Somo la mathematics kuitwa ugonjwa wa taifa kwa wanafunzi

badshah

Member
Mar 16, 2013
51
32
SOMO LA MATHEMATICS KUITWA UGONJWA WA TAIFA KWA WANAFUNZI
Kwanini Somo Hili ni Gumu sana?

Kadri miaka inavyozidi kwenda ndio thamani ya madarasa inapungua, nikimaanisha kwa aliyemaliza kidato cha nne mwaka 1970 na aliyemaliza kidato cha nne 2012 wana tofauti kubwa sana kielimu kiasi ambacho yule aliyemaliza miaka 1970 una uwezo wa kumuajiri na akafanya kazi kwa ufanisi.

Elimu ya sasa imekuwa si kitu chochote labda ufike madarasa ya juu (university) ndio unaweza kujiona kweli ni msomi. Wanafunzi wa sasa wamekuwa wakiona tabu sana pale mwalimu aingiapo darasani, au pale wanapoachiwa kazi ya kufanya baada ya kipindi cha somo kuisha.

Kitu kingine kikubwa ni ule ubaguzi wa masomo, kweli unaruhusiwa kuchagua masomo unayotaka lakini kwa mpangilio na sheria maalum zilizowekwa, kwa mfano unapofika kidato cha tatu kuna michepuo ya sayansi, arts na biashara, na huwezi kuchagua nje ya hapo. Lakini utakuta wanafunzi huchagua masomo ya kusoma ndani ya huohuo mchepuo waliochagua.

Hebu angalia mfano mdogo tu, mchepuo wa sayansi una masomo 9, lakini utaona wanafunzi wanasoma masomo matano tu. Au mchepuo wa arts una masomo saba tu, lakini wanafunzi huchagua kusoma masomo manne tu, na hasa utaona masomo yanayoachwa ni yale ya muhimu na lazima kuyachukua.

Somo linaloachwa na kupingwa na wanafunzi wengi sana hapa, na ni somo lazima ni somo la Mathematics (Hisabati), tena limepewa jina kabisa na kuitwa Baba Mkwe au Ugonjwa wa taifa., huu umekuwa ni ugonjwa sasa wa karibuni nchi nzima.


Labda kwa ufupi hebu tuangalie ni nini hasa sababu inayofanya masomo haya kuchukiwa na wanafunzi na hasa somo la Mathematics, somo hili limeonekana kuwa gumu sana kiasi ambacho wanafunzi wengi hawahitaji kufahamu chochote juu ya somo hili na hata ukimpeleka katika masomo ya ziada (tuition) lakini bado mwanafunzi huyu ataendelea kupata alama za chini.

Kitu kibaya zaidi ni kwamba yule ambaye hajui humkatisha tamaa yule anayetaka kujua, na kumbuka kuwa, wadogo zetu hutuiga sisi tuliotangulia, ndio maana ile kauli ya ugonjwa wa taifa au baba mkwe juu ya somo hili ilianza kabla hata ya hawa wadogo zetu hawajaingia sekondari na hivyo wameikuta na kuiendeleza. Kauli hizi zenye kukatisha tamaa zitaharibu kwa kiwango kikubwa sana elimu yetu na hata kama kuna mtu anataka kujitahidi juu ya kusoma na kuelewa ataacha kabisa kwani ni asilimia kubwa sana wanakatisha tamaa, na kama inavyojulikana kuwa umoja ni nguvu. Lazima wadogo zetu watajiuliza kama hawa kaka zetu na dada zetu walishindwa sisi tutaweza? Na kibaya zaidi ni kwamba hawa huchukulia kuwa kila linaloshindikana ni gumu, kumbe ukweli sio hivyo bali ni hali ya kutawaliwa na uvivu pamoja na kukosa msingi mzuri wa somo hili na hata masomo mengine vilevile.

