Somo la mathematics kuitwa ugonjwa wa taifa kwa wanafunzi

Somo la hisabati (kwa kweli masomo karibu yote) hayafundishwi vizuri. Kutoka shule ya msingi inajengwa taswira kwamba hisabati ni ngumu sana. Na walimu badala ya kuwaelekeza wanafunzi, wanatumia bakora pale mwanafunzi anaposhindwa.
Somo la hisabati ni mojawapo ya mihimili ya makuzi ya kielimu. Misingi ya mantiki, muhimu katika uwanja wowote wa fikra na taaluma, huanzia katika kujifunza hisabati. Lazima tufanye mabadiliko katika ufundishaji wa somo hili muhimu.
 
Pana hitajika juhudi za pamoja kuanzia Kwa wazazi wanafunzi na walimu kwa ujumla ili kuongeza ufaulu wa somo hilo, vilevile serikali kuwajengea mazingira wezeshi walimu na mtaala usibadilika badika mara kwa Mara.
 
nisomo rahisi sana kuliko hata kiswahili ila nashangaa kwnn watu wanaferi kumbuka mchawi wetu ni mtaalawa elimu yetu
 
Back
Top Bottom