Tofauti kubwa ya Nyerere na viongozi wa leo ni kwamba Nyerere alikuwa "visionary leader", kwamba aliweza kufanya uamuzi si tu kwa kuangalia maslahi ya taifa ya leo bali pia ya baadaye sana. Japo mara nyingine mambo hayakufanikiwa lakini siku zote alichofanya kilikuwa na mantiki sana. Alitaka Tanzania ije kuwa na "industry based economy" kwa kuwa na viwanda vya msingi na hivyo kujenga uwezo wa kuwa net exporter.
Leo viongozi wanashindwa hata kufanya uamuzi kwa vision ya mwaka mmoja tu - wanauza nyumba za serikali bila kuangalia mawaziri wajao watakaa wapi; wanasign mikataba ya kuzalisha umeme bila kuangalia deni litalipwaje; wanakopa hela bila kuangalia uwezo wa ku-service hilo deni, wanakodisha ndege bila kuangalia lini inatakiwa ifanyiwe maintanance kubwa, nk.
Yaani tuna typical viongozi wenye philosophy ya "mlaji ni mla leo, mla kesho atajiju".