Soma upuuzi wa sekta ya madini... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Soma upuuzi wa sekta ya madini...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MWANAWAVITTO, Jun 24, 2012.

 1. MWANAWAVITTO

  MWANAWAVITTO Senior Member

  #1
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Soma kisha tupia neno 6http://www.tanzania.go.tz/madini.html
   
 2. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #2
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,137
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  www.tanzania.go.tz/madini.html
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Haifunguki mazee. Tubandikie basi
   
 4. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #4
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,137
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Hakuendeki aiseeeeeee au ulimaanisha neno hili hili tu
   
 5. J

  John W. Mlacha Verified User

  #5
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  i copy na ku i paste hapa
   
 6. MWANAWAVITTO

  MWANAWAVITTO Senior Member

  #6
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  nalishughulikia mkuu
   
 7. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Majaliwa ya rasilimali ya madini
  Almasi
  Dhahabu
  Metali za besi na kundi la platinamu
  Metali za chuma
  Bati
  Vito
  Kaboneti
  Makaa ya mawe
  Madini ya viwanda
  Sera ya sekta ya madini
  Marekebisho ya sekta ya madini
  Vyama vya wataalamu


  Sekta ya madini inachangia takribani asilimia 2.3 ya pato la Taifa, ambayo inakadiriwa kufikia asilimai 10 ifikapo 2025. kama ilivyo kwenye dira ya maendeleo 2025. madini ni sehemu muhimu inayoongoza katika pato la kigeni kati ya mauzo yasiyo asilia. Aidha ina uwezo mkubwa wa ajira na inayongoza katika kuupa nguvu uchumi wa Tanzania.
  Rasilimali ya madini

  Tanzania ina madini mengi, na hasa dhahabu, metali za besi, almasi, madini ya chuma na aina kadhaa za vito, vingi vikiwa vya aina ya pekee kama tanzanaiti. Mengine ni makaa ya mawe, urani na madini ya viwandani kama magadi, kauri, jasi, fosfati na mawe mbalimbali yanapatikana kwa bei nzuri. Yafuatayo ni madini yanayovutia wengi:

  § Dhahabu hupatikana katika ukanda wa mawe kijani uliopo mashariki na kusini mwa Ziwa Victoria, na mfumo wa miamba iliyopo kusini na kusini magharibi mwa Tanzania.

  § Metali za bezi zinapatikana ukanda unaoanzia Kagera kupitia Kigoma hadi Mikoa ya Mbeya, Rukwa na Mtwara.

  § Vito vinavyopatikana ukanda wa mashariki na magharibi kutoka mpakani mwa Kenya, kaskazini mwa Msumbiji, na Mikoa ya Mbeya na Rukwa.

  § Dhahabu na almasi ndiyo madini makuu nchini.
  Almasi
  Tanzania ni mzalishaji mkubwa wa almasi kwa miongo kadhaa kutoka machimbo ya Williamson, Mwadui ambako uchimbaji wa kibiashara ulianza 1925. Miamba 300 ya kimbalaiti ipo Tanzania na asilimia 20 yake ina sifa za kuwa na almasi.
  Dhahabu

  Dhahabu ni eneo zuri sana la kuwekeza. Wasaa wa sasa upo kwenye machimbo ya zamani katika mfumo wa miamba ya ukanda wa Archaean Greenstone kando kando ya ziwa Victoria, na miamba michanga ya proterozoki. Uchimbaji wa dhahabu umeongezeka kwa kasi miaka ya 90 kwa kutumia teknolojia ya kisasa na mbinu mpya.

  Mashapo makubwa ya dhahabu yamegundulika eneo la Ziwa Victoria na yapo katika hatua mbalimbali za uchimbwaji. Dhahabu pia imegunduliwa kusini magharibi mwa Tanzania.

