Somalia yaomba kujiunga na Afrika Mashariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Somalia yaomba kujiunga na Afrika Mashariki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ileje, Mar 7, 2012.

 1. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,659
  Trophy Points: 280
  Somalia ambayo imekua ikijaribu kujikwamua toka vita vya miaka 20 imetuma maombi yakutaka kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  Kenya ambayo ndio mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya hiyo imethibitisha kupokea maombi ya Somalia.

  Somalia inakuwa nchi ya tatu baada ya Sudan Kusini na Sudan Khartoum kutuma maombi ya kutaka kujiunga na Jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki.Taarifa kutoka serikali ya mpito ya Somalia inasema kuwa wameamua kujiunga na jumuiya hiyo kutokana na hali ya kiusalama nchini Somalia kuimarika na utulivu kuanza kushuhudiwa.

  Hata hivyo azma ya Sudan kutaka kujiunga na jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki imekataliwa.
  Kwa sasa jumuiya ya Afrika Mashariki inajumuisha nchi tano, Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi.
  Mbali na nchi wanachama kuwa na ruhusa ya kufanya biashara bila vikwazo vyovote kwa wakati huu zinapanga kuwa na sarafu moja kufikia mwaka mwezi Juni mwaka huu wa 2012

  Source: bbc

  Je Somalia inaweza kuwa mshirika wa kuaminika? TUJADILI...
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hii iko jukwaa la kimataifa
   
Loading...