Kumbuka ulipokuwa chekechea ulifundishwa kuhesabu kama ni visoda, vijiti, mawe au vitu vingine. Hapa mwalimu wako alikuandaa na hesabu za mbele ambazo usingeweza kuzifanya endapo hujui kuhesabu. Wanafunzi wengi hawajiulizi kwanini mada fulani hutangulia kabla ya mada fulani? Au hawajiulizi kwanini masomo yamepangiliwa kwa mpangilio maalum? Kama lisingekuwa la muhimu suala hili, basi tungechukua vitabu vya darasa la tano tukaenda kufundishia darasa la tatu au vitabu vya kidato cha nne tukaenda kuwafundishia vijana wa kidato cha pili. Lakini haiwi hivyo kutokana na kwamba kila mada imepangwa ili kukuwezesha mwanafunzi kufahamu vyema mada ijayo na hili hasa nazungumzia katika somo la hisabati (Ugonjwa wa Taifa), huwezi kufanya hesabu ya kuzidisha kama hujui hesabu za kujumlisha. Na pia huwezi kufanya hesabu za kugawanya ikiwa hujui hesabu za kutoa, na ukitaka kuhakikisha hili jaribu kufanya maswali haya; 382 x 113 na 2865 ÷ 5 halafu uone je? Sijui kujumlisha na kutoa nitaweza kuyafanya?

Hivyo ndugu zangu tusidharau mada ndogo tukaona hazina maana kwani hatujui aliyeziweka amemaanisha nini. Sasa hebu fikiria endapo mwanafunzi amedharau hesabu za kutoa akakimbilia tu kujifunza hesabu za kugawanya hapo si ndio ugumu unapoanzia? Fikiri kwa kina sana ndugu yangu. Nakumbuka mwaka 2007 katika likizo ya katikati ya mwaka kulianzishwa mpango wa masomo ya jioni kwa wanafunzi, hivyo katika walioitwa kufundisha nilikuwa mmoja wao niliwahi kufundisha topic moja ambayo kwa sasa imefutwa, hii ilikuwa ni ya kidato cha tatu iliyoitwa Kinematics. Na kila aliyefundisha alihitajika kutunga mtihani wake mwenyewe ifikapo mwisho wa mpango huu karibia na kufungua shule, basi wakati nafundisha ingawa sikuwahesabu lakini nafikiri nilikuwa katika darasa hilo nafundisha wanafunzi wapatao 40 hivi, lakini mtihani wangu ulifanywa na wanafunzi kumi na mbili tu (12). Angalia matatizo sasa haya.

Katika kukaa muda mrefu sana na kufanya utafiti wa hapa na pale nimeona kuna tatizo dogo sana ambalo lilifanyika na limeleta madhara makubwa ndani ya somo hili la Mathematics kwa asilimia kubwa sana mpaka kufikia kuitwa ugonjwa wa taifa.

Katika mada za kidato cha kwanza, kuna mada ndogo mbili (sub topics) ambazo ni muhimu sana na ndio msingi wa somo hili. Mada hizi ni INTEGERS (application of integers)- Hasi na Chanya na mada ya pili ni BODMAS (MAGAZIJUTO) na zote hizi hupatikana katika mada kuu ya kwanza unapoingia kidato cha kwanza iitwayo NUMBERS. Unaweza kuona ni mambo ya utoto sana kuzungumzia juu ya mada hizi mbili nakuona ni vipi ziwe ni msingi wa somo hili lakini sasa hebu tuangalie ni vipi zinakuwa ni msingi wa somo hili?

Sote tumepitia huko na kusoma mada hizi lakini hatukuziweka akilini hata kidogo wala kujua kuwa zina umuhimu kwa kuziona ni ndogo na isitoshe hata shule ya msingi zinafundishwa. Ila huwezi kuamini hata mwanafunzi wa kidato cha nne wa leo ukimpa maswali yanayotokana na mada hizi mbili hawezi kufanya na kama yupo basi ni mmoja katika mia.

