa Kaigo nini wale Tamsala,Tamso majina yalikuwa yanageuka kutokana na nyakati kwani Songea Girls wanafunzi wa kwanza waliletwa kutoka Msalato ,baadaye wakaja wale ambao hawakuhamia ndio Tamso loo kaka machozi yananitoka nikikumbuka disco la box 2 na Tamsala ,huku box kulikuwa na wanaume wa ukweli, na kule Tamsala kulikuwa na wanadada wa ukweli,ingawa wachezaji wa majimaji walikuwa watuzidi kwa kuopoa kwa kuwa walikuwa na vijisenti ilihali sisi mtaji mkubwa ulikuwa Mali kauli,unaimbisha wee unapata mzigo baada ya mwezi ,ukipata hela ya kwenda chamber unakuwa huna inabidi uahirishe game
   
 12. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,947
  Likes Received: 1,507
  Trophy Points: 280
  Kapongo hapo kwenye RED pamenivunja mbavu ,naam diet ya mbufu,kuna siku kwenye disco na tamsala kuna dada alikuwa anaringa sana,na alwahi kuwaita wana box 2 NATO (ukitaka kuwaudhi box 2 waite NATO)alimwagiwa mustini mzima wa mchuzi mbufu ilibidi disco alikose akae kwenye gari hadi saa nane usiku(enzi hizo disco lilikuwa usiku kabla hali ya hewa haijachafuka)
   
 13. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wee mchokozi sana, umenikumbusha mambo mengi hasa lile bweni, nimekiona kitanda changu, siku moja hokololo akiwa mwalimu wa zamu alitushukia alfajiri kutuamusha kwa bakora eti alikuwa anajiita bulldozer. Vipi ugali na small mbofu?
   
 14. S

  SolarPower JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 226
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Japo sikusoma Songea Boys, na wapongeza kwa kukumbushana. Ila tusiishie hapa ni muhimu sana tukawa na mipango maalum ya kuzisaidia shule zetu za Msingi na Sekondari tulizosoma ili ziweze kuwa bora zaidi na kutoa wanafunzi waliobora zaidi.
   
 15. MANAMBA

  MANAMBA Senior Member

  #15
  Oct 29, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  DUUUU! Box 2, umetukumbusha maaali. Mayao ya mama thumni thumni, chai ya Omari. Mambo ya magoti na maharagwe ya mbinga! We acha tu. Tukumbushe pia vituko vya baadhi ya waalimu
   
 16. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #16
  Feb 19, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Du! Mmenikumbusha mbali saaana. Nimelikumbuka hilo kwama la shule ambalo tulikuwa tunalitumia usiku kupeleka wagonjwa hospitalini na kwenda kaigo, maposeni, paramiho na Ruvuma kwenye mpira na debate. Nimeona mabweni ya Azimio na uhuru na vitanda vyetu vya madeka. Sikuona tu Ukumbi wa misosi na mikutano ambako maharage ya binga yalikuwa yakitumika. Sikuona mashamba ya mahindi, maharage na malegea. Mimi nilikuwepo huko enzi za utawala wa Mzee Mbao. Walikuwepo akina Mwanyigu, HP wa Mkinga, Ndimbo, Mwihava, Marehemu Mahinya, Maunga na Clamp.
   
 17. Whisper

  Whisper JF-Expert Member

  #17
  Feb 19, 2012
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 502
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Duh!! Kumbukumbu zako ni sahihi. Form Five unakaribishwa na uvunaji wa marejea, kidogo niingie chaka, sikujua kama ni bonge la skuli. Ila umemsahau mzee wa dispensary anaitwa Kidato. Hilo Isuzu tulikuwa tunaliita Mustini. Mdau hajatutendea haki kuiacha picha ya bwalo letu na uwanja wetu wa Basketi wenye sakafu ya matofali. Nakumbuka maji yakikatika tulikuwa tunakwenda kuoga chemchem.

  Nakumbuka vijana waliokuwa wakitoka kusini tulikuwa tunawaita Mawia. Tulikuwa tukishinda Mbuzi ya ligi ya mabweni wanakula mpaka ngozi ya mbuzi. Vyoo vya DANIDA tulikuwa tunaviita Milango, ukitaka kwenda ni lazima uvue nguo zote la sivyo hautaweza kukaa na wenzako tena maana utakuwa unanuka mavi.
   
 18. Jeff

  Jeff JF-Expert Member

  #18
  Feb 19, 2012
  Joined: Sep 26, 2009
  Messages: 1,218
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  huyu mzee mbao nafikiri ndio alihamia mkwawa high school,
   
 19. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #19
  Feb 19, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  YA shULE rAHA SANA HASA UKISHAPITA HALAFU UKAYAKUMBUKA
   
 20. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #20
  Feb 21, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35

  Mzee umesahau vyoo vya Danida watu tulikuwa mpaka tunalia bondo! Vyoo vya kuvua nguo na kuziba pua vilikuwa vinaitwa milango saba. Pale ilikuwa nguo unaziacha umbali kama wa mita mia. Ukitoka unatoka mbio ili usitoke na upepo wa milango saba. Mawia we acha tu walikuwa moto wa kuotea mbali. Wengi wao walikuwa o'level. Siku ya punga walikuwa wanaruka mpaka juu ya meza! Du hizi srori raha kweli. (TWO MAMBO?- Hivi yuko wapi siku hizi?). (Na mzee wa kuchota?)


  M
   
Loading...