Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,894
- 168,254
Siku moja nyani saba waliwekwa ndani ya bustani yenye uzio. Katikati ya bustani hiyo kulikuwa na jukwaa, na juu ya jukwaa hilo ziliwekwa ndizi mbivu za kuvutia sana.
Lakini pia kulikuwa na bomba la mvua la maji baridi sana kwenye bustabi ile. Ikawa kila nyani mmoja anapojaribu kupanda, basi mtunza bustani anafunglia lile bomba la maji baridi na kuwamwagia nyani wote. Nyani, kama ilivyo kwa binadamu hawezi kuvumilia maji ya baridi yanayokaribia kuwa barafu. Basi nyani wote wakawa wanaogopa kusogea karibu na ngazi ya kupanda kuelekea jukwaani.
Na yeyote aliyejaribu kusogea pale, wenzake walimshughulikia kwa makofi mazito.
Baada ya siku tatu nyani wote wakawa wameshazoea kula matunda mengine huku wakiogopa kufuata zile ndizi kwa kuhofia mvua ya maji ya baridi.
Mtunza bustani akaanza kutoa nyani mmoja na kumuweka mwingine. Yule nyani mpya alipoona ndizi juu ya jukwaa pale bustani akajaribu kusogea. Lakini kabla mtunza bustani hajamwaga maji yake ya baridi, nyani wengine walimvamia yule nyani mpya na kumshushia kipigo cha hatari. Walihofia mvua ya maji ya baridi. Yule nyani mpya akaghairi.
Kisha mtunza bustani akatoa nyani mwingine wa zamani na kumweka mwengine mpya. Huyu naye akajaribu kufuata zile ndizi, akaambulia kichapo. Na yule nyani mpya wa awali aliyepigwa alishiriki kikamilifu kumpiga huyu mpya mwengine.
Sasa hawa nyani wawili wapya wakawa wamejifunza utamaduni wa pale bustani kwamba ukijaribu tu kuzifuata zile ndizi unapewa kichapo na wenzako. Hawakujua kuhusu maji ya baridi. Wale wenyeji waliogopa kumwagiwa maji ya baridi ndio maana kila walipoona mmoja wao anasogea pale walimpa kichapo kabla hajafika ili wasimwagiwe maji. Lakini hawa wapya waligopa kichapo.
Baadae, nyani wa tatu alitolewa, akaletwa mpya mwingine. Na huyu alipojaribu tu kuelekea kwenye ngazi, alipewa kichapo. Na wale wawili wapya wa awali walishiriki vizuri kutoa kichapo kwa huyu mpya wa tatu.
Akabadilisha nyani wa nne hali ikajirudia vilevile. Wale wa zamani walitoa kichapo kwa kuhofia maji ya baridi, hawa wapya wakishirikia kutoa kichapo bila kujua sababu ya msingi bali tu kwa sababu walipigwa wakati walipokuwa wageni wakijaribu kufuata zile ndizi.
Hata nyani wote saba walipobadilishwa hali ilikuwa vilevile. Kila aliyejaribu kufuata zile ndizi aliambulia kipigo. Hawa nyani wote saba ni wapya na hakuna anayejua kuhusu maji ya baridi, walichojifunza wao ni kila anayesogea pale jukwaani anapewa kichapo bila kujua sababu ya msingi.
Mtunza bustani hakuwa na haja tena ya kupoteza maji yake! Nyani walishughulikiana wenyewe kwa wenyewe.
Hivyo ndivyo tunavyoishi! Kuna mambo mengi tunaogopa kuyafanya kwa sababu tusizozijua, wakati mwingine zile hatari tunazoambiwa zitatokea ikiwa tutafanya hivi au vile, hazipo tena. Wakati mwingine sababu hizo zimepitwa na wakati.