Somo juu ya ku-balance Biological cycle katika bwawa la Samaki

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,944
18,653
Leo ningependa nitoe somo juu ya Kubalance Biological cycle katika bwawa la samaki. Hapa ni katika aina yoyote ya bwawa la samaki.

Wafugaji wengi wamekuwa wakifuga na bila kujua au kuelewa jinsi na umuhimu wa kuwa na BC katika bwawa la samaki.

BC ni mfululizo wa mabadiliko ambayo viumbe ( organism) hupitia na kurudi katika hali yake ya mara ya kwanza.

Balanced BC ni muhimu sana katika ukuaji na afya ya samaki.
Hata hivyo, Kubalance BC imekuwa changamoto sana katika ufugaji hasa katika mabwawa ya liner, PVC, tanks na ya kujengea. Aina hii ya mabwawa imekuwa ikikatisha au kuzuia Mzunguko wa kibiologia katika mabwawa.

Inafahamika kuwa, katika bwawa la samaki, hujitengeneza sumu mbalimbali ambazo ni hatarishi kwa viumbe vya majini hasa samaki. Hizi sumu hutokana na kinyesi au mabaki ya vyakula vya samaki ambavyo huoza na kuanza kutoa ammonia. Particles/ gas ya ammonia husambaa taratibu kwenye maji na mara nyingi hufanya maji kutoa harufu mbaya kama hakuna biological cycle. Hii humgharimu mfugaji kubadilisha maji mara kwa mara. Na endapo mfugaji atachelewa kubadilisha maji kwa wakati, samaki huweza kupata magonjwa kama fungus, crack head na wakati mwingine kupoteza hamu ya kula, kudumaa au kufa.

Hapa ndipo unakuja umuhimu wa kuwa na balanced BC katika bwawa la samaki. BC huweza saidia kichuja au kuondoa hizi sumu kwa wakati hata bila kubadilisha maji.

Biological cycle huondoa kiasi cha ammonia ambacho hakitakiwi kwa kutumia "Nature's Nitrogen cycle" ambayo inaondoa sumu ( detoxify) kwenye taka zilizo hai ( organic waste).

Hii process huwa hivi: kiasi cha ammonia kinapoongezeka kwenye bwawa, koloni la vijidudu vidogo sana ( macro bacteria) ambavyo humengenya ammonia, hujitokeza au kukuwa. Hizi bacteria humengenya(breakdown) ammonia na kuwa "Nitrites". Hii nitrites nayo ni sumu hatarishi kwa samaki endapo itazidi kiwango kinachohitajika kwenye maji.

Nitrites nayo ikizidi ongezeka, koloni jipya la bacteria hukuwa na kuimengenya kuwa Nitrates.

Nitrates haina madhara makubwa kwa samaki sababu sio sumu bali huwa kama mbolea aina ya Nitrogen inyofanya maji yawe kijani kutokana na ukuaji wa algaes na huwa chakula mbadala cha samaki.

Hivyo basi, ili kubalace BC katika bwawa la samaki ni muhimu kuhakikisha bwawa linaweza kuzalisha bacteria wa faida wa kutosha ili kutengeneza makoloni yatakayomengenya sumu zinazotokana na kinyesi au mabaki ya chakula cha samaki.

Mbinu ya kuhakikisha bwawa lina bacteria wa faida. ( beneficial bacteria).

Earthen ponds ni rahisi kupata bacteria wakutosha sababu BC haijakatishwa kulinganisha na mabwawa ya liner, PVC, Tanks na Concrete.

Mkulima unashauriwa kuweka udongo katika mabwawa yasiyokuwa na udongo kwa ndani. Unaweza kuzamisha viroba vya udongo au mbolea iliyooza sana ( mwaka 1 na kuendelea) katika bwawa.

Udongo ndyo Natural material inayowapa makazi bacteria ( natural habitat) mbalimbali wanaosaidia katika biological cycle. Ndyo maana Mabwawa yaliyochimbwa tu ( earthen ponds) hukuza samaki kwa haraka na gharama ndogo za kubadilisha maji sababu ardhi inakuwa inabacteria wa kutosha.

kwa sababu hii Cycle hutengeneza kiasi kikubwa cha Nitrates inayokuza algaes kwa kasi na kufanya maji kuwa kijani sana, mfugaji anashauriwa pia kupandikiza mimea maji au magugu maji katika mabwawa ambayo yatatumia Nitrates kwa kasi na ni rahisi mfugaji kuyapunguza katika bwawa. Aina ya magugu yanayoshauriwa sana ni "water lettuce". Hii huwa na mizizi mirefu inayoliwa na samaki, rahisi kuyapunguza, hayatumii disolved oxygen( oxygen ya kwenye maji) , pia mizizi yake huweza kuchuja maji na kuyafanya yawe clear.

Water lettuce huweza tumika kulisha mifugo kama ngombe na ngurue. Pia wakulima wengine huweza kuiozesha na kutengeneza mbolea ya mboji.

Mafunzo mengi kama haya yanapatikana katika group la UFUGAJI SAMAKI KIBIASHARA
UFUGAJI SAMAKI KIBIASHARA

Maelezo zaid 0759741303.
View attachment 992466

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulichozungumzia icho kinatokea kwenye RAS ambapo maji yanayotumika kufuga samaki yanakuwa yanazunguka hayohayo muda wote kwaio inashauriwa kuwa na Biofilter ambao watajiatach somewhere ili waweze kukonsume Ammonia pia kwenye RAS inashauriwa kuwa na Fish tank fulfilled with water, plant tank, biofilter, water pump, kuwe na Sand/gravel kwa ajiri ya kusafisha maji kabla ya kurudi kwenye tank la samaki ili wasiweze kupata madhara ya Ammonia wanayodhalizisha wenyewe kupitia mkojo wao wanaokojoa hayo ni machache kuhusiana na RAS.
NB; mtaongezea mengine kama nimesahau kwenye mada inayohusiana na kufuga samaki kwenye RAS!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulichozungumzia icho kinatokea kwenye RAS ambapo maji yanayotumika kufuga samaki yanakuwa yanazunguka hayohayo muda wote kwaio inashauriwa kuwa na Biofilter ambao watajiatach somewhere ili waweze kukonsume Ammonia pia kwenye RAS inashauriwa kuwa na Fish tank fulfilled with water, plant tank, biofilter, water pump, kuwe na Sand/gravel kwa ajiri ya kusafisha maji kabla ya kurudi kwenye tank la samaki ili wasiweze kupata madhara ya Ammonia wanayodhalizisha wenyewe kupitia mkojo wao wanaokojoa hayo ni machache kuhusiana na RAS.
NB; mtaongezea mengine kama nimesahau kwenye mada inayohusiana na kufuga samaki kwenye RAS!



Sent using Jamii Forums mobile app
RAS ni Mechanical method ya kufilter maji, hapa nazungumzia Natural method ya kufilter maji. Sio kila mfugaji ataweza kufunga RAS katika mabwawa yake ukizingatia gharama zake.

Hapa ni kitu kinachotokea hata kwenye natural habitats za samaki ambako hakuna cha RAS lakini samaki wanasurvive, na kukuwa kwa wing.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hii siyo Aquaponics system?
Yah ni kma ivyo ila hatujainvolve upandaji wa mimea au mbogamboga zinazoliwa. Badala ya kutumia Water lettuce mfugaji anaweza kupanda mimea juu ya bwawa na ikasaidia kutumia iyo nitrogen itokanayo na kinyesi cha samaki

Kama ivyo.
Screenshot_20190118-031134_Google.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom