Somo nililojifunza McDonald Restaurant

unajua haya mambo ya kuteuliwa na mara Rais, mara Waziri/Mtu influential ka-influence fulani ateuliwe............ndiyo yanayoturudisha nyuma sana........kwa sababu watu wanawajibika huku akikumbuka fadhila za kupewa ulaji na Rais au Waziri/Mtu influential.......na matokeo husahau kuwatumikia wananchi................na ndio maana hata kujiuzulu kwao........eti kwa manufaa ya umma inakuwa jambo la ajabu
 
Tatizo la viongozi wetu, na labda Watanzania kwa ujumla, ni kwamba hawajawahi kufanya kazi McDonalds.

Watanzania wengi ambao hawapata kuishi nga'mbo hawajui kazi maana yake nini.

Nafikiri kati ya viongozi waliopo sasa wengi wasoma nje ya nchi. na hao walio ubalozini wengi pia kama sikosie wamepitia huko na ku panga mabox na kufanya kazi mcdonald, lakini bado wako hivyo hivyo. tena usishangae wengi wanao haribu ndio waliso kaa nje ya nchi zaidi na kufanya hizo kazi sana tu.

kwa mtazamo wangu hili tatizo ni la kijamii ya watanzania wote (ingawa kwa sasa tunawaona hawa waliopo). na sema ni lakijamii kwa maana hatujalelewa katika mazingira ya kupanga na kuchagua. familia zetu wengi hatujui hata kwa mwaka kipato chetu ni shilingi ngapi, na katika hizo zipi zinatumika kwa nini. kikubwa ni kwamba ipo inatumika haipo tunakopa kwa jirani. ilimradi siku imepita. ya kesho yatajulikana kesho.

wangapi wanaosimamia bajeti yetu wameshawahi hata kuwa na mpango wa miaka miwili nyumbani kwao wa nini anataka kufanya na atapata wapi pesa na matumizi yatakuwaje. sasa kama mtu hajalelewa katika mazingira hayo ya kuwa na mipango na namna ya kuikamilisha, unapompa mpango wa matumizi anaona ni yayle yale tu, kesho zitapatikana nyingine tu.

kikubwa ni kwamba katika familia zute kwa watoto na wakubwa hakuna Immediate consequences za kutopanga. Kama mjadala unavyokwenda kwa wenzetu kidogo tu hauna kazi. inabidi haya mambo tuyaanzie mbali kwa watoto wetu ili wao wasije wakawa kama sisi. wajue kupanga, wajue wasipopanga kuna consequences tena hasi sio chanya.

lakini kwa sisi sasa ndio ipo kazi tanajitahidi kujifunza siku zinavyo kwenda, haya tuiowapa kazi zetu, pia tumewagaramia ili waweze kupata amabyo wenzetu kwa kiasi kikubwa ni sehemu ya maisha yao. na tunaowaliosoma kweli kweli. lakini bado moja ambalo MMk analisema, hatujajifunza kutoa adhabu pale mtu anapoonyesha udhaifu. wengi wetu kwa viboko (ingawa siku hizi havikubaliki) tulibadilishwa mienendo yetu iloyokuwa inakwenda kushoto, na wadogo zetu wakajifunza baada ya kuona kaka na dada wanagugumia maumivu ya viboko. tunahitaji hili kwa watendaji wetu, kama tumewapa nyezo na uwezo wakufanya vyote sawa halafu kwa makusudi hawatekelezi vilivyo adhabu ni muhimu sana.

tukiwadhibu basi kesho watajua nini lakutegemea tukiwapa nafasi nyingine. Naamini bila adhabu tena kali Tanzania kujikwamua hapa tulipo itakuwa ngumu. ndio nitatizo la kijamii ila Adhabu ni muhimu sana katika kufundisha. shuleni adhabu ya kukosea mtihani ni kunyimwa maksi, katika maisha adhabu ya kukosea kuitumikia jamii vizuri kunyimwa nafasi ya kuitumikia tena (nafikiri)
 
Mzeeba, I couldn't agree with you more, Excellent post with so much wisdom!
 

Umeenda umezunguka halafu umerudi pale pale kwenye nilichokisema na Mwnkjj: hakuna work ethics grounded in accountability kama za MickyD au workplace nyingine yoyote ya nchi zilizoendelea.

Na point yako ya kusema tuanze kuwafundisha watoto consequences za kutokupanga ni nzuri lakini ipo misplaced au incoherent katika mada ya accountability kazini kwa sababu umeshasema watoto wanachapwa fimbo toka mwanzoni lakini wakifikia kazini hawajajifunza bado. Kwa hiyo I guess kuwafundisha na bakora toka utotoni hakusaidii kuwafundisha accountability.

Tatizo ni work ethics za McDonalds au workplace ya nchi zilizoendelea hakuna. Wabongo hatujajua kazi maana yake nini.
 