  Metali za Bezi na Kundi la Platinamu

  Kijiolojia, miamba ya Archaean na Proterozoki ina uwezekanao wa kuwa na metali za bezi na kundi la platinamu. Ugunduzi wa hivi karibuni kaskazini magharibi mwa Tanzania umeonesha kuwepo kwa hazina kubwa ya madini ya nikeli, kobati na shaba iendanayo na mfumo wa miamba ya Karagwe-Ankole.

  Zaidi ya hapo, kundi la metali za kroniumu na platinamu limeonekana. Hazina kubwa ya nikeli iliyo na ngegu pamoja na kobati imebainika. Kuna akiba ya shaba, fedha na urani mkoani Shinyanga.
  Metali za chuma

  Mawe yenye madini ya chuma yametambulika kwenye miamba ya proterozoki huko Liganga kusini magharibi mwa Tanzania karibu na makaa ya mawe ya Ketewaka-Mchuchuma. Madini ya titani yanapatikana kwenye mchanga wa pwani ya bahari pia.
  Bati na madini ya kutengeneza chuma cha pua

  Bati na madini ya kutengeneza chuma cha pua na filameni za taa za umeme yanapatikana Karagwe kaskazini magharibi mwa Tanzania.

  Vito

  Tanzania imejaliwa aina nyingi za vito ikiwemo Tanzanaiti inayopatikana kwenye mfumo wa miamba ya Usagara na Ubendi. Tanzanaiti inachimbwa Mererani.

  Vito vingine vinavyochimbwa nchini ni rubi, rodolaiti, johari ya rangi ya samawati, zumaridi, ametisti, krisoprase, peridoti na tormalini. Hivi karibuni ugunduzi ulifanywa Mkoani Ruvuma, Mtwara na Lindi wa krisoberi, spineli, zumaridi, ganeti, zikoni na almasi.

  Mauzo nje ya vito yalikaribia US $ 10 millioni mwaka 1996, na vingi vikiwa ghafi. Kuna nafasi kubwa ya kuwekeza katika usanifu na unakishaji wa tasnia ya vito.

  Kaboneti
  Zaidi ya kaboneti 20 zinazohusiana na volkano zimebainishwa nchini, na ambazo zimekuwa chanzo cha elementi adimu kama nibimu na fasfati.

  Makaa ya mawe
  Hazina ya makaa ya mawe iliyo na ubora sawa na ile ya Gondwana Afrika ya Kusini, inapatikana Ruhuhu na Songwe-Kiwira Kusini-Magharibi mwa Tanzania. Jumla ya tani za akiba 1.5 billioni zimegunduliwa. Machimbo pekee ya mkaa wa mawe yapo Kiwira, yenye kuzalisha tani 35,000 kwa mwaka, na yote yakitumiwa hapa nchini kwa kuzalisha umeme.

  Madini ya viwandani

  Chokaa ya mawe yenye usafi mkubwa inapatikana kama marumaru nyeupe Mkoani Morogoro.

  Udongo wa mfinyanzi aina mbalimbali kama bentonaiti, kauri na mfinyanzi wa kutakasia vitambaa unapatikana kwa vingi, na umetumiwa kidogo sana. Amana kubwa ya kauri iiliyopo Pugu, kilomita 30 magharibi mwa Dar es Salaam, ina nafasi kubwa ya kuendelezwa.

  Chumvi na madini mengine yanayoyeyuka yenye umuhimu kiuchumi inahusiana na maziwa ya bonde la ufa. Uchunguzi wa magadi Ziwa Natron umeonyesha kuna uwezekano wa kupata zaidi ya tani milioni moja kwa mwaka. Uzalishaji wa chumvi hivi sasa ni tani 105,000 kwa mwaka.

  Grafati ya gredi ya juu inapatikana kwenye mfumo wa mwamba wa Usagara. Akiba ya kutosha imebainishwa Mererani, Tanzania kaskazini, yenye kuweza kuchimbwa kwa miaka 40 kwa kiasi cha tani 15,000 kwa mwaka, na iliyo na usafi wa 97-98%. Machimbo hayo hutoa pia tanzanaiti ambayo hupatikana kwa pamoja na grafati.