Fanya utafiti kwa wanafunzi kama 10 hivi wa kidato cha nne au hata cha tatu ambao unahisi wanapata shida katika somo hili, na shida hizi si kwasababu ya mada kubwa kama vile Trigonometry, Transformation, Logarithms, Vectors, Algebra, Circle, Linear Programming, Probability N.k. hapana! Ni kwasababu ya hizi hizi hesabu ndogo ingawa bado hawajatambua. Hebu wape maswali haya yafuatayo:
1. (-3) – (-4) = 2. (-2)+(-6)-8 = 3. 6+5-(-8) = 4. 4+(-4) =
5. (-60)+7(8-(-2))÷(-5) 6. (-13)+(+11)= 7. 11+(-2) = 8. (-2)-6+4-5
9. (-12)-(-12) = 10. 17+(-21)=

Ukishawapa angalia sasa majibu yao uone matatizo haya.

Hizi ni hesabu ndogo sana ambazo chimbuko lake ni darasa la sita (Primary) lakini ajabu mpaka leo mwanzafunzi wa kidato cha nne au cha tatu zinamshinda, na sio hao tu hata wa kidato cha pili na wenyewe wa kidato cha kwanza. Sasa hivi akitokea mtoto wa darasa la sita kumfuata dada au kaka yake wa kidato cha nne amfundishe hesabu hizi si matatizo hayo? Na je si itakuwa ni aibu? Jamani hebu tujitahidi sana kutatua tatizo dogo hili ili lisituharibie somo zima tukaliona gumu na kulichukia mpaka kufikia kuliita ugonjwa wa taifa au baba mkwe.

Kumbuka kuwa hesabu hizi haziishii tu hapa, na kama zingekuwa zinaishia hapa tu tunapofundishwa basi isingekuwa tatizo. Ila unafundishwa hizi kwaajili ya kujiandaa na hesabu za mbele na karibia hesabu zote zilizobaki huhitaji msaada wa mada ndogo hizi mbili. Hivyo basi, kama utaon akuwa hizi mada ni za kitoto na ukaona hazifai basi ujue umeutupa ufunguo wa somo hili.

Ningependa kuwaonyesha uhusiano wa mada hizi ndogo na mada zilizobaki lakini makala hii imekuwa ni ndefu sana hivyo nimeifupisha kwa kuandika makala nyingine inayohusiana na jinsi mada ndogo hizi mbili zinavyokuwa na uhusiano na mada nyingine zilizobaki. Nitaiweka makala hiyo hivi karibuni.

Ni matumaini yangu kuwa endapo nawe una tatizo kama hili basi ni muda wako sasa wa kujirekebisha na tatizo dogo hili ikiwa ni mwanafunzi, na kama ulishamaliza basi ni vema uwaelekeze wadogo zako walio mashuleni sasa.

Staryte - Elimu, Burudani na Maendeleo
 
Nini kifanyike kuokoa somo la hisabati kwa shule za sekondari?
Maana hali ya ufaulu kwa sasa siyo nzuri.
 
Madogo wakomae na twisheni sije wakageuka vilaza,suala la elimu ni la mtu binafsi,kama mtu akibweteka wengine wanakomaa na shule na wanatoka
 
Wanakuja toka msingi wakiwa hawana kabisa maarifa ya hesabu, yaani ni shida huko darasani kwa kweli walimu wanapata kazi sana
 
Huwa natamani kusema somo hili lifanywe kama chaguo kuanzia kidato cha kwanza ili kuondoa mrundikano wa wanafunzi wengi wasiopenda hesabu
 
Wanafunzi waandaliwe toka wakiwa primary. na wingi wa masomo upunguzwe kama vile history huwa yanakuwa marahsi na wanafunz wengi hupenda vilaini
 
NYUMBANI!!! Mabadiliko yaanzia nyumbani.

Baba yangu alikuwa akituambia, "Hesabu ni mchezo wa namba (Maths is just but a game of numbers)"

Tuliipenda hesabu kutokea nyumbani. Emphasis ya wazazi wetu kwenye hesabu ilikuwa sawa na ile ya kujua na kuongea Kiingereza na kupenda kusoma.