Je kazi ni mahali pa kupata mapato (njia ya kujipatia mshahara na kipato) au pia ni mahali pa kutoa huduma na bidhaa? Je mtu anaweza kuwa na kazi bila kuhakikisha anatoa huduma nzuri na bidhaa nzuri as long as anapata kipato chake?

Makampuni kama MacD pamoja na utani mwingi dhidi yao they exist because of service and not just service but good and quality service. Wakifanya biashara mbaya mtu haiendi kula hapo tena. So it is in their interest to provide excellent service. Na hilo linalazimishwa kwa kuweka matokeo ya kazi mbaya na usimamizi mbaya.

Kwetu sisi hofu yangu ni kuwa bado kuna watu ambao hawajali what kind of service/products wanatoa au ina ubora gani as long as wao wanalipwa. Watu hawa hawajali sana kama taratibu za kazi zinafuatwa as long as at the end of the month wanapatiwa mshahara wao. Sasa kwa watu hawa, kutotia sahihi karatasi fulani, kutohoji malipo fulani n.k (kama nilivyoonesha hapo mwanzo) kwao si tatizo kwani at the end of the day kesho wakija kazini kibarua kipo, gari lipo, na fedha nyingine zipo.

Ndio maana miaka kadhaa iliyopita nilitoa pendekezo la kuwapa viongozi uwezo wa kumfukuza mtu on the spot na kuwa na ajira za "at will" ili watu wajue kuwa at any given time you can be replaced.

Just imagine, kesho usikie Waziri fulani amefukuza kazi so and so kwa uzembe. Hakuna cha mahakama wala nini unafikiri huyo mwingine atakayeingia atasikia yuko salama? We can force responsibility in people by using forceful means. Uzembe should never be tolerated nor incompetence rewarded.
 
Nadhani ni vizuri kukawa na due process katika ufukuzaji kazi
 
Tusimumunye sana, Wabunge Kenya wanataka roho ya Waziri wa Fedha kwa Uzembe na Ulaghai, sisi kinatushinda nini?

 
Employment at Will.

How come it creates accountability, productivity, efficiency, responsibility and loyalty? Why Tanzania iwe ngumu? Would this be a motivation for people to pay attention to their jobs and expectations?

 
La nyongeza

 
Mimi nikisema Waafrika Ndivyo Tulivyo naambiwa eti nina complex.......
iferiority complex.....!
JE HAO COLOURLESS HAWANA MAPUNGUFU.....? the tatizo hao wenye matatizo washughulikiwe, na si wote wenye matatizo....!
 
Nadhani ni vizuri kukawa na due process katika ufukuzaji kazi

siyo katika nafasi zote, due process mojawapo ni one is being employed "at will". That is "due" enough.

Hata wale wa kwenye mikataba, we have to create mikataba ambayo inakuwa rahisi kuwawajibisha na wakati huo huo kuwazawadia wanapofanya vizuri.
 
Mwanakijiji,

Jana baada ya kulonga, mara tatu nilipotaka kuanzisha thread kuhusiana na hiyo ripoti ya CAG, Comcast wakawa wanaleta kokoro, nikashindwa kuiposti. Nilikwenda kuisoma ile ya Kizungu, maana ya Kiswahili lugha za kihasibu zanipiga chenga.

Bottom line is this, we do not have an accountable government period!

Siyo Raisi, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Bunge, Mahakama, Wabunge, Makamishna, Taasisi, Kurugenzi or whatever, kila mahali kuna "ujanja ujanja" na kukosekana kabisa miiko ya kimahesabu na kiuhasibu.

Hivi kweli tuna Serikali au ni vikatuni-vikaragosi ndio walio viongozi? Inakuwaje Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Taasisi ambazo zina historia ya ufujaji wa pesa na kukosa nidhamu ya pesa za umma na matumizi yake wanaendelea kushikilia nyadhifa zao?

Kama wao wakiwa wakubwa wanashindwa kuhakikisha kuna uwajibikaji, je wanafikiria ni vipi Taifa linaweza kuwa na Maendeleo?

Hivi kazi yote na mapendekezo ya Mkaguzi Mkuu hutupwa Chooni?

Nitabandika hapa mengine ya ziada mujionee wenyewe ni jinsi gani Tanzania ni kichwa cha Mwendawazimu na mjiulize kosa la nani na kwa nini tunaendelea kuwa Wanyonge na Masikini!



Kila kitu hapa ni irregularity! Ina maana tumesha halalisha Irregularities!​

 
Wanabaraza,
Tanzania kuna tatizo kubwa kuliko linavyoonekana kwa nje. Ni tatizo la jamii kukumbatia ufisadi. Yaani watanzania bado hatujaona kwamba utajiri unaopatikana kwa njia isiyo halali ni utajiri unaonuka. Ni wangapi kati yetu wakipewa nafasi katika hizo ofisi za serikali hawatakula bila kunawa mikono? Jihoji nafsini mwako na uwe mkweli kwako mwenyewe kwanza.

