Free ideas is only because you are not free thats why you are hanging,you are blinded and GOD is not tested,you are not wise thats why you cant know your creator,you gave satan your thoughts and hes using them accordingly but very ignorant,
WHO IS GOD?
if you dont even know GOD what proof do you want???
Imethibitika kwamba mpaka sasa hakuna aliyeweza kuthibitisha hapa kwamba mungu yupo.Swala hili mbona ni rahisi na kwa nyie mnao amini kayika mungu mngeshalijibu.?.Kukwepa kujibu na kutukana wasioamini ni dalili tosha kwamb hamjui kwa nini mnaamini ispokuw ani utamaduni mlioukuta na mkaamua kuufuata bila kushughulisha akili zenu.
Binafsi sina tatizo na mungu wenu(kama yupo),lakini kushindwa kwenu kukithibitisha kwa ushahidi kile mnachokifuata na kukitolea sifa za pekee ni dalili ya kwamba mnakiumba wenyewe akilini mwenu na sio kwamba kwel kipo.Wewe unaeamini mungu yupo kwa sababu tu umeamua ama kwa kuwa kuna baadhi ya vitu unadhani haviwezekani bila ya mungu ama nguvu flani huo ni uoga na uzembe wa kufikiri.Narudia tena,"Dini ni ugonjwa mbaya kuliko magojwa makuu yale yasiyo na tiba.Dini ni umasikini,dini ni ufukara,dini ni uoga ,dini ni wasiwasi wa mwanadam katika kuyaendesha maisha yake mwenyewe!.
Kuna watu mamilioni wanakwenda kanisani na misikitini lakini hawajui wanafuata nini,labda kwa sababu ni ijumaa na jumapili na wako off!.Lakini pia swala la kujiuliza ni kwamba dini imekusaidia nini mpak sasa?.Hata yule aliye maskini sana anamwomba mungu huyu huyu ambaye matajiri wanamwomba.,Dini ni kujifariji kusiko na tija.Ukitaka kuwa na mawazo mgando na kukosa ufumbuzi binafsi wa matatizo yako basi base katika dini.,Dini zinafumba macho,dini inapumbaza,dini haikupi solution ya matatizo yako ispokuwa ina kujengea tena tatizo na kukupotezea muda w akusolve matatizo.
Kabla sijamaliza kuandika hii sentensi kuna watoto sabini wamefatiki duniani wakiwa vitandani na mama zao wakimwomba mungu awaponye.Inawezekana mungu hakupenda kuwaponya ama ameamua kuacha wafe ama hana muda ama basi hana uwezo huo.
Mungu aliyeamua kwa mapenzi yake kumuumba malaika aliyekuja kuwa shetani(ndivyo msemavyo),Mungu aliyejua kabisa ninik itatokea lakini bado kaweka hukumu kwa viumbe wake.
Nachukia sana mtu anaposema kitu flani hakiwezekani ama ni cha ajabu so lazima mungu amefanya ama amehusika.Mawazo ya hivi huwa hayajengi ispokuwa yanabomoa maana hayajibu swali hata wapi alipotoka mungu.Ikiwa mungu ni personal figure huwezi sema kwamba ilitokea tu.Na ikiwa hamkubaliani na sisi(mimi) kwamba dunia inaweza kuwa imetokea pasipo kuumbwa iweje mkubali kwamba mungu ametikea tu ??.Mimi (sisi)naweza kueleza kila step ambapo dunia imepita mpaka kufika hapa tulipo,lakini swali la mungu katoka wapi kwenu ni kufuru na mtu akiuliza anaonekana mwehu.
Kuna siku niliwauliza je ,imekuwaje mungu akaacha ghafla kuwasiliana na watu wake kupitia mitume na manabii?.Enzi za upumbavu zimepita.Akurupuke mtu sasa aseme mungu kamtokea kamwambia blah blah kwanza hakuna atakaye mwamini pili atachekwa kisha anapimwa akili,mnajua kwa nini??.
Miaka ya nyuma tz alikuepo babu aliyesema anatibu ukimwi kwa tsh.500,tangu siku ya kwanza kupata habar hiyo mi nilipinga na kusema kwamba huu ni usanii tu na kwa sababu watu hawajui hata mungu ni nini basi atapata watu.Hakika alipata na cha ajabu hakuna aliyethibitisha kwamba kapona.Kwa sasa hakuna anayeenda kwake tena watu wamejua ni uongo.Hakina nawaambia ipo siku pia watu watajua dini na uwepo wa nguvu kuu (mungu) ni uongo.