Somo nililojifunza McDonald Restaurant | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Somo nililojifunza McDonald Restaurant

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 2, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 2, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ukifanya kazi McD hasa kwenye cashier register hawaruhusu cash register yako iwe na upungufu wa zaidi ya dola mbili mwisho wa mauzo ya siku. Ukiwa na upungufu huo mara tatu wanakutimua!

  Kwa muda sasa nimekuwa nikipitia ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa serikali ya mahesabu ya serikali ya mwaka wa 2006-2007 ulioisha Juni 30, 2007. Ingawa nimekuwa nikipitia ripoti hiyo mara kadhaa lakini jana kwa namna ya pekee it hit me! Hatuna usimamizi wa fedha (which is understatement); siyo tu ripoti yenyewe inashtua lakini mambo yanayotajwa yanaudhi na kama una moyo mwepesi unaweza kujikuta unapata kiungulia cha ubongo.

  Hebu angalia mifano ya kile ambacho CAG alikigundua katika uchunguzi wake na maneno anayotumia kuelezea.

  Jeshi la Wananchi:
  Malipo bila hati za malipo (payments without payment vouchers) Sh.614,980,930

  Malipo yenye shaka kwa Meremeta Ltd = 200,980,370

  • Kitengo cha ukaguzi wa ndani hakijawahi kutoa taarifa ya
  ukaguzi

  Shirika la Mzinga
  Hati ya Ukaguzi: Yenye Shaka
  Masuala yaliyopelekea kutoa hati hiyo
  • Amana na malipo ya awali ya muda mrefu ambayo
  hayajashughulikiwa Sh.6,091,761,309

  Vipuri visivyotumika vyenye thamani ya Sh.252,216,000vimeendelea kuonyeshwa katika taarifa za fedha za Shirika la
  Nyumbu kwa miaka 15 iliyopita bila kufutwa kwenye vitabu.
  • Jumla ya Sh.220,019,955 zililipwa kwa Kampuni ya Kimataifa
  kwa ajili ya vifaa ambavyo hadi sasa havijapokelewa.

  Wizara ya Mambo ya Nje
  Malipo ya ruzuku kwa Chuo cha Diplomasia yasiyotolewa
  maelezo Sh.1,531,278,729

  Wizara ya Mifugo
  Ng’ombe wa maziwa wenye thamani ya Sh.86,000,000walionunuliwa hawakupokelewa.

  Tume ya Ukwimi Tanzania
  Matengenezo yenye thamani ya Sh.2,023,560 yalifanywa
  kwa Mkandarasi asiyeidhinishwa
  • Matumizi ya kiasi cha Sh.16,030,000 hayakuwa na nyaraka

  Msajili wa Vyama vya Siasa
  • Taarifa za mwaka za hesabu zilizokaguliwa za vyama vya
  Siasa zinazoonyesha matumizi ya jumla ya
  Sh.13,667,340,694 hazikuwasilishwa kwa Msajili wala
  kutangazwa

  Balozi zetu kadhaa
  London – Uingereza
  Masuala ya msisitizo
  • Matumizi ya Sh.2,379,251,838 nje ya bajeti iliyoidhinishwa
  • Usimamizi dhaifu wa mali za kudumu
  • Malipo ya awali kwa ajili ya pango £ 7,200 hazikurejeshwa
  kwa balozi.

  Paris – Ufaransa
  Masuala ya msisitizo
  • Matumizi bila idhini sahihi Sh.1,171,099,881

  Berlin – Ujerumani
  Masuala ya Msisitizo
  • Matumizi zaidi ya bajeti Sh.301,016,847• Mafuta ya magari yasiyoingizwa vitabuni Sh.20,532,535

  New York – Umoja wa Mataifa• Kuchelewa kupeleka benki fedha zilizokusanywa
  Sh.116,601,861• Matumizi zaidi ya idhini Sh. 66,840,160• Kuripotiwa pungufu kwa matumizi Sh.38,236,905• Fedha isiyorejeshwa Sh.25,130,225
  • Kukosekana kwa hati za malipo Sh.255,628,000