EVERYTHING BEGINS AT HOME...
 
Nadhani ili wanafunzi wafanye vizuri katika somo la hesabu kwanza waboreshewe mazingira ya kujifunzia bila kusahau kuboresha mazingira kwa walimu,vifaa,kupewa mazoez ya Mara kwa Mara ......
 
Jamii kwa ujumla ipambane na matatizo haya:
1. Mathematics Anxiety
2. How to Study Mathematics
Kuanzia umri mdogo watoto waelimishwe kutoogopa hesabu na namna sahii ya kusoma hili somo.
Tukiweza haya, hayo mengine Kama mazingira, motisha kwa walimu nakadhalika ndo vifuate. Vinginevyo hakuna kitu.
 
NYUMBANI!!! Mabadiliko yaanzia nyumbani.

Baba yangu alikuwa akituambia, "Hesabu ni mchezo wa namba (Maths is just but a game of numbers)"

Tuliipenda hesabu kutokea nyumbani. Emphasis ya wazazi wetu kwenye hesabu ilikuwa sawa na ile ya kujua na kuongea Kiingereza na kupenda kusoma.

EVERYTHING BEGINS AT HOME...

Kuna kichwa kimoja duniani huko kinaitwa Mwalimu Sifuel Malisa...akaja kumzaa mwanae Aiwinia S. Malisa na sasa kuna Mjukuu anaitwa Karamaeli Malisa aliyepata Masters yake ya Hesabu juzi juzi..Shikamoo hisabati!
 
Ili somo la hesabu wanafunzi wafanye vizuri waandaliwe kwanza wanafunzi wengi kwa kuwapa motisha kuwa atakayesoma na kufaulu vizuri hisabati asomeshwe bure ktk kuanzia kdto cha tano vyuo vya ualimu ili kuwapata walimu wa hesabu wengi halafu na walimu wa hayo masomo wapewe motisha.
 
serikali ifanye haya.
Zamani tukiwa shule tulifundishwa hisabati na walimu walokuwa wana uwezo na kuipenda hisabati,kwa sasa hali ni tofauti maana kila mwalimu wa shule ya msingi anafundisha hisabati.
bila utaratibu wa zamani kurudishwa hadi mwisho wa dunia hakuna chochote kitakacho fanyika.
 
Tatizo masomo mengi mno afu yote yana assaiment kesho Mwalimu anataka kazi ukusanye bado hujasoma kulingana n ratiba yko ulipanga....Em nambie Mwalimu mwenyew anafundisha huku anamawazo y kuongezewa mshahara...darasa linawanafunzi 90-100 n kitu(hapo ticha haezi kumfundisha moja moja kwakumuelekeza) yan changamoto n nying kuliko maelezo kwa kweli hesabu nlijitahd Sana nifanye vzur lkn ajuae n Mungu nlicho kipata
 
Jamii kwa ujumla ipambane na matatizo haya:
1. Mathematics Anxiety
2. How to Study Mathematics
Kuanzia umri mdogo watoto waelimishwe kutoogopa hesabu na namna sahii ya kusoma hili somo.
Tukiweza haya, hayo mengine Kama mazingira, motisha kwa walimu nakadhalika ndo vifuate. Vinginevyo hakuna kitu.
Hili ndilo neno. Ukiamini unaweza kuelewa Mathematics na kusimamia kwa vitendo unaloliamini, haitokuangusha. Hakuna muujiza pale ni kuelewa principles then mazoezi ya kutosha. Ukiogopa lazima ufeli.
 
Mwanafunzi akijiamini kwanza hata mwalimu asipokuwa mzuri sana kufaulu kutakuwepo. Zaidi ya asilimia 60 ni psychology ya mwanafunzi kwanza then mengine yanafuata. Usiogope.
 
Back
Top Bottom