Soma majibu ya ovyo ya customer care wa kampuni kubwa ya simu Tanzania

C.T.U

JF-Expert Member
Jun 1, 2011
5,070
3,718
juzi nikiwa katika restaurant moja kati kati ya jiji walikuja wadada wawili wakaanza kuongea kuhusu mitandao ya simu
sasa katika kuongea yule dada akaanza kulalamika anamsimulia mwenzake kuhusu mkasa wa kampuni moja ya simu ambayo wao wanadai ndio ina wateja wengi tanzania hii
akawa anasema alikuwa ana matatizo katika mtandao wake wa blackberry messenger hivyo basi akapiga customer care kuuliza kuwa kwanini hapati huduma hiyo ilhali amekwisha recharge?
Jibu alilopea dada yule na yule dada a customer care ilinifanya mie mwenyewe niliyekuwa nakunywa juice kidogo inipalie kwa jibu ambalo yule dada amepewa

huwezi amini yule customer care alimwambia yule dada kuwa simu yake imeoza kwa kweli nilikuwa kama lowassa yaani nilihuzunishwa sana , sikitishwa sana na fedheheshwa sana

sasa nikajiuliza kama yule dada kajibiwa vile basi si ajabu yule customer care ndio tabia yake na sio yeye tu ma customer care wengi ndio tabia yao ya majibu ya ovyo

nikasema huu mjadala nije niwape wadau najua wadau mtakuwa mmekutana na majibu ya ajabu ila mmeamua kukaa kimya

hivyo basi kama ume experience chochote kuhusu hawa customer care katika shughuli zako za kila siku hebu share na sisi na najua wenye makampuni wapo hapa na wanaona hivyo basi wakiona malalamiko ya wateja wao watajua kuwa wameajiri watu wa aina gani

nawasilisha
 
Nakubaliana na wewe japo mie sikujibiwa mbovu kiasi hicho ila sikuridhishwa na majibu ya dada mmoja pale airtel baada ya kuwa nimeweka fedha ktk cm yangu na baada tu ya muda mfupi wala sijapiga cm salio hakuna!

Nilipouliza nikaambiwa nilikuwa na mkopo! Nikasema hata kama nilikopa basi katika hiyo let say 2000 kateni balance iwepo na siyo 0 kabisa! Baada ya kuwa mkali wakakata cm na nilipo jaribu kupiga tena nikawekewa mziki na nikajulishwa kwamba cm nayopiga ikipokelewa itachajiwa.

Ki msingi nilikerwa sana na huyo dada. Yaonekana ajira yake ina utata! Nimesha kutana na kadhia hiyo pia Tigo kwa namna tofauti lakini kiwango cha kero ni kilekile ila kwa kuwa hatuna pa kulalamikia basi tuu tunaishia kutupa line kapuni au inakuwepo tuu kwa kupigiwa si ku recharge!!
 
Mkuu kama viongozi wana hisa kwenye hizo kampuni ya cmu utategemea nini..? Angalia Rwanda walivyo na heshima.. Juzi juzi kampuni moja kubwa 2 ya cmu imeponea chupuchupu kutimuliwa kule.. Wish 2ngempata Kagame wetu hapa..
 
customer kero 'care' za makampuni ya cm ni kichefuchefu tupu hasa ukiwa na tatizo kubwa au maswali mengi mimi cku hz nimeacha kabisa kuwapigia nipatapo shida
 
Ubaya ni ubaya hata ukimpata mwenzio. Kama ni wewe ungesubiri mpaka ukukute wewe ndio ulalamike ?
mimi sitalalamika nitachukua hatua kwa kwenda sehemu husika, sijui umenisoma mdada! wadandia treni kwa mbele wewe,utachan........... mthamba
 
Hizi ni habari za upande mmoja ambazo hatuna taarifa za upande wa pili. Kutoa hukumu kwa kutumia taarifa za upande mmoja ni kutoutendea haki upande wa pili. Je huyo customer care alianza tu from nowhere kusema simu yake imeoza? Au naye huyo mdada aliyekuwa anatoa hiyo story mdomo wake ni mchafu??????????????
 
Kweli Likasu mwambie, kwani hawa jamaa wana kera kweli,me ilishatokea mpaka nikaenda kwenye ofc mojawapo na nilileta zaga ile mbaya mpaka wakanipeleka chumba cha ndani na kunipooza kwa maneno ya upole lakini hata waliokuwepo pale walifurahia.

Imagine mtu unaweza hata kwenda kwenye ofc zao na ukawekwa kwenye foleni na hata inapofika zamu yako bado unapata huduma mbovu. Wana unyanyasaji usio na msingi sijui ni kwa sababu huwaoni unapowapiga simu.

Cha ajabu ni kweli eti kuna baadhi unapopiga customer care eti unachajiwa.wezi tu hawa. Na wengine wamefanya simu zetu ndio za matangazo,Imagine unampigia mtu simu wanaanza na matangazo yao,sijui pata ofa kupiga nje kwa sijui nini then ndio simu inaanza kuita.

Hivi TCRA mpo wapi?
 
Nahisi huyo mtu wa customer care amekopi na kupesti maneno ya makonda wa daladala...
 
Hizi ni habari za upande mmoja ambazo hatuna taarifa za upande wa pili. Kutoa hukumu kwa kutumia taarifa za upande mmoja ni kutoutendea haki upande wa pili. Je huyo customer care alianza tu from nowhere kusema simu yake imeoza? Au naye huyo mdada aliyekuwa anatoa hiyo story mdomo wake ni mchafu??????????????

Mie alipokea halafu akaendelea kupiga story na mwenzake mmoja hadi nikakata simu!:smash:
 
mimi nilifikiri imekutokea wewe kumbe ulikuwa una sikiliza umbea wa kina dada!

ngoja nikuulize swali moja mdogo wangu (sorry kwa kukuita mdogo wangu maybe umenizidi umri ila nakuita mdogo wangu kwa kuangalia akili yako since una akili ya kitoto)

hivi information zote na thread zote zinazoandikwa au habari zote unazozipata yule ambaye amekuja kukwambia ni yeye imemtokea ? bado hujajua kuwa information unaweza pata kwa kuona, au kwa kusikia?
 
thanx kaka!leo umenisaidia kujua kuwa umbea ni source of information but is not realiable to expose in public

Tatizo la wabongo kutokujua na kutojishughulisha kujua haki zao. Ni haki ya mteja kupata msaada kama atakuwa na tatizo kwenye simu yake. Na ndio maana hizi namba za huduma kwa wateja nyingi unapiga bila kulipishwa hela (bure).

Sasa kama amejibiwa vibaya na mtoa huduma na pia tatizo lake halijashughulikiwa, alichukua hatua gani? Kulalamika tuu hakusaidii sana kama mteja mwenyewe hachukui hatua. Simu zote zinazopigwa customer care zinarekodiwa na ukiwa na malalamiko tu yakifika kwa wahusika ile simu inatafutwa na kusikilizwa.

Hii inanikumbusha matatizo ya daladala kukatisha ruti na abiria wanakubali kushuka na kwenda nyumbani kulalamika vijiweni.
 
Back
Top Bottom