  Washington – Marekani• Malipo yaliyofanywa bila ushindani wa bei Sh.32,966,854• Matumizi yasiyo na nyaraka Sh.85,278,900
  • Kandarasi na Zabuni zilizotenganishwa ili kuidhinishwa
  kinyume cha Sheria Sh.58,340,972• Kuidhinishwa kwa kandarasi kwa kiwango kinachozidi uwezo
  wa Afisa Masuuli mdogo Sh.65,784,765

  Cairo – Misri
  • Malipo yasiyokuwa na nyaraka yaliyofanywa na mwambata
  wa Jeshi Sh.190,352,770

  My Take:[/B]

  I can't take anything! Nimewaambatanishia ripoti ya Serikali Kuu (unaweza kusoma ripoti nyingine kwenye http://www.nao.go.tz na ukipitia pitia unaweza kuona vitu vingine vingi ambavyo vinaweza kukusababishia lile jinamizi la utotoni kukurudia!
   

  Attached Files:

 2. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Ndio maana kuna haja ya kufanya kazi kwa kina ili kuhakikisha kuwa mafisadi wa kisiasa wanaondoka kwani najua kuwa hata hawa watendaji watakuwa makini sana .

  Pili ripoti hii ni nzuri kuliko ya mwaka jana kwani imeonyesha upotevu wa pesa ila sio nyingi kama mwaka jana japo fedha zilitolewa nyingi kwa kipindi cha mwaka huu.

  Kuna kazi kubwa sana ya kufanya siku za huko mbeleni kwani kunahitajika total overwhal kwenye leadership ya taifa hili .

  We are in leadership crisis now.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Jul 2, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hivi inakuwaje mtu anawasilisha ripoti ya malipo bila risiti, tena ya mamilioni ya shilingi halafu mtu huyo kesho yake anarudi tena kazini? Inawezekanaje mtu ananunua kitu bila risiti na kitu hicho hakipokelewi halafu bado anaendelea na kibarua kesho yake? Inakuwaje mtu anaamua kumlipa mkandarasi kwa fedha za umma bila idhini halafu mtu huyo kesho yake anarudi na tai yake ofisini? Tukisema serikali imeubeba ufisadi kama mtoto kwenye mbeleko tutakuwa tunawazushia?
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Jul 2, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Mimi nikisema Waafrika Ndivyo Tulivyo naambiwa eti nina complex.......
   
 5. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2008
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0


  THEORY OF MCDONALDIZATION, Watu wanafikiri hizi zinabakia kuwa theory za kwenye vitabu, hata kwenye uongozi pamoja na maisha yetu kwa ujumla yanatendeka. Mkuu Mzee Mwanakijiji nimekupata sana, Analysis Hii imetulia mno.
   
 6. M

  Mgaya JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 520
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  waafrika ndivyo tulivyo na kama watu wanabisha wamuulize mugabe wa zim
   
 7. M

  Maskini Mimi Member

  #7
  Jul 2, 2008
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KWA UFAHAMU WANGU WA SHERIA ZA KODI, UNAPOKAGULIWA NA TRA WAKIKAMATA MANUNUZI YASIYO NA STAKABADHI (DOCUMENTARY EVIDENCE), TRA WATAKULIMA NA ASSESSMENT NA KUKDAI KODI AMBAYO NI PAYABLE WITHIN 30 DAYS -IF NOT 10 DAYS.

  KWA MANTIKI YA HAPO JUU, HAO WALAFI/MAFISADI LAZIMA WACHUKULIWE HATUA KWANI TAX IS SAID TO BE FAIR TO ALL CITIZENS, LAKINI KWA NINI WATU WACHACHE WAENDELEE KUIBA TU BILA YA KUCHUKLIWA HATUA ZA KINIDHAMU. UTOUH ALISHAKUWA MKUU WA NBAA KWA MUDA MREFU, HIVYO KITU CHA KWANZA NI KUWAADHIBU HAO WAHASIBU AMBAO WANAENDELEZA HUO UWIZI, HALAFU NDIO WAKUU WA SYSTEM WAADHIBIWE PIA.

