Somo kuhusu kujimiliki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Somo kuhusu kujimiliki

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Andrew Nyerere, Jun 26, 2010.

 1. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #1
  Jun 26, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Mwalimu alikuwa mfano mzuri wa kujimiliki nafsi kwa binadamu. Alipotukanwa,hakutukana,alipoteseka,hakuzungumza lugha ya vitisho dhidi ya waliomtesa,alipofanyiwa udhalimu na adui zake,yeye alijiweka tu kwenye hukumu ya haki ya Baba wa mbinguni.

  Katika moja ya mijadala ya jioni,Andrew alimuuliza Yesu;''Mwalimu,tunatakiwa kujinyima kama Yohana alivyotufundisha au tunatakiwa kuwania kuzimiliki nafsi zetu kufuatana na mafundisho yako? Mafundisho yako wewe yanatofautiana vipi na mafundisho ya Yohana?'' Yesu akajibu,''Yohana kweli aliwafundisha njia ya haki kufuatana na mwangaza na sheria za baba zake,na ile ilikuwa ni dini ya kujichunguza nafsi na kujinyima. Lakini mimi nakuja na habari mpya ya kujisahau nafsi na kujimiliki nafsi. Nawaonyesha njia ya maisha kama ilivyofunuliwa kwangu na Baba yangu wa mbinguni.

  ''Kweli nakuambia yeye anayeitawala nafsi yake ni wa maana kuliko yule anayeuteka mji. Kujimiliki nafsi ndio kipimo cha uadilifu alio nao mtu na kielelezo cha maendeleo yake ya kiroho. Katika mpango wa zamani mlifunga na kusali,kama viumbe wapya mliozaliwa upya katika roho,mnafundishwa kuamini na kufurahi. Katika ufalme wa Baba mnatakiwa kuwa viumbe wapya,vitu vya zamani vinapaswa kupita. Tazameni,nawaonyesha jinsi ambavyo vitu vyote vinaweza kufanywa viwe vipya. Na kwa upendo wenu baina yenu muifanye dunia iamini kwamba mmetoka kwenye utumwa na mpo katika uhuru,kutoka kwenye kifo na kuingia katika uzima wa milele.

  ''Kwa njia ya zamani mnatafuta kukandamiza,kutii na kuzifuata kanuni za kuishi;kwa njia mpya kwanza mnageuzwa naRoho wa Kweli na kwa njisi hiyo mnaimarishwa katika roho yenu ya ndani kwa akili yako kutengenezwa upya kiroho tena na tena,na kwa hiyo wapewa uwezo wa hakika na wa furaha ,ili ufanye utashi mzuri,unaokubalika na uliokamilika wa Baba. Usisahau-ni imani yako binafsi katika ahadi kubwa na za thamani za Baba ndizo zinahakikisha kwamba unashiriki katika maumbile ya kitakatifu. Kwa hiyo,kwa imani yako na kugeuzwa na roho mnakuwa kwa kweli mahekalu ya Mungu,,na roho yake kwa kweli inaishi ndani mwako. Kama,kwa hiyo,roho inaishi ndani mwako,ninyi sio tena watumwa wa mwili ila ni watoto huru,mliokombolewa kwa roho. Sheria mpya ya roho inakupa uhuru wa kujimiliki nafsi badala ya sheria ya zamani ya kuhofu kuwa mfungwa wa nafsi na mtumwa wa kujinyima.

  ''Mara nyingi,ulipofanya uovu,umefikiria kusingizia matendo yako yamefanywa kwa taathira ya uovu wakati kwa kweli unapotoshwa na tabia zako mwenyewe za maumbile. Hakusema Nabii Jeremiah zamani sana kwamba moyo wa binadamu ni wa udanganyifu kuliko vitu vyote na wakati mwingine hata umejaa uovu mkubwa? Tazama ilivyokuwa rahisi kujidanganya katika nafsi zenu na kwa ajili hiyo kuanguka katika uoga wa kijinga,ashiki za kila aina,starehe zinazowafanya muwe watumwa,uhasama,wivu,na hata chuki ya kutaka kulipiza kisasi!

  ''Wokovu ni kuhuishwa kwa roho na sio kwa vitendo vya haki vya nafsi yako vya mwili. Unaokoka kwa imani ambayo inaambatana na rehema,sio kwa woga wa kujinyima katika mwili,hata hivyo,watoto wa Baba ambao wamezaliwa kwa roho daima wanamiliki nafsi na yote yanayohusiana na hamu za mwili. Ukifahamu kwamba unaokolewa kwa imani,una imani ya kweli katika Mungu. Na wote wanaofuata katika hii amani ya mbinguni hatimaye watatakaswa ili watumikie milele kama watoto ambao wanaendelea kila wakati wa Mungu wa milele. Kuanzia hapo,inakuwa sio wajibu ila ni heshima kujitakasa na maovu yote ya akili na mwili wakati unatafuta ukamilifu katika upendo wa Mungu.

  ''Utoto wako unakuwa na msingi wa imani, na hautatikiswa na woga. Furaha yako inazaliwa katika kuliamini neno takatifu,na hutakuwa na shaka tena kuhusu upendo na huruma ya Baba. Ni uzuri wa Mungu ndio unawaongoza watu katika toba ya kweli. Siri yako ya kuimiliki nafsi inaambatana na imani yako katika roho anayeishi ndani,ambaye anafanya kazi kwa upendo. Hata hii imani inayookoa hunayo kwa uwezo wako:hiyo pia ni zawadi ya Mungu. Na kama ninyi ni watoto wa imani iliyo hai,ninyi,sio tena watumwa wa nafsi ila ni watu ambao ni washindi mnazimiliki nafsi zenu,watoto wa Mungu ambao mmekombolewa.

  ''Kama,kwa hiyo,watoto wangu,mmezaliwa katika roho,mtakuwa huru milele kutokana na utumwa wa nafsi katika maisha ya kujinyima na kujichunga kuhusu hamu za mwili,na mnaingia katika ufalme wa furaha ya kiroho,ambapo mnaonyesha matunda ya roho katika maisha yenu ya kila siku:na matunda ya kirohi ndio msingi wa furaha ya juu na kitu ambacho kitakuwezesha uimiliki nafsi,hata vilele vya juu kabisa vya mafanikio ya binadamu-kuimiliki nafsi kwa kweli.''
   
Loading...