Tanzania sasa hivi tunadanganyana. Serikali inadai inalipa wafanyakazi wake kumbe haiwalipi kitu. wafanyakazi nao wanaidanganya serikali kwamba wako kazini kumbe hamna kitu. Ni kudanganyana tu. We fikiria mtu ana shahada ya uzamili(masters degree) analipwa laki 2 na nusu kwa mwezi. Mtu huyo ataishije bila kuwa na njia zinginezo? Mtu huyo halipwi bali anadanganywa kwamba analipwa!!!! Mtu anaingia kazini saa 2 anatoka 9.30 mchana na hapo amekwenda lunchi saa 7 hadi 8.30 mchana. Pia amekuwa akisoma tu jamii forums tangu asubuhi. je, mtu huyo amefanya kazi kweli? Ni udanganyifu pande zote

Ili mtu afanye kazi lazima ana kitu anachotegemea, sasa huko serikalini mtu anafanya kazi ili apate nini ilihali mshara hakuna. Ni wazi mtu anfanya kazi ili asafiri nje ya cnhi au apate safari ya kikazi nje ya kituo au apate extra duty allowance au aweze kuunganisha deal apate hela ya kufika mwisho wa mwezi

HII NDIO HALI HALISI SERIKALINI.

Tuendelee na mjadala sasa
 
Kwa haraka haraka pesa ambazo matumizi yake yana utata ni karibu Shs 2,800,000,000,000.00 au dola za Kimarekani Billioni 2.2 ukichanganya Mikoa, Wizara na Idara!

How in the hell can we have such huge discrepancies in our money?
 
I've said it before, I'll say it again, Watanzania we are not serious... karibu trilioni 3 hazina maelezo ya kueleweka, yaani ndio zishakwenda hivyo na hakuna consequences zozote kwa wahusika?! Halafu mheshimiwa rais anashangaa akidai hajui kwanini umasikini umetuandama namna hii...
 
Mimi naomba kujua, hivi tutaumia nahizi report na kujibiwa mikato na wahusika mpaka lini, hivi hamuoni kuwa kuna haja ya kubadili strategy??
 
Mimi naomba kujua, hivi tutaumia nahizi report na kujibiwa mikato na wahusika mpaka lini, hivi hamuoni kuwa kuna haja ya kubadili strategy??

Yes we need to change strategy, so which one? may be Tuandamane,

Mko wapi vyama mbadala? itisheni maandano nchi nzima tuwaunge mkono, tupaze sauti kila kona kwa hawa watawala wetu waweze kutimiza wajibu wao, hizi pesa zisizo na maelezo zirudishwe, wahusika wakamatwe na kufilisiwa, na kama hawawezi wastep down waachie vichwa vifanye kazi nchi isonge mbele!
 


Forget Political Parties...we Need Pressure Groups zenye kujua kazi.



One thing to give credit for ni huyu Mkaguzi Mkuu wa Serikali...hizi ripoti zake katika miaka ya karibuni zimekuwa na UWAZI na pia zinaandikwa kitaalamu kuliko miaka ya nyuma...bado kunahitajika kuboreshwa zaidi isipokuwa jitahada zake zinaonekana.
 
Haya ni madhambi ambayo hawayakutaka kuwekwa hadharani na kujuilikana lakini kwa vile serikali wameona kuwa watanzania ni mazuzu na hata yakifanyika madudu hawafanywi kitu na tutaendelea kupiga kelele na wao wanasema kelele za mpangaji hazimwachi mwenye nyumba kulala.

Kama hatukubadilisha mbinu za kuleta mabadiliko katika nchi hili genge litafanya litakavyo na hakuna litalobadilika. Kwa nini tusianzishe Kampeni ya kudai katiba mpya ambayo wengi tunakubaliana kuwa ndio njia muafaka ya kupunguza makali ya serikali ya Chama kimoja.

Kelele na kufichua maovu sipingi zinaweza kuleta mabadiliko lakini ni ya pole pole sana na tunaweza kuwa vizee au hata kufariki na mabadiliko hayajatokea kwani kama hawa ni watu wa kuona soni wasingeanika ripoti hiyo hadharani na hata wasiwe na kitetemeshi - hii ni sawa na kuzini na mke wa mtu na ukaingia chumbani mwao na mume yuko ukumbini anakuona.

Masikini nchi yangu Tanzania.
 
Kwa haraka haraka pesa ambazo matumizi yake yana utata ni karibu Shs 2,800,000,000,000.00 au dola za Kimarekani Billioni 2.2 ukichanganya Mikoa, Wizara na Idara!

How in the hell can we have such huge discrepancies in our money?

Rev,

Haya mambo ndiyo yananipelekea mimi kuitisha Kikwete astaafu maana sasa haya ni makusudi na sio bahati mbaya. Nchi imepoteza mwelekeo kabisa na hakuna anayejali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…