Sometimes in April

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
18,849
67,285
Miaka 22 sasa toka mauaji ya kimbari ya Rwanda
CfYeaYIUIAAVFAD.jpg
CV4WjLZWoAAS5vw.jpg
 
Hii ni bora kuliko zile nyingine zote huyo ni Idris Elba the next bond sema wazungu wamembania kisa ni black
 
Hii ni moja ya movie ambayo sitakaa niisahau...

Wacha tu! kuna yule mdogo wake (ki movie) anaitwa "Gregwaa" (Gregory in English). nilikesha siku moja huko Kyela, nikiangalia collection ya Rwanda genocide movies! Hii iliniliza kwa kweli, na kwa mimi nakumbuka fika huo mwezi April 1994 for some personal tragic moment! kweli ni "Sometimes in April"

Specifically siku taarifa za kutunguliwa ndege ya Habyerimana, nilikuwa nasafiri Kondoa - Arusha, na kimvua fulani hivi kinanyesha, kila nikiangalia hii movie, memories of that April becomes very fresh!
 
huyo jamaa Idris Elba kazi anaiweza kila akicheza muvi anaitendea haki
 
Sometimes in April....the best Movie ever........ nilikua na Boss wangu alinieleza aiseee dah, yeye ndio baadhi ya watu ambao walienda kuokoa watu kwenye madimbwi ya damu.
 
Poa ngoja niitafute, alicheza vizuri sana kwenye Pacific Rim.

Uingalie pamoja na ile "Hotel Rwanda" na "Shooting the Dogs (Beyond the Gates" halafu pia usome kitabu cha Kamanda wa vikosi vya UN vilivyokuwa Rwanda (UNAMIR) Luteni Genarali Romeo Dellaire "SHAKE HANDS WITH THE DEVIL" (Failure of humanity in Rwanda)

Mimi tangu niliposoma kitabu (personal accounts) na kuangalia hizo movie, nimejikuta naichukia UN kwa ujumla! Lut Gen Romeo anaeleza ambavyo alitelekezwa na UN ndani ya Rwanda, na ambavyo mtazamo wa UN ulivyokuwa, at the time Rwanda walikufa malaki ya watu the same time kulikuwa na mauaji kule Chechinia na ukiangalia resources zilizopelekwa huko vs namba ya watu waliokuwa at risk is very unresoanable,

Pia Lut Gen Romeo anaeleza wizi uliokuwepo Bandari ya Dar es salaam na ambavyo uliathiri utendeji kazi wake, anasema kuna magari "Cruiser" kama 2 hivi ziliyeyuka kati ya Dar na Kigali, achilia mbali accessories zilizonyofolewa kwa zile zilizoweza kufika Rwanda!

Na anamkubali sana Paul Kagame kama askari na kiongozi, nakubaliana nae sana kwamba ni Askari mwenye nidhamu (disciplined) ukiangalia uongozi wake kwa RPF (then) na Nchi (sasa) utakubaliana na Lt Gen Romeo

Kitabu kinapatikana soft copy via Kindle @ Amazon km $ 10 tu
 
In sometimes in April wabelgiji wanaonekana wanawapima wanyarwanda pua kwa kutumia vernia calliper at the beginning of the movie sijui kama hii ilikuwa na ukweli iliongezwa tuu
 
Back
Top Bottom