Mkuu ni kweli ushirikiano mara zote ni muhimu, lakini ni lazima tuwe makini.
Kulinda ajira, viwanda vyetu, uchumi wetu ni jukumu letu na hatuwezi kuliachia soko huria kufanya hivo ingawaje ushindani ni muhimu.
Hivyo basi tuhnahitaji wachumi wetu wawe wazuri sana kuona mashimo tunayoweza kutumbukia na kuvunja miguu ili tuweze kuyaepuka.
Suala la Ugiriki si utani, watu wamefikia adi kujinyonga kwa kuuziwa numba na maisha ya kistaarabu waliyoyazoea, na bado deni la taifa ni kubwa mno kiasi cha Ugiriki kuanza kuonekana kama 3rd world country.
Waingereza wale ni ligi tofauti sana, pamoja na matatizo yao yote hawajawahi hata kidogo kukubali nchi yao iingie katika Eurozone.
London bado ni a robust financial capital.