Somo la uzalendo ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ ๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ธ

Uzalendo wa mtu kwa nchi yake uko kwenye vitendo vyake, matamshi yako na hata anavyojisikia moyoni mwake kuliko kwenye viashiria kama bendera na nyimbo ya taifa.

Na ukumbuke viashiria kama bendera au nyimbo za taifa kila nchi ina utaratibu wake, nchi kama Marekani hairuhusi kuinamisha bendera yao chini lakini nchi zingine duniani hawajali hilo.
 
Ramani tumechorewa,mfumo wa utawala tumewekewa , bendera yenyewe haina hata miaka 60...huo uzalendo ni wa nini hasa??
 
Tanzania nadhani ukipeperusha bendera nyumbani kwako huo ni msala...kama unabisha jaribu uone?

Ova
 
NAKAZIA:
TUKILINGANISHA DEMOKRASIA YETU NA MAREKANI TUSISAHAU KULINGANISHA NA UZALENDO WETU NA WAO.
 
Kwani unadhani Marekani kila raia anakubaliana na viongozi waliopo madarakani?

Umewahi kuona kwenye hafla ya kitaifa ya Marekani watu wanavaa nguo za vyama? Umewahi kuona huko Marekani vyombo vya dola kuonyesha wazi wazi kufanya upendeleo kwa chama kilicho madarakani? Umekosa vya kufananisha au na wewe unataka uonekane unajua kuanzisha uzi?
 
Kama ni hivyo basi hamna hata haja ya kuwa na bendera, siyo?

Kwani bendera ndio kipimo cha uzalendo zaidi ya alama ya taifa? Kwa hiyo ili ujue mtu ni mzalendo ni kwa kuweka bendera ya taifa alipo?
 
Hii Mada Ya Kuonyesha Uzalendo Kwa Kupeperusha Bendera Imenikaa Kwa Kweli.,,,,,,,wakuu Niombe Kuuliza Hivi Ikitokea Umeamua Kumiliki Bendera Yako Kiuzalendo ,,Taratibu Za Kuipandisha Na Kuishua Kila Siku Zitakuwa Ni Zile Zile Za Kupuliza Filimbi Ili Watu Wapitao Karibu Na Makazi Yako Wasimame Au Waweza Kuishusha Kiholela Tuu,,,,,, Halafu Nipende Kujuzwa Bei Ya Bendera 1 Na Mahali Pa Kuipata Hata Kama Ni Kwa Kufuata Taratibu
 

Maswali yako yamenichekesha ingawa ni ya msingi.
 
Ukitembea sehemu mbalimbali Tanzania pia utaona bendera za CCM zinapepea kwenye nyumba nyingi ,magari mengi nimeyaona yakiwa na bendera na nembo za CCM, ofisi nyingi zina picha ya Mh.Rais,huu wote sio uzalendo kwako?
 
Rangi za bendera ya Marekani ziko hadi kwenye chupi, vaa chupi yenye rangi za bendera ya Tanzania kama hujabambikiwa kesi eti umeidharau bendera ya Tanzania.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