  Fosfati inachimbuliwa Minjingu Mkoani Arusha, na takribani tani 48,000 kwa mwaka hutumiwa katika uzalishaji wa mbolea. Kutokana na kufungwa kiwanda cha mbolea cha Tanga, matumizi ya sasa ni ya moja kwa moja mashambani.

  Sera ya Sekta ya Madini

  Sera ya Madini Tanzania ya mwaka 1997 inasisitiza juu ya sekta binafsi kuendeleza madini, na wakati huo huo Serikali ikiwa na jukumu la kuidhibiti, kuikuza na kuiwezehsa kuendelea. Jukumu la umma, pamoja na mengine ni:

  ¨ Utungaji wa sera itakayojumuisha mfumo mzima wa Sera za Serikali

  ¨ Kushauri juu ya sheria, taratibu na masuala ya fedha yahusyo sekta.

  ¨ Kukusanya mapato kutoka mirabaha, pango la mwaka, haki za uchimbaji na leseni.

  ¨ Kufuatilia shughuli za uchimbaji madini .

  ¨ Kukusanya na kuweka takwimu za kiufundi za kijiolojia, kwa madhumuni ya kujitangaza, na kutoa huduma za ugavi kwa wachimbaji wadogo

  ¨ Kusimamia na kukagua shughuli za uchimbaji madini.

  Malengo ya Sera za Madini ni:

  § Kuhamasisha ugunduzi na uchimbaji madini.

  § Kudhibiti na kuboresha uchimbaji mdogo mdogo.

  § Kuhakikisha kuwa utajiri utokanao na madini unasaidia uchumi endelevu na maendeleo ya jamii, kuondoa au kupunguza athari mbaya ziwezazo kutokea kwa jamii na mazingira kutokana na shughuli za uchimbaji madini.

  § Kukuza na kuwezesha bidhaa zinazohusiana na madini kuwa na soko.

  § Kupunguza umaskini, hasa wa wachimbaji wadogo

  § Kukuza na kuendeleza Tanzania kama kituo cha vito Afrika

  Sheria na Udhibiti wa Sekta ya Madini

  Yanayojitokeza katika Sheria ya Madini 1998 ni yafuatayo:

  I. Haki ya kufanya biashara ya hati za madini.

  II. Kurahisisha na kuweka pamoja sheria za zamani za uchimbaji na biashara ya madini.

  III. Kuboresha haki ya umilikaji kwa kuondoa uwezo wa Wizara na kuweka kamati ya ushauri itakayaomshauri Waziri juu ya maamuzi ya kufanywa.

  § Kukuza uwazi
  § Taratibu za utoaji leseni zilizo za haki, zisizo na mizengwe na zisizobagua
  § Kusimamia mazingira


  Sheria ya Madini Tanzania inakataza kuhodhi habari za uvumbuzi mpya, kushikilia maeneo ya kiuchunguzi kwa lengo la kuyalangua, kuhamisha uwekaji bei na ukwepaji kodi. Motisha ya kifedha kwa anayetafiti ugunduzi na uchimbaji wa madini, ni pamoja na :

  § Msamaha wa kodi ya uingizaji nchini na VAT kwa vifaa na bidhaa muhimu hadi atakapoanza kuzalisha; baada ya hapo atalipia asilimia 5.

  § Kipunguzi cha uchakavu asilimia 10.

  § Kuhamisha mtaji na faida itokanayo na madini, na

  § Ushiriki wa Serikali kwa ridhaa.

