SOMBETINI SPECIAL THREAD: Kampeni zote za CHADEMA hapa!

SOMBETINI SPECIAL THREAD: Kampeni zote za CHADEMA hapa!

Deo MUNISHI: wabeba madawa wakuu nchi hii ni wanawake
 
Deo Munishi: Rais awataje wauza madawa ya kulevya kwani ana list yote. Kipaumbele cha taifa ni elimu lakini mara zote wanawafelisha wanafunzi.
 
Anaongea sasa mwenyekiti wa BAVICHA JOHN HECHE: CHADEMA haitegemei umaarufu wa mtu mmoja tena!
 
John Heche: Serikali inawafahamu majangili kwani sio rahisi upakie mzigo wa meno ya tembo na pembe zake then ipite JNIA yasionekane while hata sindano ikipitishwa inaonekana. Bado yote pia yanapitishwa bandarini na kupakiwa kwenye meli za KINANA.
 
CHADEMA haitakubali kushiriki uchaguzi wa katiba mpya bila kuandikisha wapiga kura wapya. Pia chadema ina mpango wa kuongea na wananchi Tanzania nzima kwa kutumia helikopta kumi. Mwisho anamuombea kura ndugu Ally Bananga kuwa diwani wa SOMBETINI.
 
Lete updates zaidi Arushaone, tumetega antenna tunakufuatilia.
 
Last edited by a moderator:
Sasa anaingia Tundu Lissu.

Wakati mnapigwa bomu SOWETO mwaka jana, mimi na ALLY BANANGA tulikuwa ISEKE kwenye kampeni ambako baada ya uchaguzi ule, CHADEMA ilishinda pale ISEKE SINGIDA. Nawaombeni mumpe kura za udiwani bwana Bananga.
 
Arusha mmekuwa wahanga wa mateso ya serikali hii ya CCM kwa kupigwa mabomu ya machozi, na mabomu ya kuua bila kusahau risasi, mkiendelea kupigia chama cha mapinduzi ni kujidhalilisha. Pigeni kura kwa Ally Bananga.
 
System ya nchi ni mbovu kwani akipewa leseni mchimba mafuta au wenye migodi serikali inampa haki ya kumiliki eneo husika na pesa zipatikanazo ni zake... mfano MACHIMBO YA MADINI, VITALU VYA UWINDAJI, PIA MACHIMBO YA GESI.
 
Serikali inaelekea kuanguka kwani haijawahi kutokea kwenye serikali zingine zilizopia kurusha mabomu ya kuua, kugeuzia raia wake bunduki kuua waandishi wa habari, kutesa kiongozi wa madaktari kuunda operation tokomeza ikitesa raia wake, CCM imekufa
 
Serikali ya TANZANIA ina muundo mbovu kwani kuna amiri jeshi wawili, mmoja wa magogoni na mwingine yuko Mnazi mmoja ZANZIBAR kila mmoja ana jeshi lake. Kitatokea nini wakipishana kauli?

Lazima tukubali serikali tatu kama tume ya Warioba ilivyosema!
 
Maskini Cuf hapa sombetini
Kwani kuna mtu ana mda nao basi!!!!
 

Attachments

  • 1390659826365.jpg
    1390659826365.jpg
    65.1 KB · Views: 104
  • 1390659843641.jpg
    1390659843641.jpg
    62.1 KB · Views: 101
Back
Top Bottom