  Jee tutafika na mpango huo wa uwizi. TRA wako speed kuwakamata waliipa kodi wa kawaida lakini wakuu wa idara wanatakiwa wafuatiliwe na idara yenye nguvu zaidi ya TRA na NAO.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Jul 2, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Maskini.. kama Utoh hana nguvu za kufanya hivyo itakuwaje?
   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,596
  Likes Received: 1,996
  Trophy Points: 280
  HII NI KUFURU!
  UHAI WA WATZ UNACHEZEWA!
  Wanawezaje kufuja pesa zote hizo na huku kuna wananchi wanakufa kila siku kwa njaa na magonjwa?
  Na kweli nimeshaona kama hao watu hawatachukuliwa hatua tena na sisi yanaweza kutukumba ya wenzetu kama ya hapo kwa BABA MOI.
   
 10. M

  Maskini Mimi Member

  #10
  Jul 2, 2008
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KWA UFAHAMU WANGU WA SHERIA ZA KODI, UNAPOKAGULIWA NA TRA WAKIKAMATA MANUNUZI YASIYO NA STAKABADHI (DOCUMENTARY EVIDENCE), TRA WATAKULIMA NA ASSESSMENT NA KUKDAI KODI AMBAYO NI PAYABLE WITHIN 30 DAYS -IF NOT 10 DAYS.

  KWA MANTIKI YA HAPO JUU, HAO WALAFI/MAFISADI LAZIMA WACHUKULIWE HATUA KWANI TAX IS SAID TO BE FAIR TO ALL CITIZENS, LAKINI KWA NINI WATU WACHACHE WAENDELEE KUIBA TU BILA YA KUCHUKLIWA HATUA ZA KINIDHAMU. UTOUH ALISHAKUWA MKUU WA NBAA KWA MUDA MREFU, HIVYO KITU CHA KWANZA NI KUWAADHIBU HAO WAHASIBU AMBAO WANAENDELEZA HUO UWIZI, HALAFU NDIO WAKUU WA SYSTEM WAADHIBIWE PIA.

  Jee tutafika na mpango huo wa uwizi. TRA wako speed kuwakamata waliipa kodi wa kawaida lakini wakuu wa idara wanatakiwa wafuatiliwe na idara yenye nguvu zaidi ya TRA na NAO.
   
 11. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,596
  Likes Received: 1,996
  Trophy Points: 280
  Tunaomba tuwekewe na majina ya hao walioidhinisha hiyo KUFURU hapo juu.
  Tafadhali tunaomba muweke majina yaliyoidhinisha!
  Ahsante.
   
 12. M

  Maskini Mimi Member

  #12
  Jul 2, 2008
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkjj, we need to acquire a new vehicle since overhaul will not help, since the vehicle is beyond repair!
   
 13. M

  Maskini Mimi Member

  #13
  Jul 2, 2008
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KWA UFAHAMU WANGU WA SHERIA ZA KODI, UNAPOKAGULIWA NA TRA WAKIKAMATA MANUNUZI YASIYO NA STAKABADHI (DOCUMENTARY EVIDENCE), TRA WATAKULIMA NA ASSESSMENT NA KUKDAI KODI AMBAYO NI PAYABLE WITHIN 30 DAYS -IF NOT 10 DAYS.

  KWA MANTIKI YA HAPO JUU, HAO WALAFI/MAFISADI LAZIMA WACHUKULIWE HATUA KWANI TAX IS SAID TO BE FAIR TO ALL CITIZENS, LAKINI KWA NINI WATU WACHACHE WAENDELEE KUIBA TU BILA YA KUCHUKLIWA HATUA ZA KINIDHAMU. UTOUH ALISHAKUWA MKUU WA NBAA KWA MUDA MREFU, HIVYO KITU CHA KWANZA NI KUWAADHIBU HAO WAHASIBU AMBAO WANAENDELEZA HUO UWIZI, HALAFU NDIO WAKUU WA SYSTEM WAADHIBIWE PIA.