  Urekebishaji wa Sekta za Madini

  Kama zilivyo Sekta nyingine za uchumi nchini, sekta ya madini iliingizwa kwenye marekebisho yaliyofanywa na Serikali miaka ya 80 na 90, yanayopendelea zaidi maendeleo ya sekta binafsi na kutawaliwa na nguvu za soko. Kwa msingi huu. Serikali inakaribisha ubia wa kuendeleza wenye shauku sekta binafsi na kuchochea kukua kwa uchumi. Kutokana na mabadiliko haya, jukumu la Serikali limebadilika, kutoka kuwa mmiliki na mwendeshaji na kuwa anayetoa sera zilizo wazi, kuhamasisha uwekezaji binafsi na kusaidia wawekezaji.

  Marekebisho haya ni kwa mujibu wa Sera ya Madini Tanzania 1997, Sheria ya Madini 1998, na Vivutio vya Kumotisha 1998.

  Vyama vya Kitaalam

  Chama cha Wasafirishaji Madini Nje Tanzania

  Chama cha Kijiolojia Tanzania.
   
 8. mzalendokweli

  mzalendokweli JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 578
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Alaf bado mnasema na ccm tutaondokana na umasikini..labla miaka mingapi ijayo?wao ndo wanendelea kua matajir mbaya zaid mabilion wanaficha uswis.
  Yan nimesoma hyo nimepata hasira sana. Nchi yenye hayo yote tunafanana hv?kweli huu si upuuzi huu?
   
 9. S

  SPANERBOY UDZUNGWA JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 623
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  hapa tunahitaji raisi ambae ni creative bila ivyo hatufiki popote
   
 10. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Hapa kuna takwimu za uzalishaji wa dhahabu Tanzania kwa miaka 11 iliyopita.

  [TABLE="class: grid, width: 500"]
  [TR]
  [TD]Mwaka[/TD]
  [TD]Kilo[/TD]
  [TD]Ounce[/TD]
  [TD]Average price
  $/ounce[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]2001[/TD]
  [TD]30,090[/TD]
  [TD]962,880[/TD]
  [TD]271.04[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]2002[/TD]
  [TD]43,320[/TD]
  [TD]1,386,240[/TD]
  [TD]309.73[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]2003[/TD]
  [TD]48,018[/TD]
  [TD]1,536,576[/TD]
  [TD]363.38[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]2004[/TD]
  [TD]48,178[/TD]
  [TD]1,541,696[/TD]
  [TD]409.72[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]2005[/TD]
  [TD]52,276[/TD]
  [TD]1,672,832[/TD]
  [TD]444.74[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]2006[/TD]
  [TD]47,000[/TD]
  [TD]1,504,000[/TD]
  [TD]603.46[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]2007[/TD]
  [TD]40,193[/TD]
  [TD]1,286,176[/TD]
  [TD]696.39[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]2008[/TD]
  [TD]36,434[/TD]
  [TD]1,165,888[/TD]
  [TD]871.96[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]2009[/TD]
  [TD]40,000[/TD]
  [TD]1,280,000[/TD]
  [TD]972.35[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]2010[/TD]
  [TD]35,600[/TD]
  [TD]1,139,200[/TD]
  [TD]1224.54[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]2011[/TD]
  [TD]40,400[/TD]
  [TD]1,292,800[/TD]
  [TD]1571.52[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Bei ya dhahabu inazidi kupanda. Ilifikia kiwango cha juu $1781 tarehe 28 Februari, na hivi sasa ni around $1600.

  laiti Taifa lingefaidika kikamilifu na dhahabu hii!


  Iwapo wakati wanafanya appraisal ya kuanzisha miradi bei ya dhahabu ilikuwa chini hivyo, na bado wakafanya projection ya faida wakaona inalipa, kisha bei inapanda kiasi kikubwa hivi Makampuni hayo yanafaidi kweli.
   
 11. N

  NANKY Member

  #11
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ccm is a company being driven by richest share holders who intend to destroy our nation,future and destiny. there we are now alarmed by their doings therein we now not ready to see this,M4C FOREVER:dance:
   
Loading...