Soko la kuuza umeme bongo lipo tena ni la uhakika.
I think na mimi niingie kwenye mchakato wa kununua hiyo mitambo ya Dowans endapo Songas watashindwa.
Je, nikinunua hiyo mitambo hamtatumia umeme utazalishwa na mitambo hiyo?
Naona Mr. Mkandara bado yuke kule kule kwenye siasa za kijamaa. Hapa tunazungumzia a business proposition. Hizo sentiments zenu za kisiasa hazina nafasi hapa. Tena mkisema songas ni wazungu ndio kabisaa.
Ahsante sana kwa kashfa yako. Sisi umetufikiria hivyo, sijui wewe nawe ukichunguzwa utakutwa kwenye kundi gani. Ni Mlalahoi kweli au umejaa kishenzi, isipokuwa tu malalamiko yako kwa hao mafisadi ni washindani wako wa kishughuli tu (kama kulangua viwanja!!). Conflic of interest???
Soko la kuuza umeme bongo lipo tena ni la uhakika. Je, nikinunua hiyo mitambo hamtatumia umeme utakaozalishwa na mitambo hiyo?
Tunawashukuru Songas kwa kutuondolea kiwingu."Hata kama tukihitaji kununua mitambo ya kuzalisha umeme, bado hatuwezi kununua mitambo iliyokwishatumika kwa sababu hiyo si sera ya Songas.
"Unafahamu kazi ya kuzalisha umeme ni ngumu na inahitajika kuwa na vifaa imara na vyenye uwezo mkubwa, hivyo itakuwa jambo la kushangaza tukiingia kwenye mchakato wa kununua mitambo hiyo yenye mgogoro mkubwa hapa nchini.
"Pili Songas ni kampuni inayoaminika na yeye uwezo mkubwa kifedha, hivyo itakuwa jambo la kushangaza tukijiingiza kwenye mgogoro wa kununua mitambo ya Dowans."
Dawakali,
Mkuu hizi ni tetesi tu Songas inaongozwa na wazungu na nakuhakikishia hawawezi kununua mitambo ya Dowans kwa sababu ambazo sisi tumezitaja, Haiwezekani! hawaihitaji mitambo hiyo isipokuwa sisi ndio tunalazimisha..ni swala la logic tu kwa mfanya biashara..
Na kama mnafikiria yatakuwa basi tusubiri ukweli unless Tanesco wenyewe wananunua kwa kutumia hadithi ya kwamba Songas wamenunua..
You were right to the point jamaa wamechomoa kwa kusema kama waliokuwa wakipinga kuwa hawawezi kununua mitumba. sasa tunasubiri tk na mtanzania washabiki vipofu wa dowans sijui watakuja na longolongo gani
Tulisha waeleza in business terms kwanini Songas aiwezi kununua mitambo ya Dowans, watu wakasema tunaongea siasa. Lakini as presumed, Songas wamerudi na jibu hilo hilo.Kama investors wa Kiwira wamekimbia kwasababu ya politics, nita washangaa sana Songas kujiingiza katika mzigo very risky kama huu wakununua mitambo ya Dowans ambayo politically ni very sensitive nchini. Sidhani kama Songas watataka kujiiniza kwenye situation just for 100Mw and jeopardise investments zao. Kwahio this deal does not make sense
Cpt Hadock,
You are missing the point here, binafsi sishabikii Dowans wala sina maslahi yoyote na Dowans, ninachosema tutumie sababu za kiuchumi kuamua kama tunataka kununua au la na wala sio sababu za kisiasa. Kama hakuna sababu za kiuchumi, basi hakuna haja ya kununua, hiyo ndio point yangu tokea mwanzoni. Kitu ambacho mimi napinga ni hii sababu ya kwamba tusinunue kwasababu Dowans watafaidika, kwa mimi ningeangalia je taifa litafaidika?
Kama Songas wametumia sababu za kiuchumi kutoa uamuzi wao mimi niko happy nao. Pia wao wamesema hawana tatizo na uzalishaji wa umeme. Kama wameogopa kuwa PR dissaster pia nitawaelewa maana ni hatari kwa private investor kuwa kwenye vita na wananchi, PR inakataza unless kuwe na maslahi makubwa sana kwenye hilo jambo.
Kwa Tanesco matatizo yao ni kuingiza siasa badala ya kutafuta solution. Miezi inaenda hakuna kinachofanyika na hapo ndipo kwenye tatizo. Tutaendelea kubishana hapa lakini tatizo liko pale pale na uzalishaji TZ unaenda chini shauri ya matatizo ya umeme.
Tanesco wameshaamua hawanunui hiyo mitambo, sawa, lakini pia inatakiwa pia watuletee solution nyingine haraka.