Bwiree
Senior Member
- Nov 12, 2016
- 164
- 103
Mithali 28:1-28
[1]Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu;
Bali wenye haki ni wajasiri kama simba.
[2]Kwa sababu ya maasi ya nchi wakuu wake huwa wengi;
Bali kwa wenye ufahamu na maarifa hali ya nchi hudumishwa
[3]Mtu mhitaji awaoneaye maskini,
Ni kama mvua ya dhoruba isiyosaza chakula.
[4]Wao waiachao sheria huwasifu waovu;
Bali wao waishikao hushindana nao.
[5]Watu wabaya hawaelewi na hukumu;
Bali wamtafutao BWANA huelewa na yote.
[6]Afadhali maskini aendaye katika unyofu wake,
Kuliko mpotofu wa njia angawa ni tajiri.
[7]Yeye aishikaye sheria ni mwana mwenye hekima;
Bali aliye rafiki wa walafi humwaibisha babaye.
[8]Yeye azidishaye mali yake kwa riba na faida,
Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini.
[9]Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria,
Hata sala yake ni chukizo.
[10]Kila mtu awapotezaye wenye haki katika njia mbaya,
Ataanguka katika rima lake mwenyewe;
Bali wakamilifu watarithi mema.
[11]Mtu tajiri ana hekima machoni pake mwenyewe;
Bali maskini mwenye ufahamu humchunguza sana.
[12]Wenye haki washindapo, uko utukufu mwingi;
Bali waovu waondokapo, watu hujificha.
[13]Afichaye dhambi zake hatafanikiwa;
Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.
[14]Mwanadamu mwenye kicho yu heri sikuzote;
Bali mshupavu wa moyo ataangukia madhara.
[15]Kama simba angurumaye, na dubu mwenye njaa;
Ndivyo alivyo mtu mbaya awatawalaye maskini.
[16]Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu sana;
Bali achukiaye kutamani ataongeza siku zake.
[17]Aliyelemewa na damu ya mtu
Atalikimbilia shimo; wala mtu asimzuie.
[18]Aendaye kwa unyofu ataokolewa;
Bali mkaidi wa njia zake ataanguka mara.
[19]Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele;
Bali afuataye mambo ya upuzi atapata umaskini wa kumtosha.
[20]Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele;
Lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa.
[21]Kupendelea watu si kwema;
Wala mtu kuasi kwa ajili ya kipande cha mkate.
[22]Mwenye husuda afanya haraka kuwa tajiri;
Wala haufikiri uhitaji utakaomjilia.
[23]Amkemeaye mwenzake hatimaye atapata kibali;
Zaidi ya mtu ajipendekezaye kwa ulimi wake.
[24]Aibaye mali ya babaye au mamaye, na kusema, Si kosa;
Mwana huyo ni rafiki wa mtu mharibifu.
[25]Mwenye nafsi ya kutamani huchochea fitina;
Bali amtumainiye BWANA atawandishwa.
[26]Mwenye kujitumainia moyo wake ni mjinga;
Bali yeye aendaye kwa busara ataokolewa.
[27]Mwenye kuwagawia maskini hatahitaji kitu;
Bali afichaye macho yake atakuwa na laana nyingi.
[28]Wasio haki wainukapo, wanadamu hujificha;
Bali waangamiapo, wenye haki huongezeka.