Lavan Island
JF-Expert Member
- Oct 24, 2015
- 2,377
- 2,048
Wanandoa waliokuwa ndio kwanza wanaanza maisha walihamia katika mtaa mmoja na kupanga nyumba katika eneo hilo,Siku ya pili wakiwa wanapata chai asubuhi mke alimwona jirani kwa mbaali kupitia dirishani akianika nguo alizotoka kuzifua.
Mke akamwambia mumewe nguo zile hazikufuliwa vizuri na hazikutakata yule mama hajui kufua nguo au anahitaji sabuni nzuri zaidi,Mme alitazama pia ila hakutamka neno zaidi ya kukaa kimya.
Ikawa kila siku yule jirani anapo anika nguo yule mama lazima angeongea neno kwani nguo bado zilikuwa zinaonekana hazikutakata.Baada ya mwezi mmoja hivi siku moja yule mama aliamka na kushuhudia yule jirani akianika nguo zilizo fuliwa na kutakata vizuri sana,bila hata ya kusubiri alimwambia mumewe.
Woow angalia mume wangu yule mama kapata somo sehem angalia alivyofua nguo na kutakata vizuri sijui nani kamfundisha.
Mme akasema nimeamka leo mapema na kuyasafisha madirisha yetu,na ndio maisha yetu yalivyo kile tukionacho kwa wenzetu kinatokana na usafi wa madirisha yetu jinsi yalivyo.
Ni rahisi kwa sisi kuongea mengi juu ya wenzetu na maisha yao ambayo sisi hayatuhusu,Na tunasahau kuwa sisi ni wachafu zaidi.