  Jee tutafika na mpango huo wa uwizi. TRA wako speed kuwakamata waliipa kodi wa kawaida lakini wakuu wa idara wanatakiwa wafuatiliwe na idara yenye nguvu zaidi ya TRA na NAO.
   
 14. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #14
  Jul 3, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280


  Loh, hiyo inaumiza kweli kweli. Halafu nikisema tunataka Tanzania iwe na highway za njia mbilimbili waziri anasema serikali haina uwezo wa kufanya hivyo.

  Hapa sifanyi ushabiki wa kisiasa, ila ninapenda kujua eti hizo Taasisi zote ni za serikali inayoongozwa na chama gani. Kuna haja ya kufanya mageuzi ya dhati sana ili kumaliza matatizo haya. Watu husema ukikuta nyoka wa sumu ndani ya nyumba yako, mpige kichwani kwa nguvu sana. Ama sivyo atakusumbua sana na anaweza kukutemea mate yakakudhuru
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Jul 3, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,818
  Likes Received: 83,217
  Trophy Points: 280


  Kwenye ofisi zetu za ubalozi kuna ufisadi wa hali ya juu unaofanywa katika manunuzi ya nyumba au ofisi, matengenezo ya nyumba hizo au ofisi lakini hakuna yeyote aanayejali. Wanaweza wakafanya matengenezo ya pound 200 wakapeleka bill ya pound 20,000 yaani ni wizi wa hali ya juu ambo unasikitisha sana. Kweli Mvunja nchi ni Mwanachi
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Jul 3, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mimi kinachonisumbua ni jinsi watendaji wanavyokiuka taratibu with impunity! Yaani ni sawa na wale ambao wanaona kuna mahali panasema "Stop" na wao wanaendelea kana kwamba ile "Stop" inasema "ongeza mwendo" Ukiwauliza kwanini wanasema hawakudhani ile alama ina wahusu wao!
   
 17. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #17
  Jul 3, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Tatizo la viongozi wetu, na labda Watanzania kwa ujumla, ni kwamba hawajawahi kufanya kazi McDonalds.

  Watanzania wengi ambao hawapata kuishi nga'mbo hawajui kazi maana yake nini.
   
 18. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #18
  Jul 3, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mwanakijiji,

  Experience yako ya Mcdonalds sio tofauti na ya kwangu ambayo nilijifunza kuna kitu kinaitwa discipline, accountability na responsibility. Katika kufanya kazi kwangu Tanzania atmosphere ilikuwa laid back kidogo, ila nilipofika huku hawachezi. Discipline inatokana na kitu unachokiamini na uko tayati kukifanya, kwa mfano, kufika kazini on time sio in time. Na kuwajibika hasa. Na mtu anayecheza na kazi anakuwa disciplined ipasavyo pamoja na kufukuzwa kazi, kupewa onyo au kuwa trained upya.

  Discipline ni mtu kuji-programu kuwa hata kama mtu hakuoni utafanya kila kitu sawa bila kusubiri mtu wa kusukuma au kukuuliza mbona hili ulikosea na hujalirekebisha. Sasa Mkaguzi mkuu anaonekana kukosa vyote vitatu, discipline, accountability na responsibility. Kama kuna yote haya na yeye anaridhika kutoa report tu bila ku-question au kuchukua hatua ambazo nafasi yake inaweza kumruhusu then I guess hata akifufuka mfu na kumletea ujumbe wa responsibility na discipline hawezi elewa. Sina maana ya ku-undermine his capability and abilities to excute his duties but I rather find him more wanting.
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Jul 3, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kuhani umenichekesha kiasi kwamba natamani kuanzisha a MacDonald. Si nasikia Bongo na wenyewe wameanzisha hizo fast food au wanafanya tofauti, Tanzania style?
   
 20. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #20
  Jul 3, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Zipo bongo fast food ila hazina u-fast wowote, unasubiri wakati mwingine utafikiri wameufata huo msosi outskirts. Ila kazi iwe kumuchangamsha huyu mkaguzi wetu kwa sababu akiwa anaendelea hivi hivi ni sawa na kama anaidhinisha ufisadi.
   
Loading...